Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Singida Mwl. Ayoub Mchana akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa shindano la Tahajia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Madini Kanda ya Kati uliyopo jirani na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida.
Zaidi ya wanafunzi 400 wa shule za msingi na sekondari kutoka mkoa wa Singida wamependekezwa kujifunza jinsi ya kutekeleza ubora katika tahajia ya maneno kwa njia rahisi na ya ubunifu kufuatia uzinduzi wa shindano la 2018 Spelling BEE uliyofanyika leo (Juni 7, 2018) mkoani Singida. Shindano hili litafanyika tarehe 29 Septemba mwaka huu katika chuo cha uhasibu Singida.
Akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo Meneja wa Shindano Bi. Upendo Mushi kutoka Cece & Daniel Enterprise amesema, Madhumuni ya mashindano
haya ni kuhamasisha ubora wa mafunzo kwa njia ya ushindani wa tahajia
(spelling) katika lugha ya Kiingereza na
Kiswahili, na washiriki ni wanafunzi wa darasa la nne hadi kidato cha nne kutoka
shule za umma zaidi ya 32 kutoka mkoa wa Singida na inatarajiwa kuwa zaidi ya
shule 15 binafsi na za kimataifa watahudhuria shindano hili.
Mkoa wa
Singida kwa ujumla una shule za msingi
551 (za umma 530 na binafsi 22) 164 (za umma 142 na 22 za binafsi) za sekondari
ikiwa ni pamoja na shule 4 za wanfunzi
wenye mahitaji maluum. Kitaifa shule za halmashauri za wilaya ya Itigi na Manyoni
zinafanya vizuri katika mkoa wa Singida katika mitihani ya darasa la 7 na
kidato cha nne. Ufaulu wa halmashauri ya
Itigi kwa mtihani ya darasa la 7 mwaka wa 2017 ilikuwa nafasi ya 56 kati
ya halmshauri 186 nchini, na ufaulu wa halmashauri ya Manyoni katika mitihani ya kidato cha nne ni nafasi 47
kati ya halmashauri 186.
Pamoja na ufaulu
huu mzuri uliojionyesha kwa halmashauri hizi mbili, kiwango cha ufaulu wa shule
zote za sekondari kimepanda ila katika shule za msingi za mkoa ufaulu ulishuka
kwa ujumla na Mkuu wa Mkoa Dkt. Rehema
Nchimbi ameahidi kushirilkiana na wadau wote na jamii katika kuboresha elimu
mkoani Singinda. Hii ni kutokana na ujio
wa mpango wa kuboresha ubora wa elimu
Tanzania – EQUIPT ambao umeanza kutekelezwa rasmi mkoani Singida kuanzia Januari 2018.
Shindano la 2018
Spelling BEE ni la kwanza kushirikisha watoto wenye mahitaji maluum Afrika
Mashariki na ambalo litajumuisha shindano
la tahajia la Kingereza na Kiswahili kwa
wanafunzi viziwi.
Akizungumza
katika uzinduzi wa shindano, Meneja wa shindano hili, Upendo Wanguvu
alisema, "Leo tumeanza safari ya kuchochea ubora wa elimu kwa shindano la
tahajia ambalo tumelenga shule za msingi na sekondari nchini Tanzania. Tunauhakika
ya kwamba mashindano yetu yatahamisha ustadi wa wanafunzi kujifudisha maneno,
maana ya maneno, jinsi ya kutumia maneno katika sentensi na tahaji ya maneno na
hii ni mojawapo ya msingi bora wa elimu.
"Safari yetu mwaka huu imeanza mkoani Singida na tunatarajia ya kwamba shindano hili
litajumuisha mikoa yote 31 ndani ya miaka mitatu ijayo. Aidha, uzinduzi wetu
leo unafungua rasmi wigo wa kujisajili kwa shule binafsi na za kimataif kwa
kutumia tovuti yetu ya www.spellingbee.co.tz
ya shindano letu ” Wanguvu alisema.
Shindano la
Special Needs BEE ni la wanafunzi viziwi ambalo litafanyika kwa lugha ya
Kiswahili na kingereza na wanafunzi watafanya tahajia kwa lugha ya ishara.
Matuamani ya shindano hili ni kuwa zaidi wa wanafunzi 100 kutoka shule za
maitaji maalum mbalimbali Tanzania watahudhuria.
Akizungumza juu
ya Shindano la Special Needs BEE Bw. Yasin Mawe, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika
la Tanzania la Viziwi alisema "Hii ni mara ya kwanza katika historia ya
Tanzania na Afrika Mashariki kuwa na shindano la tahajia ambalo limehusisha wanafunzi
viziwi. Ushirikiano kati ya wanafunzi
wenye mahitaji maalum na wanafunzi wengine ni nguzo kuu ya maendeleo na
tunafurahia ya kuwa mashindano ya 2018 Spelling BEE imejumuisha swala hili na itajenga msingi mzuri wa ushirikiano kati
ya watu wa mahitajii maalum na wengine.
Shindano hili
limeandaliwa na Cece & Daniel Enterprise wakishirikiana na Chuo Kikuu cha
Dodoma (UDOM), Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), Taasisi ya Elimu ya
Tanzania (TIE), Taasisi ya Africa For Inclusive Communities (AFIC), Shirika la
viziwi Tanzania pamoja na ofisi ya rais TAMISEMI na ni mpango wa kipekee wa
ushirikiano kati ya mashirika binafsi na mashirika ya umma (Public Private
Partnership - PPP).
"Lengo kuu
la PPP hii ni kuchochea tabia ya kusoma vitabu miongoni mwa wanafunzi
na tunaamini
kuwa ubora wa kujifunza unapatikana pale mwanafunzi anapokuwa anajua maneno,
maana yake na jinsi ya kutumia maneno haya katika sentensi. Kwa kawaida maneno
yanapatikana katika vitabu na kuhamasisha wanafunzi kujifunza maneno mapya na tahajia
ya maneno itasababisha kujenga tabia ya kusoma kati ya wanafunzi "alisema
Bi. Upendo.
Wito kwa wananchi wa mkoa wa Singida, wanafunzi, makampuni, wadau na wataalamu wa elimu nchini
Tanzania kuunga mkono mpango huu wa kipekee wa 2018 Spelling BEE kwa kushirikiana nao katika shindano hili.
Awali, kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Singida Mwl. Ayoub Mchana amesema kuwa, Faida ya shindano hili kwa wanafunzi ni kujifunza maneno mapya na maana zake, ambayo ni msingi bora wa elimu, Kuongeza ujasiri kwa wanafunzi kwa kusimama mbele za umma na kujieleza, Kuwajengea wanafunzi ujuzi mbalimbali katika matumizi ya lugha ni njia pekee ya kuwapata waandishi fasaha wa lugha.
Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Singida Mwl. Ayoub Mchana akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa shindano la Tahajia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Madini Kanda ya Kati uliyopo jirani na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida.
Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Singida Mwl. Ayoub Mchana akionyesha kitabu chenye Mwongozo wa Shindano la Tahajia waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa shindano la Tahajia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Madini Kanda ya Kati uliyopo jirani na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida.
Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Singida Mwl. Ayoub Mchana akionyesha kitabu chenye Mwongozo wa Shindano la Tahajia (spelling) katika lugha ya Kiingereza waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa shindano la Tahajia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Madini Kanda ya Kati uliyopo jirani na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida.
Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Singida Mwl. Ayoub Mchana akisikiliza maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa shindano la Tahajia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Madini Kanda ya Kati uliyopo jirani na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida.
Meneja wa Shindano (Event Manager-The Spelling BEE) Upendo Mushi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa shindano la Tahajia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Madini Kanda ya Kati uliyopo jirani na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida.
Meneja wa Shindano (Event Manager-The Spelling BEE) Upendo Mushi akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa shindano la Tahajia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Madini Kanda ya Kati uliyopo jirani na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida.
Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Singida Mwl. Ayoub Mchana akinakili jambo wakati wa uzinduzi wa shindano la Tahajia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Madini Kanda ya Kati uliyopo jirani na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida.
Meneja wa Shindano (Event Manager-The Spelling BEE) Upendo Mushi akionyesha kitabu chenye Mwongozo wa Shindano la Tahajia katika lugha ya Kiswahili mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa shindano la Tahajia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Madini Kanda ya Kati uliyopo jirani na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida.
Meneja wa Shindano (Event Manager-The Spelling BEE) Upendo Mushi akionyesha kitabu chenye Mwongozo wa Shindano la Tahajia (spelling) katika lugha ya Kiingereza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa shindano la Tahajia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Madini Kanda ya Kati uliyopo jirani na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida.
Waandishi wa habari wakiuliza maswali
Meneja wa Shindano (Event Manager-The Spelling BEE) Upendo Mushi akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani).
Waandishi wa habari wakiuliza maswali
Imetolewa na:
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
SINGIDA.
No comments:
Post a Comment