Singida
Taasisi ya Utafiti wa
Kilimo Tanzania (TARI) na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele(NARI) kwa
kushilikiana na Bodi ya Korosho Nchini pamoja na Serikali ya Mkoa wa Singida imeendesha mafunzo maalum
ya kilimo bora cha zao la Korosho ili kufufua zao hilo ambalo limeonyesha
kusitawi kwa kiwango kikubwa katika Mkoa
huo kutokana na hali ya kijografia ya eneo hilo.
Akiongea kwa
niaba ya ujumbe maalum
wa Taasisi hizo, ofisini kwa Mkuu
wa MKoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi,
Afisa Mfawidhi wa Bodi ya Korosho Kanda ya Kati Bw.Ray Mtangi amesema lengo kuu
la mafunzo hayo ni kuwawezesha wakulima
kuingia sokoni wakiwa na Korosho zenye
uboro unaokubalika katika masoko
ya kimataifa ili kupata bei nzuri.
Amesema mafunzo hayo
yanatolewa katika wilaya zote za Mkoa wa Singida ambapo kwa sasa yameanzia
Wilayani Manyoni na yanasambazwa katika wilaya
zote kwa kuwa utafiti umebaini
kuwa eneo kubwa la mkoa huu linafaa
kwenye kilimo cha zao la Korosho.
“Serikali imeona ni muhimu kuelekeza nguvu zake katika Mkoa huu kwa kuwa
kilimo cha zao la Korosho kitakuwa
ni mkombozi wa kweli kwa wananchi wa Singida” alisisitiza Mtangi
Pia Dkt.Geradina Mzena
ambaye ni Mratibu wa zao Korosho nchini amewapongeza wadau mbalimbali ambao
wameonyesha mwitikio mkubwa kutoka sehemu mbalimbali nchini kuhudhuria
mafunzo hayo ambapo amesema Serikali
imejipanga kuhakikisha kuwa mafunzo hayo
yatatolewa katika kanda mbalimnali hapa nchini ili kuleta mageuzi
makubwa katika sekta ya kilimo kwa ujumla
Aidha ameipongeza Serikali
ya Mkoa wa Singida kwa kuwa na mkakati
kabambe wa kuanzisha mfumo wa
mashamba makubwa ya pamoja ya bega kwa bega ambayo yameifanya Singida kuwa
miongoni mwa mikoa ambayo ni
wazalishaji wakuu wa zao hilo
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt.Rehema Nchimbi amefafanua
kuwa hadi sasa kuna takribani ekeli
26,000 za zao la korosho ambazo zimelimwa katika Wilaya ya Manyoni, Ikungi na
Itigi ambapo amesema kwa sasa serikali imesitisha ugawaji wa mashamba ya
pamoja kwenye wilaya ya Manyoni
kwa vile
tayari eneo kubwa limetolewa
“Napenda kufafanua
kwamba kwa sasa tumesitisha
ugawaji wa mashamba ya Manyoni
kwa vile eneo lote la mkoa wetu linafaa kwa kilimo hicho hivyo wananchi
wanaopenda kulima watapatiwa maeeneo
hayo sehemu nyingine na kwamba mashamba
hayo ni maalum kwa ajili ya zao hilo pekee” aliongeza Dkt. Nchimbi
Pia amesema Mkoa wa Singida
ulikuwa ukisifika kwa sifa ya ukame lakini jitihada zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano kupitia tafiti mbalimbali zilifanya utafiti
wa zao la kudumu katika Mkoa huu kwa
kuwa kulikuwa na viashilia vya mikorosho mizee hivyo ndio vilikuwa viashilia
vya kugundua kuwa Korosho inastawi Singida.
Mkurugenzi wa Idara ya
Maendeleo ya Mazao kutoka Wizara ya Kilimo Nyaswebwa Chimagu amesema Wizara
itaendelea kutoa Sera ambazo zitatasaidia
kuleta mapinduzi ya sekta ya
kilimo ili kuhakikisha kiliomo kinachangia kwenye uchumi wa Taifa na
kwamba wananchi wajitokeze kwa wingi
kwenye zoezi la uelimishaji linaloendelea.
"Wito wetu kama
Serikali na Wizara kwa ujumla watu waje wajifunze katika maeneo haya juu ya
kilimo cha korosho" alisisitiza
Chimagu
No comments:
Post a Comment