Wednesday, June 06, 2018

DC MKALAMA AKUTANA NA WAKULIMA WA ALIZETI PAMOJA NA SHIRIKA LA 'FAIDA MALI' ILI KUHAMASISHA KILIMO CHA KISASA

Akizungumza katika sherehe ya Siku ya Mkulima kwa zao la Alizeti  iliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali FAIDA MALI katika kijiji cha Nduguti kilichopo Kata ya Nduguti wilayani Mkalama mwanzoni mwa mwezi huu, Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhandisi Jackson J. Masaka amesema, mbinu bora za Kilimo ndio mafanikio ya mavuno mengi na yenye Tija ambayo yatawasaidia wakulima kuinua kipato cha Kaya na Usalama wa Chakula kwa ujumla.

Mhe. Masaka alisema, madhumuni ya sherehe hizo ni kuwajengea uwezo wakulima kutambua umuhimu wa elimu ya kilimo bora cha alizeti kwa kutumia pembejeo bora; mbegu bora ya Hysun 33 (Chotara) zinazozaa zaidi na zenye kutoa mafuta mengi zinazosambazwa na Kampuni ya Bytrade kwa  ushirikiano wa shirika la Faida Mali ili kuleta tija kwa Wakulima.

Alisema katika kusambaza teknolojia kwa wakulima na wadau wengine ni vyema maandalizi ya siku ya mkulima yafanyike ambapo elimu kwa vitendo hutolewa ambapo mkulima atapata fursa ya kujionea mwenyewe na hatimaye kufanya uchaguzi mzuri.

Mhandisi Masaka, amelipongeza na kulishukuru Shirika la Faida Mali kwa niaba ya wakulima wa wilaya ya Mkalama kwa mchango wao katika kuwaleta pamoja watoa huduma mbalimbali pamoja ili kuwezesha upatikanaji wa huduma kibiashara zinazohitajika kwa wakulima wadogo katika vikundi vyao zikiwemo; Pembejeo, Masoko ya uhakika, Huduma za kifedha, Huduma za bima za mazao, Taarifa za masoko pamoja na kuwapatia wakulima hao mafunzo mbalimbali ili kusimama wenyewe katika soko lenye ushindani.

Kwa upande wake Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Alizeti kutoka Shirika la Faida Mali mkoa wa Singida  Bi. Maria Daniel Hungii alisema, kwa wilaya ya Mkalama Mradi utapanua wigo zaidi baada ya kuona maeneo mengi ya wilaya yanakubali kilimo cha zao hilo la Alizeti.

"Mradi huo pia unahamasisha wananchi kuwa na sehemu moja ya kuuzia mazao yao yaani collection center kila Kata na utahamasisha ujenzi wa Maghala" Alisema. Bi. Maria 

Aidha, Katika lengo la kuhakikisha wakulima wanatumia mbegu bora Hysun 33 (Chotara) kwa msimu huu mradi umeanzisha mashamba ya mfano 127 kati ya hayo; Mkalama 48, Singida 25, Iramba 24 na Ikungi 30 (demo-plot).

Kwa mkoa wa Singida, shirika linatekeleza mradi katika mnyororo wa thamani wa alizeti chini ya ufadhili wa AMDT ambapo mradi umepanga kuwafikia wakulima 32,000 mpaka ifikapo 2020.

Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhandisi Jackson J. Masaka akizungumza na wakulima katika sherehe ya Siku ya Mkulima kwa zao la Alizeti  iliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali FAIDA MALI katika kijiji cha Nduguti kilichopo Kata ya Nduguti wilaya ya Mkalama mkoani Singida. 

Wakulima wakifuatilia hotuba ya mkuu wa wilaya Mkalama Mhandisi Jackson Masaka (hayupo pichani) wakati akizungumza katika sherehe ya Siku ya Mkulima kwa zao la Alizeti  iliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali FAIDA MALI katika kijiji cha Nduguti kilichopo Kata ya Nduguti wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

Usajili wa wakulima wa mahitaji ya mbegu Chotara ukiendelea. 
Afisa Ugani Kilimo kata ya Nduguti Bw. Arthur M. Nyaki akitambulisha viongozi waliohudhuria Siku ya Mkulima kwa zao la Alizeti  iliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali FAIDA MALI katika kijiji cha Nduguti kilichopo Kata ya Nduguti wilaya ya Mkalama mkoani Singida.
Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Alizeti kutoka Shirika la Faida Mali mkoa wa Singida  Bi. Maria Daniel Hungii akisalimia umma uliohudhuria Siku ya Mkulima kwa zao la Alizeti iliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali FAIDA MALI katika kijiji cha Nduguti kilichopo Kata ya Nduguti wilaya ya Mkalama mkoani Singida. 
Wakulima na wadau mbalimbali wa kilimo cha alizeti wakielekea kwenye shamba ambalo lilipandwa mbegu bora chotara  tarehe 5/2/2018 lenye ukubwa wa ekali 1 na nusu kama shamba la mfano.

Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhandisi Jackson Masaka (mwenye koti jeusi) akiongozana na wakulima na wadau mbalimbali wa kilimo cha alizeti kwenye shamba ambalo lilipandwa mbegu bora chotara  tarehe 5/2/2018 lenye ukubwa wa ekali 1 na nusu kama shamba la mfano.
Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Alizeti kutoka Shirika la Faida Mali mkoa wa Singida  Bi. Maria Daniel Hungii (mwenye kibanio kichwani) akitoa maelekezo shambani wakati wa Siku ya Mkulima kwa zao la Alizeti  iliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali FAIDA MALI katika kijiji cha Nduguti kilichopo Kata ya Nduguti wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

Mkulima mwana kikundi (mwenye ushungi mweusi) akitoa ushuhuda wa mbegu bora Chotara ilivyotoa matunda mazuri shambani.

Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhandisi Jackson Masaka akishuhudia matoke ya mbegu bora Hysun 33 (Chotara). 


Burudani zikiendelea

Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Alizeti kutoka Shirika la Faida Mali mkoa wa Singida  Bi. Maria Daniel Hungii akizungumza kuhusu kazi zinazotekelezwa na Shirika Faida Mali pamoja na mradi wa Alizeti wakati wa Siku ya Mkulima kwa zao la Alizeti wilayani ya Mkalama. 



Wakulima wakifuatilia hotuba ya Mratibu Msaidizi mradi wa alizeti  kutoka Faida Mali Bi. Maria Daniel Hungii (hayupo pichani) wakati akizungumza katika sherehe ya Siku ya Mkulima kwa zao la Alizeti wilayani Mkalama.

Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhandisi Jackson Masaka akifuatilia hotuba ya Mratibu Msaidizi mradi wa alizeti kutoka Faida Mali Bi. Maria Daniel Hungii (hayupo pichani) wakati akizungumza katika sherehe ya Siku ya Mkulima kwa zao la Alizeti wilayani Mkalama.

Burudani zikiendelea


Usajili wa wakulima wa mahitaji ya mbegu Chotara ukiendelea.

Afisa Kilimo wilaya Mkalama Bi. Augenia Baithazar Minja akizungumza wakati wa Siku ya Mkulima kwa zao la Alizeti wilayani Mkalama.
  


Sehemu ya Meza Kuu 


Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhandisi Jackson J. Masaka akizungumza na wakulima katika sherehe ya Siku ya Mkulima kwa zao la Alizeti  wilaya ya Mkalama mkoani Singida.


Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Alizeti kutoka Shirika la Faida Mali mkoa wa Singida  Bi. Maria Daniel Hungii akizungumza na wakulima katika sherehe ya Siku ya Mkulima kwa zao la Alizeti wilaya ya Mkalama mkoani Singida.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nduguti Bw. Julius Samweli Gunda akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wanakijiji na wakulima wa alizeti kwa mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhandisi Jackson Masaka pamoja na Shirika la Faida Mali mkoa wa Singida kwa kufanikisha Siku ya Mkulima wilayani Mkalama.

Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Alizeti kutoka Shirika la Faida Mali mkoa wa Singida  Bi. Maria Daniel Hungii akisalimiana na wakulima mara baada ya kuhitimisha sherehe ya Siku ya Mkulima kwa zao la Alizeti iliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali FAIDA MALI katika kijiji cha Nduguti kilichopo Kata ya Nduguti wilaya ya Mkalama mkoani Singida (kushoto ni mkuu wa wilaya Mkalama). 





"Ninaamini kwamba muda wote wa kilimo tangu maandalizi ya shamba hadi sasa mmeendelea kujifunza katika shamba ambalo tumelitembelea, na mengine kati ya yale yaliyolimwa na wakulima wenzenu katika vikundi au mkulima mmoja mmoja"

"Ni matumaini yangu kuwa mmefurahia uwepo wa Shirika la Faida Mali katika kutoa huduma ya elimu ya kilimo bora na chenye Tija kwa kushirikiana na Kampuni ya pembejeo 'Bytrade' ambapo imeweza kuuza na kugawa kwa ajili ya mashamba darasa, mashamba ya mfano na yale ya maonesho" Mhandisi Jackson Masaka

Imetolewa na:
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa 
SINGIDA

No comments:

Post a Comment