Friday, May 25, 2018

ZAO LA ALIZETI LATANGAZWA RASMI KUWA ZAO MKAKATI KWA MKOA WA SINGIDA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (mwenye beseni la Alizeti) akifurahi na wakulima wa kijiji cha Mangida Kata ya Msange wilayani Singida mara baada ya kuvuna kitaalamu Alizeti iliyopandwa kwa mbegu bora ya Hysun 33 wakati wa siku ya Mkulima kijijini Mangida, Shughuli iliyo andaliwa na shirika la FAIDA MALI Singida.

WAKULIMA  Wilayani Singida wametakiwa  kutumia fursa ya kulima mbegu bora ya Alizeti aina ya Hysun 33 (Chotara) ili iwe mkombozi katika kuboresha maisha yao na maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Mhe. Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi katika hafla ya Siku ya Mkulima iliyofanyika katika kijiji cha Mangida Kata ya Msange mkoani Singida, iliyoratibiwa na Shirika (NGO's) la Faida Mali na kusisitizia kuachana na kutumia mbegu zisizo na tija alizoziita mbegu hasara. 

Dkt. Nchimbi alisema Wakulima hawana budi kuhakikisha wanalima kilimo chenye tija kwa kulima mbegu bora ya Alizeti ya Hyssun 33 (chotara) ambayo itawasaidia  wakulima hao kulima eneo dogo na kupata mazao ya kutosha ukilinganisha na mbegu hasara zinazotumia eneo kubwa kwa kuzalisha mazao machache.

Ni mpango mkakati wa Tanzania kuhakikishi kwamba tunajitosheleza kwa mafuta yetu ya kula kutoka viwanda vyetu  vya ndani, hivyo ni lazima tuzalishe malighafi zakutosha, hivyo ni lazima tuzalishe Alizeti ya kutosha ili kupata mafuta ya kula ya kutosha” alisema Dkt. Nchimbi

Aliongezea kuwa Viwanda vyetu vya Mkoa wa Singida vinauwezo wa kuzalisha mafuta ya kula ya kutosha hapa nchini Tanzania akitolea mfano wa viwanda vya Sukari vyenye uwezo wa kuzalisha sukari ya kutosha mahitaji ya ndani ya nchi.

"Iwapo kiwanda kimoja cha sukari kinauwezo wa kuzalisha sukari ya kutosheleza Tanzania sembuse viwanda vyetu vya kati vilivyopo mkoani Singida pamoja na kiwanda kikubwa cha kusindika mafuta ya Alizeti cha Mount Meru Millers kilichopo Singida"  Alisema Dkt. Nchimbi.


AIDHA, DKT. REHEMA NCHIMBI AMALITANGAZA RASMI ZAO LA ALIZETI KUWA NI ZAO MKAKATI NAMBA MOJA KWA MKOA WA SINGIDA AKIYATAJA MAZAO MKAKATI MENGINE YA PAMBA, KOROSHO, VITUNGUU, KUKU NA KUSISITIZA KUWA MKOA WA SINGIDA NI MIONGONI MWA WAZALISHAJI WAKUBWA WA MBEGU ZA PAMBA NA KUPEWA HESHIMA YA UZALISHAJI WA MBEGU ZA PAMBA

"Kuanzia leo hii na hasa baada ya kuona mbegu nzuri ya Hysun 33 (Chotara), mazao mazuri na bora natamka kwamba zao la Alizeti kwa mkoa wa Singida sio zao la kawaida tuu ni zao Mkakati namba moja" Dkt. Nchimbi

Aidha, alisisitiza kuwa, zao lolote linapotangazwa kuwa zao mkakati lazima kila mtu ashiriki katika kulisimamia na kulitetea, kulihakikishia usalama wa ardhi yenye udongo rafiki, maji na kulilinda kwa namna yoyote. 

Hivyo, Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameagiza kila mmoja kuwa ni Afisa Ugani wa Alize, mkuu wa mkoa ni Afisa Ugani wa Alizeti, mkuu wa wilaya Afisa Ugani wa Alizeti, maafisa kilimo kuwa Afisa Ugani wa Alizeti, watu wa vyama vya ushirika maafisa Ugani ili kuondoa hali ya kulaumiana kuwa kuna mmoja alikosea sehemu na kupelekea kutofanya vizuri, 

Hata hivyo akawaomba viongozi wa Dini mbalimbali wa Mkoa wa Singida kuwa maafisa Ugani wa Alizeti ili kuwa na mavuna makubwa zaidi katika kilimo cha Alizeti, zao mkakati namba moja kwa mkoa wa Singida.


Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akifurahia mavuno ya Alizeti yaliyopandwa na wakulima wa kijiji cha Mangida Kata ya Msange wilayani Singida mkoa wa Singida kwa mbegu bora ya Hysun 33 (Chotara) wakati wa siku ya mavuno ya Alizeti Mei, 2018.


Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiliangalia zao la Alizeti lenye tija wakati wa uzindua rasmi wa mavuno ya Alizeti yaliyopandwa na wakulima wa kijiji cha Mangida Kata ya Msange wilayani Singida mkoa wa Singida kwa mbegu bora ya Hysun 33 (Chotara) wakati wa siku ya mavuno ya Alizeti Mei, 2018.

 Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizugumza na wananchi, akiwapongeza wakulima wa zao la Alizeti na kuwatakia kheri katika mavuno yao na kutamka rasmi zao la Alizeti kuwa zao mkakati namba moja kwa mkoa wa Singida kwa kutumia mbegu bora ya Hysun 33 (Chotara) wakati wa siku ya mavuno ya Alizeti hafla iliyofanyia katika kijiji cha Mangida Kata ya Msange wilayani Singida mkoa wa Singida.

 Dkt. Nchimbi alihitimisha hotuba yake kwa kuhimiza mbegu ya Hysun 33 (Chotara) ni vyema izalishwe nchini kwetu Tanzania hasa mkoa wa Singida ili iwe rahisi kupatikana na kusema kuwa kisayansi Mbegu ikizalishwa katika udongo mwenyeji inafanya vizuri sana katika udongo mwenyeji.

KWA UPANDE WAKE, Mratibu wa Faida Mali Christopher Mkondya alisema lengo la Kampuni hiyo ni kuboresha mfumo mpya wa masoko katika zao la Alizeti Mkoani Singida.

‘’Kampuni ya Faida Mali inashughulika na Halmashauri za Mkoa wa Singida ambazo ni Halmashauri za Singida, Mkalama, Ikungi na Iramba ambapo lengo lake ni kuwanufaisha wakulima 32,000 wa zao la Alizeti’’

‘’Malengo mahsusi ya Mradi huu ni kuhamasisha wakulima kulima mbegu bora chotara ya Alizeti, Mkulima wa Singida aweze kupata huduma mbalimbali ili kumwezesha kuzalisha Alizeti kwa kiwango bora, awe na bima ya mazao, kupata mikopo toka taasisi za kifedha kama vile kukopa matrekta, halikadhalika kuwajengea uwezo kwenye vikundi au ushirika’’ alisema Mkondya

Alisema mbegu bora chotara ya Alizeti (hyssun 33) ambazo eka moja hutoa magunia 18 na mbegu zake zinamafuta mengi"

‘’Mbegu ya hyssun 33 inatoa mbegu nyingi ya Alizeti ukilinganisha na mbegu hasara  kwani kwa ekari moja hutoa magunia kuanzia 16 hadi 18 wakati mbegu hasara ilikuwa ikitoa magunia kuanzia 3 hadi 5’’ alisema Mkulima.

Kwa upande wa uzalishaji mafuta mbegu ya hyssun 33 hutoa asilimia 40 ya ubora wa mafuta wakati mbegu hasara ilikuwa ikitoa asilimia 16 ndiyo maana tunaita hyssun 33 ni mkombozi wa Mkulima.

Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akisalimiana na Mkurugenzi wa Faida Mali Bw. Tom Sillayo mara baada ya kuwasili shambani katika siku ya mavuno ya Alizeti iliyoratibiwa na Shirika la Faida Mali mkoa wa Singida ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya Tano ya viwanda inayoongozwa na Mhe.Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 


Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akisalimiana na mratibu wa shirika (NGO's) Faida Mali mkoa wa Singida, Bw. Christopher Mkondya mara baada ya kuwasili shambani katika siku ya mavuno ya Alizeti iliyoratibiwa na Shirika la Faida Mali mkoa wa Singida ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya Tano ya viwanda.

 Bw. David Vallence Yamagaji kutoka kampuni ya Bytrade wasambazaji wa mbegu aina ya Hysun 33 (Chotara) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Singida mara baada ya kuwasili shambani kwaajili ya mavuno ya Alizeti zao mkakati namba moja kwa mkoa wa Singida 2018.


Wakulima wa kijiji cha Mangida Kata ya Msange wakimpokea Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida mara baada ya kuwasili shambani kwa ajili ya mavuno ya Alizeti kijijini hapo.

 Wakulima wa kijiji cha Mangida Kata ya Msange wakimsindikiza shambani Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida mara baada ya kuwasili shambani kwa ajili ya mavuno ya Alizeti kijijini hapo.

 Sehemu ya Shamba la Alizeti 

 Wakulima wa kijiji cha Mangida Kata ya Msange wakimsindikiza shambani kwenye mavuno ya Alizeti Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi kwa ajili ya mavuno ya Alizeti.
 Mkulima akimkabidhi kisu na beseni (vifaa vya kuvunia Alizeti) Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa ajili ya kuzindua rasmi mavuno ya Alizeti kijijini hapo.
 Mkulima akimkabidhi kisu na beseni (vifaa vya kuvunia Alizeti) Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Elias Tarimo kwa ajili ya kuzindua rasmi mavuno ya Alizeti kijijini hapo.
 Bw. David Vallence Yamagaji kutoka kampuni ya Bytrade wasambazaji wa mbegu aina ya Hysun 33 (Chotara) akiwaonyesha wakulima wa zao mkakati la Alizeti kwa mkoa wa Singida akiwemo Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ambaye ndiye mgeni rasmi akiambatana na mkuu wa wilaya ya Singida Bw. Elias Tarimo na timu kutoka sekretarieti ya mkoa jinsi ya kuvuna kitaalama zao hilo wakati wa sherehe za siku ya mavuna yaliyofanyika katika kijiji cha Magida Kata ya Msange wilayani Singida mkoa wa Singida.

Bw. David Vallence Yamagaji kutoka kampuni ya Bytrade wasambazaji wa mbegu aina ya Hysun 33 (Chotara) akiwaonyesha wakulima wa zao mkakati la Alizeti kwa mkoa wa Singida akiwemo Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ambaye ndiye mgeni rasmi akiambatana na mkuu wa wilaya ya Singida Bw. Elias Tarimo na timu kutoka sekretarieti ya mkoa jinsi ya kuvuna kitaalama zao hilo wakati wa sherehe za siku ya mavuna yaliyofanyika katika kijiji cha Magida Kata ya Msange wilayani Singida mkoa wa Singida.


Bw. David Vallence Yamagaji kutoka kampuni ya Bytrade wasambazaji wa mbegu aina ya Hysun 33 (Chotara) akielezea jinsi ya kuvuna Alizeti kitaalamu wakati wa sherehe za siku ya mavuna yaliyofanyika katika kijiji cha Magida Kata ya Msange wilayani Singida mkoa wa Singida.


Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizindua rasmi mavuno ya Alizeti yaliyopandwa na wakulima wa kijiji cha Mangida Kata ya Msange wilayani Singida mkoa wa Singida kwa mbegu bora ya Hysun 33 (Chotara) wakati wa siku ya mavuno ya Alizeti Mei, 2018.



 Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Singida Bw. Elias Tarimo akishiriki kwenye mavuna ya Alizeti mara baada ya kupata utaalama jinsi ya kuvuna zao hilo wakati wa sherehe za mavuna yaliyofanyika katika kijiji cha Magida Kata ya Msange wilayani Singida mkoa wa Singida.

Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Bw. Slauslaus B. Choaji akishiriki katika mavuno ya Alizeti.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Singida Bw. Eliya Digha akishiriki katika mavuno ya Alizeti.
Mratibu wa shirika lisilo la kiserikali (NGO's) Faida Mali mkoa wa Singida, Bw. Christopher Mkondya akishiriki katika mavuno ya Alizeti.

Wakulima wa zao la Alizeti kijiji cha Magida Kata ya Msange wilayani Singida mkoa wa Singida walioshiriki kwenye sherehe za mavuno.

Wakulima wa zao la Alizeti kijiji cha Magida Kata ya Msange wilayani Singida mkoa wa Singida wakitoa burudani mbele ya mgeni rasmi. 

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Elias Tarimo akizungumza na wakulima wa zao la Alizeti kijiji cha Magida Kata ya Msange wilayani Singida mkoa wa Singida walioshiriki kwenye sherehe za mavuno. 

 Mjumbe kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Singida akizungumza jambo wakati wa sherehe za mavuna ya Alizeti katika kijiji cha Magida Kata ya Msange wilayani Singida mkoa wa Singida.

Mjumbe kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Singida akizungumza jambo wakati wa sherehe za mavuna ya Alizeti katika kijiji cha Magida Kata ya Msange wilayani Singida mkoa wa Singida.

Mkurugenzi wa Faida Mali Bw. Tom Sillayo akizungumza jambo na kutoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi wakati wa sherehe za mavuna ya Alizeti katika kijiji cha Magida Kata ya Msange wilayani Singida mkoa wa Singida.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Singida Bw.Bw. Eliya Digha akizungumza jambo na kutoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi wakati wa sherehe za mavuna ya Alizeti katika kijiji cha Magida Kata ya Msange wilayani Singida mkoa wa Singida. 

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Elias Tarimo akizungumza jambo wakati wa sherehe za mavuna ya Alizeti katika kijiji cha Magida Kata ya Msange wilayani Singida mkoa wa Singida.  



Mkurugenzi wa Faida Mali Bw. Tom Sillayo akiteta jambo na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi wakati wa sherehe za mavuna ya Alizeti katika kijiji cha Magida Kata ya Msange wilayani Singida mkoa wa Singida. 

Mwenyekiti wa kikundi cha wakulima wa Alizeti katika kijiji cha Mangida Kata ya Msange akizungumza jambo na kutoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi wakati wa sherehe za mavuna ya Alizeti katika kijiji cha Magida Kata ya Msange wilayani Singida mkoa wa Singida.  

      Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Bw. Stanslaus B. Choaji                            akizungumza jambo wakati wa sherehe ya mavuno ya Alizeti.

  Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na wakulima wakati wa                                                 sherehe ya mavuno ya Alizeti.

Wakulimawa zao la Alizeti wakimpongeza Mhe. Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi mara baada ya kuzungumza wakati wa sherehe ya mavuno ya Alizeti. 

 Wakulimawa zao la Alizeti wakimpongeza Mhe. Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi mara baada ya kuzungumza wakati wa sherehe ya mavuno ya Alizeti.

Wakulima wa kijiji cha Mangida 



Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi wakisherekea kwa pamoja na wadau na washiriki waliohudhuria kwa kucheza muziki wenye asili ya Kinyaturu wakati wa sherehe ya mavuno ya Alizeti wilayani Singida.

Imetolewa na:
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida.
Mei, 2018

No comments:

Post a Comment