Mkurugenzi wa TIC Geoffrey Mwambe (wa kwanza kushoto) akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wa kwanza Kulia) katika kikao cha kumuaga, Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo na Mkuu wa Wilaya Mkalama Jackson Masaka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) Geoffrey Mwambe akiwashukuru viongozi wa Mkoa wa Singida kwa ushirikiano katika kikao kifupi cha kumuaga.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) Geoffrey Idelphonce Mwambe ametoa tahadhari
kwa wawekezaji wote wa nje na ndani ambao hawana nia njema na maendeleo ya
taifa kuwa hawana nafasi nchini na kwamba hawatapata fursa yoyote Tanzania.
Mwambe ametoa
tahadhari hiyo jana jioni katika kikao kifupi kilichoandaliwa na Mkuu wa Mkoa
wa Singida Dokta Rehema Nchimbi kwa ajili ya kumuaga rasmi Mkurugenzi huyo mara
baada ya uteuzi wake ambapo hapo awali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni.
Amesema kituo cha
uwekezaji kitashirikiana na wawekezaji wenye nia njema tu ila wale ambao
wanataka kujinuafiasha wao na kuliacha taifa bila faida yoyote hawatapewa fursa
yoyote ya kuwekeza nchini.
Mwambe ameongeza kuwa
atahakikisha kuwa wawekezaji wenye ubora na ambao uwekezaji wao unamgusa
mtanzania moja kwa moja wanapatikana hasa wale ambao watasaidia kutoa ajira kwa
wananchi na kukuza uchumi.
“Nina imani na
wawekezaji wadogo ambao nitajitahidi kuwaunganisha na wawekezaji wakubwa ili
wakue na wajenge uchumi wa taifa itawasaidia pia hao wawekezaji wadogo watapata
uzoefu na hivyo kuwa wawekezaji wakubwa”, amesema.
Mwambe ameongeza kuwa
hatausahau Mkoa wa Singida kwenye fursa za uwekezaji na kuongeza kuwa mkoa wa
Singida una fursa nyingi hasa vitunguu ambavyo vimekuwa vikisafirisha nje ya
nchi na kufungashwa kwa jina la nchi hiyo ya jirani.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dokta Rehema Nchimbi amempongeza Mkurugenzi Mwambe kwa kuendelea
kuaminiwa na Mheshimiwa Raisi kutokana na uchapakazi na uadilifu wake.
Dokta Nchimbi amesema
Mkoa wa Singida umekuwa ukizalisha bidhaa nzuri na zenye ubora pamoja na
kuzalisha watendaji waadilifu na wachapakazi na hivyo uteuzi wake utaendelea
kuwapa hamasa vijana na watumsihi wengine waendelee kuwa waadilifu.
Ameongeza kwa Singida
ina fursa za kutosha kuleta maendeleo ya Mkoa huu pamoja na taifa kwa ujumla
pia unajivunia fursa hizo ambazo baadhi yake ni kilimo cha alizeti, vitunguu na
asali bora.
Dokta Nchimbi amemuasa Mkurugenzi Mwambe kuiwakilisha Singida katika majukumu yake na pia kutumia uchapakazi wake katika kuboresha mazingira ya uwekezaji ili yawavutie wawekezaji wa nje na ndani ili kufikia lengo la tanzania ya Viwanda.
Aidha amemkaribisha tena Singida na kumuahidi kuwa Mkoa uko tayari kwa ajili ya uwekezaji wowote wenye tija kwa wananchi na pia Singida iwe sehemu ya viwanda na kuipa nafasi Dodoma kuwa makao makuu ya nchi.
Mkurugenzi wa TIC Geoffrey Mwambe (wa kwanza kushoto) akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wa kwanza Kulia) katika kikao cha kumuaga, Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo na Mkuu wa Wilaya Mkalama JacksoN Masaka.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi na Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo wakifungua zawadi ya saa ambayo ina picha ya mazao ya alizeti na vitunguu ambavyo huzalishwa kwa wingi na ubora Mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akimpongeza Mkurugenzi Mpya wa TIC kwa uteuzi bw. Geoffrey Mwambe ambaye alikua Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, kulia kwake ni mkurugenzi Mwambe na kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Injinia Jackson Masaka.

No comments:
Post a Comment