Wakazi wa
Kijiji cha Ughandi B Singida Vijijini wamekabidhiwa rasmi
Mradi wa maji wenye ujazo wa Lita Elfu 90 na wametakiwa kutunza Mazingira na
vyanzo vya maji ili uweze kudumu kwa muda mrefu.
Hayo yamesemwa
leo na Msaidizi wa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa
2022 Emmanuel Ndege Chacha wakati wa uzinduzi wa Mradi wa maji unaomilikiwa na
Wakala wa maji na usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) ambapo aliwataka
wananchi kutunza mradi huo pamoja na
kuyalinda Mazingira kuzungukia vyanzo vya maji ili yaendelee kupatika kwa muda
mrefu.
Kabla ya kuzindua
Mradi huo kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru alibainisha baadhi ya kasoro
katika chanzo cha maji na taratibu za malipo hapo aliwataka kufanya marekebisho
hayo madogo huku wananchi wakiendelea kupata manufaa ya mradi huo.
Chacha
amezitaka kamati za maji za eneo hilo kuhakikisha wanatunza na kukarabati
miundombinu ya maji badala ya kusubiri RUWASA.
Hata hivyo
Kiongozi huyo amewataka Wahandisi kufuata maelekezo yaliyotolewa na Wizara ya
maji katika kutekeleza miradi hiyo.
Hata hivyo
amewataka RUWASA kuwa na kawaida ya kutoa taarifa kwa wananchi pindi
wanapofanya usafi au matengenezo ya miundombinu ya maji hayo ili kuondoa
usumbufu kwa wananchi.
Awali Meneja
wa RUWASA Mhandisi Athumani Mkalimoto amesema Mradi huo umekamilika na umeanza
kuhudumia wananchi wa eneo hilo.
Hata hivyo
Mhandisi amebainisha kwamba Mradi umeokoa kiasi cha Milioni 155.1 baada ya
kutumia gharama kiasi cha Tsh.Milion 410.4 ambapo ulitengewa bajeti ya Tsh.Milioni
565.5 mpaka kukamilika alieleza.
Aidha
Mhandisi Athumani ameeleza kwamba wananchi wapatao 5500 wa Kijiji cha Ughandi B
wamekuwa wakifaidika na uwepo wa Mradi huo.
Mwenge wa
Uhuru huo umekamilisha mbio zake katika Wilaya ya Singida baada ya kukagua na
kuzindua miradi mitano na programu tano ambazo Mwenge wa Uhuru zote
zilipitishwa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment