Manyoni
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi ametembelea
Kituo cha Wazee kwenye Kijiji cha Sukamahela
Wilayani Manyoni, Mkoani Singida na kuwapatia
mahitaji ya vyakula yenye thamani ya takribani shilingi milioni mbili
ikiwa ni zawadi ya Mkoa kwa ajili ya maadhimisho ya mwaka huu ambayo hufanyika Oktoba Mosi kila mwaka.
Akizungumza na Wazee waishio katika Kituo hicho, amesema mageuzi na mapinduzi ya kiuchumi yaliofanywa na Selikari ya Awamu ya Tano ni makubwa ambayo yanalenga kuwanufaisha wananchi wake katika umri wa sasa hadi wanapokuwa wazee.
Ameyataja baadhi ya
maendeleo hayo kuwa ni pamoja na ujenzi wa Reli ya Mwendokasi, Ujenzi wa
Bwawa la Mwalimu Nyerere la kufua Umeme,
utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi, Ujenzi wa Vituo vya Afya na
ununuzi wa ndege.
"Ndugu zangu tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu
na kumshukuru baba yetu Magufuli kwa
kuwa haya yote ni kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi yetu na kunufaisha kila
mtu pamoja na Wazee wa sasa na wajao.
"Alisema Mkuu wa Mkoa.
Pia, aliwaomba Watumishi wa Mungu kuwaombea Wazee ambapo
alisisitiza kuwa Wazee ni baraka na
kwamba tunajifunza mambo mengi kutoka
kwao.
"Familia zenye Wazee zina baraka na mimi nataka
Mkoa wa Singida uwe na historia ya kuwa na Mzee mwenye miaka mingi kuliko wote
duniani" aliongeza Dkt.Nchimbi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wazee wasiojiweza Ndugu,
Andrea Yohana alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa zawadi ya mbuzi, nyama ya Ng'ombe
Michele, Sukari pamoja na sabuni ya kufulia ya unga.
"Tunawashukuru kwa zawadi hii mliyotupatia Mungu
awabariki na kuwaongezea mlipotoa na siku nyingine mtukumbuke zaidi"
aliongeza
No comments:
Post a Comment