Sunday, May 27, 2018

RC SINGIDA, DKT. REHEMA NCHIMBI AFANYA ZIARA KUKAGUA KILIMO CHA PAMOJA CHA KOROSHO WILAYANI MANYONI

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amefanya ziara ya kukagua kilimo cha pamoja cha zao la Korosho katika kijiji cha Masigati Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kwa ajili ya kuendelea kuhamasisha wakulima mkoani Singida kulima zao hilo mkakati la Korosho pamoja na mazao mengine mbalimbali kwa wingi kwa njia ya kitaalamu  ambayo yatawafanya wakue kiuchumi, mkoa na kitaifa kwa ujumla.

Dkt. Nchimbi amefanya ziara hiyo hivi karibuni Mei, 2018 wilayani Manyoni katika kijiji cha Masigati palipotengwa shamba lenye ukubwa wa ekari 10,000 na Serikali ya kijiji Masigati kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manyoni mkoani Singida pamoja na Sekretarieti ya mkoa wa Singida, shamba mahususi kwa kilimo cha Korosho.

Aidha, amejionea zao hilo lilivyopandwa na wakulima kwa njia ya kitaalamu na kuwataka wakulima kuendelea kutii maagizo ya Serikali kwa kulima zao hilo la biashara na chakula ambayo yatabadili mfumo wa maisha yao.

Akizungumza na baadhi ya wakulima waliohudhulia kwenye ziara hiyo akiwa shambani, Dkt. Nchimbi alisema kuwa kwa kilimo hiki cha pamoja cha Korosho katika eneo hilo ambalo lililotengewa zaidi ya ekari 10,000 akisisitizia nidhamu ya pamoja, uwajibikaji wa pamoja na hakutaruhusiwa kwa mkulima yeyote yule miongoni mwa wakulima hao awe chanzo cha kuzalisha wadudu au uchafuzi wa mazingira. 

"Iwapo mwenzetu mmoja hatapalilia kwa wakati ambao tunatakiwa kupalililia atatuponza maana mimea yake itazalisha wadudu na sisi hatuko tayari kuwa na mtu ambaye atatuzalishia wadudu." alisema Dkt. Nchimbi

Aidha Dkt. Nchimbi ameagiza kwa yeyote yule aliyechukuwa eneo katika shamba hilo la kulima Korosho ajipime kwanza kama ataweza kuwa na nidhamu ya pamoja na uwajibikaji katika kilimo hicho, vinginevyo watu hao wasifurahie tuu kuja kununue eneo la kulima Korosho na kuwataka waache kabisa kununua eneo kama hatoweza kulisimamia ipasavyo. 

Dkt. Nchimbi, amewataka Uongozi wa Serikali ya kijiji cha Masigati kutunga sheria ndogo zitakazoweza kusimamia misingi, malengo na miongozo mbalimbali ili kufikia lengo kuu la kuwa na kilimo cha pamoja chenye tija.


Dkt. Nchimbi aliagiza kuwa, wale wote walionunua maeneo katika shamba hilo la pamoja kwa kilimo cha korosho ni vyema kusafisha maeneo yao kwa wakati vinginevyo watanyang'anywa. "Eneo hili ni kwaajili ya kilimo cha pamoja cha Korosho, Serikali halikutoa  eneo hili ili liwe pori, ukishindwa kusafisha tutakunyang'anya" Alisisitizia Dkt. Nchimbi

Kwa upande wake Afisa kilimo wa wilaya ya Manyoni alisema kuwa wanategemea mkulima ambaye atahudumia kwa karibu zaidi kwa kufuata masharti yaliyoelekezwa na Afisa Ugani  ili kumpatia tija na kumuwezesha kupata matunda makubwa na kuwataka wale waliochelewa kuandaa shamba kwa ajili ya msimu ujao kufika mapema shambani hasa wale walionje ya mkoa wa Singida ili kupanda kwa kwa pamoja na kupalilia kwa pamoja.

"Kuna kipindi maalum cha kupalilia kipindi ambacho kinakuwa na ushindani mkubwa wa virutubisho kati ya mmea na mimea mingine, mimea mingine ikiwa mikubwa hupelekea kuchukua chakula kingi zaidi na kupelekea madhara ya kuuharibu mkorosho" Alisema Afisa Kilimo Wilaya Manyoni.

Katika msimu huu wa kilimo Halmashauri ya wilaya ya Manyoni ililenga kuzalisha miche 121,917 (sawa na wastani wa ekari 4064). Miche iliyosambazwa bure kwa wakulima ni 119,619 (sawa na wastani wa ekari 3987). Miche hii imepandwa na wakulima katika kata na vijiji mbalimbali ikiwemo na shamba la Masigati.


 Mhe. Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba) akisalimiana na mwenyekiti wa kijiji cha Masigati wilayani Manyoni.
 Mkuu wa wilaya ya Ikungi ambaye pia ni kaimu Mkuu wa wilaya ya Manyoni Mhe. Miraji Mtaturu akisalimiana na mkulima (mwenye kofia ya njano) wa kijiji cha Masigati  wilayani Manyoni.
  Mkuu wa wilaya ya Ikungi ambaye pia ni kaimu Mkuu wa wilaya ya Manyoni (wa kwanza kulia) Mhe. Miraji Mtaturu akifurahia jambo shambani Masigati.
  Mhe. Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na wakulima wa kilimo cha pamoja cha korosho katika kijiji cha Masigati wilayani Manyoni.
                Mhe. Mwenyekiti wa kijiji cha Masigati akizungumza jambo.
  Mhe. Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiongozana na baadhi ya maafisa na wakulima wa kilimo cha pamoja cha korosho katika kijiji cha Masigati ili kukagua maendeleo ya miche iliyopandwa wilayani Manyoni.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi ambaye pia ni kaimu Mkuu wa wilaya ya Manyoni Mhe. Miraji Mtaturu (mwenye shati la bluu) akikagua mche wa korosho  uliopandwa katika kijiji cha Masigati  wilayani Manyoni. 
Afisa Ugani wa wilaya ya Manyoni akiuelezea mche korosho uliochipua katika shamba la kilimo cha pamoja cha korosho katika kijiji cha Masigati wilayani manyoni. 
 Afisa Ugani wa wilaya ya Manyoni akielezea jamba kuhusu miche ya korosho iliyopandwa katika shamba la kilimo cha pamoja cha korosho katika kijiji cha Masigati wilayani manyoni. 
Mkurugenzi wa wilaya ya Manyoni Mhe. Sharles E. Fussi akitoa taarifa ya kilimo cha pamoja cha korosho katika kijiji cha Masigati pamoja na kazi zilizofanyika na zinazoendelea shambani na wilayani kwa ujumla.
  Mhe. Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba) akizungumza jambo mbele ya mche wa korosho aliyoupanda wakati wa uzinduzi wa shamba la kilimo cha pamoja cha korosho katika kijiji cha Masigati wilayani Manyoni.
 Mkuu wa wilaya ya Ikungi ambaye pia ni kaimu Mkuu wa wilaya ya Manyoni (wa kwanza kulia) Mhe. Miraji Mtaturu akizungumza jambo shambani Masigati.
 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba) akisisitiza jambo shambani Masigati.
Ziara shule ya msingi Masigati 
                                      Ziara shule ya msingi Masigati 
 Ziara shule ya msingi Masigati 
Mkuu wa shule ya msingi Masigati mwalimu Muungano Rajabu Iddy akiteta jambo na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi wakati wa ziara shuleni hapo.
Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiongea na mwanafunzi wa shule ya msingi Masigati wakati wa ziara shuleni hapo.
Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Masigati wakati wa ziara shuleni hapo. 
 Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimpa mwanafunzi mkono wa pongezi mara baada ya kumuombea (sala) wakati wa ziara shuleni hapo. 

KAZI ZINAZOENDELEA SHAMBANI HIVI SASA
  • Ukamilishaji wa ufyekaji wa shamba na kugawa kwa wakulima ambao bado hawajagawiwa mashamba yao.
  • Wakulima kuendelea na palizi pamoja na upogoleaji wa matawi kwenye miche ya mikorosho.
  • Kuweka miti ya kuzuia upepo kwenye miche ya mikorosho (staking).
Imetolewa na:
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Singida

No comments:

Post a Comment