WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba (mwenye kipaza sauti-mic) akizindua ununuzi wa Pamba mkoani Singida mwishoni mwa wiki hii (Juni 8, 2018).
Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba amewaagiza wanachama wa vyama wa Ushirika nchini kurudia chaguzi na kuwaondoa madarakani haraka viongozi wa vyama hivyo iwapo tu watagundua viongozi waliopo madarakani sio waadilifu.
Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba amewaagiza wanachama wa vyama wa Ushirika nchini kurudia chaguzi na kuwaondoa madarakani haraka viongozi wa vyama hivyo iwapo tu watagundua viongozi waliopo madarakani sio waadilifu.
Waziri Tizeba ametoa
kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi kwenye mikutano
ya hadhara katika Vijiji vya Kikio na Misughaa wilayani Ikungi katika ziara
yake ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya
kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa
ujumla.
Kauli ya Waziri wa
Kilimo Dkt. Charles Tizeba huenda ikaleta faraja na matumaini mapya kwa
wananchama wa vyama vya ushirika hasa baada ya kuchoshwa na ubadhirifu na
mizigo ya madeni iliyosababishwa na baadhi na viongozi wasio waaminifu.
Akizungumza na
wananchi wa vijiji vya Kikio na Misughaa wilayani Ikungi mkoa wa Singida katika
mikutano ya hadhara, Waziri Tizeba
ametoa onyo kwa
viongozi watakaobainika kufanya vitendo vya ubadhirifu.
Pia amewaagiza viongozi
wa Bodi ya Pamba nchini na viongozi wa vyama vya Ushirika kuacha mara
moja kuwalazimisha wananchi kufungua akaunti ili fedha walizouza Pamba
zipitie benki.
“Kuna dhana ya Ushirika na ushiriki wao wa kuuza na kununua"
"Sitarajii kila
mwananchi wa kijijini awe na akaunti, hivyo niwaombe bodi msilazimishe watu
kwenda kufungua akaunti, fanyeni ushawishi, waelimisheni watu faida ya kufungua
akaunti”. Alisema Dkt. Tizeba
Aidha amewaagiza
wakulima wote nchini kuchoma moto masalia ya mazao yaliyovunwa pamba, mahindi
na mazao mengine ili kuua wadudu wanaojulikana kwa jina la Viwavijeshi. Wadudu
hao ni wapya aina ya Fall Armyworm (FAW) wanajulikana kitaalamu kama spodopter frugiperda
ambao wametajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuharibu mazao mbalimbali hususani mahindi
ambalo ndio zao kuu la chakula nchini. (sifa yake mdudu huyo (viwavijeshi) anakula mimea aina 80).
“Kila alipoonekana mdudu Kiwavijeshi mhakikishe baada ya mavuno shambani, kuchoma masalia yote ya mazao, hivyo usiingie kwenye kilimo msimu ujao bila
kuchoma moto masalia ya mazao yaliyovunwa shambani”. Alisisitiza Dkt. Tizeba
Kwa upande wake Mkuu
wa wilaya ya Ikungi, Mhe. Miraji Mtaturu amesema wakulima wa wilaya hiyo kwa
sasa wanafanya vizuri katika kilimo cha Pamba hivyo ameomba Serikali
kuongeza maafisa Ugani ambao watasaidia kuelimisha wananchi kutumia njia bora
na za kisasa katika kilimo cha pamba.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Mkurugenzi wa kampuni ya BioSustain ya Singida Dkt. Riyaz Haider amemshukuru Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba kwa ziara yake mkoani Singida ambapo kampuni hiyo imepewa kazi ya ununuzi wa zao hilo la pamba Singida
"Nashukuru kwa ujio wa mheshimiwa Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba kwenye eneo letu mkoani Singida pamoja na viongozi wa Bodi ya Pamba nchini kwa kushirikiana kwenye mfumo mpya ambao unazingatiwa sheria na sheria za bodi ya pamba kwenye kupata ubora wa pamba, sheria za upandaji na uvunaji (uchambuaji) ili kuweza kuwaamsha wakulia ili kuepukana na changamoto zilizojitokea katika misimu iliyopita" Alisema Dkt. Riyaz Haider
Wananchi wa vijiji vya
Kikio na Misughaa wilayani Ikungi wanasema tangu Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Joseph Magufuli iingie madarakani wameanza kupata mafanikio makubwa sana katika kilimo kutokana na
jitihada za viongozi mbalimbali wa Serikali kwa kuhakikisha wakulima wananufaika.
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba kushoto akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji J. Mtaturu mara baada ya kuwasili wilayani Ikungi katika ziara yake ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba kushoto akisalimiana na Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi Winfrida Funto mara baada ya kuwasili wilayani Ikungi katika ziara yake ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba kushoto akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Ndg. Ally J. Mwanga mara baada ya kuwasili wilayani Ikungi katika ziara yake ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba kushoto akisalimiana na Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ikungi mara baada ya kuwasili wilayani Ikungi katika ziara yake ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba kushoto akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya BioSustain Dkt. Riyaz Haider mara baada ya kuwasili wilayani Ikungi katika ziara yake ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba kushoto akisalimiana na ICS BioSustain Manager ( Internal Control System) wa Kampuni ya BioSustain Bw. Deogratius Paul mara baada ya kuwasili wilayani Ikungi katika ziara yake ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba kushoto akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Mhe. Bi. Rustika Turuka mara baada ya kuwasili wilayani Ikungi katika ziara yake ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba kushoto akisalimiana na Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Ndg. Stastelaus Choaji mara baada ya kuwasili wilayani Ikungi katika ziara yake ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba kushoto akisalimiana na Mrajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoa wa Singida Ngd. Thomas Nyamba mara baada ya kuwasili wilayani Ikungi katika ziara yake ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ikungi Ndg. Mika Likapakapa akisalimia wakati wa mkutano wa ziara ya Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt. Charles Tizeba ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Ndg. Ally J. Mwanga akisalimia wakati wa mkutano wa ziara ya Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt. Charles Tizeba ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Ndg. Stastelaus Choaji akizungumza wakati wa uzinduzi wa ununuzi wa Pamba uliozinduliwa na Mhe. Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba katika Kata ya Kikio, wilaya ya Ikungi mkoani Singida
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji J. Mtaturu akizungumza wakati wa uzinduzi wa ununuzi wa Pamba uliozinduliwa na Mhe. Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba katika kijiji cha Kikio, wilaya ya Ikungi mkoani Singida
Mkutano ukiendelea wakati wa uzinduzi wa ununuzi wa Pamba uliozinduliwa na Mhe. Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba katika Kata ya Kikio, wilaya ya Ikungi mkoani Singida
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba kushoto akizungumza
wilayani Ikungi kata ya Kikio katika ziara yake ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
Sehemu ya viongozi na wadau wa pamba mkoa wa Singida wakimsikiliza Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba wakati akizungumza wilayani Ikungi kata ya Kikio katika ziara yake ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
Mkurugenzi wa Kampuni ya BioSustain Dkt. Riyaz Haider akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa ununuzi wa Pamba uliozinduliwa na Mhe. Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba katika Kata ya Kikio, wilaya ya Ikungi mkoani Singida
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akisisitiza jambo kwa wakulima wa zao la pamba wilayani Ikungi kata ya Kikio katika ziara yake ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
Baadhi ya viongozi wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo kwa makini wakati akizungumza wilayani Ikungi kata ya Kikio katika ziara yake ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akifurahia jambo katika mazungumzo yake kwa wakulima wa zao la pamba wilayani Ikungi kata ya Kikio katika ziara yake ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba, Marco Mtunga akizungumza wakati wa uzinduzi wa ununuzi wa Pamba uliozinduliwa na Mhe. Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba katika Kata ya Kikio, wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akijibu maswali ya wakulima wa pamba wilayani Ikungi kata ya Kikio katika ziara yake ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akisisitiza umakini wa upimaji katika mizani ili mkulima wa pamba asipoteze hata shilingi moja wakati wa vipimo. "Msimu huu tunakaga hadi penati" alisisitiza.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji J. Mtaturu akizungumza wakati wa uzinduzi wa ununuzi wa Pamba uliozinduliwa na Mhe. Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba katika Kata ya Kikio, wilaya ya Ikungi mkoani Singida
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akisoma mizani wakati wa upimaji katika mizani ili mkulima wa pamba asipoteze hata shilingi moja wakati wa vipimo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya BioSustain Dkt. Riyaz Haider pamoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo wakisalimia mara baada ya kutambulishwa kwa wakulima wa pamba katika ziara ya Waziri wa Kilimo ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
Mkutano ukiendelea katika kijiji cha Misughaa wilayani Ikungi mkoa wa Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji J. Mtaturu akimkabidhi zawadi ya fedha kwa niaba ya wanakijiji wa Misughaa kwa niaba ya Mhe. Waziri wa Kilimo zawadi kwa mapokezi mazuri ya ugeni huo wakati wa uzinduzi wa ununuzi wa Pamba uliozinduliwa na Mhe. Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba katika Kata ya Misughaa, wilaya ya Ikungi.
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba (mwenye Kaunda Suti) akisindikizwa kwa shangwe na ndelemo za wanakijiji wa Misughaa wilayani Ikungi mkoa wa Singida mara baada ya kuhitimisha mkutano wa hadhara.
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akisindikizwa kwa shangwe na nderemo za wanakijiji wa Misughaa kata ya Misughaa wilayani Ikungi mara baada ya kumaliza mkutano na wakulima wa pamba kijijini hapo katika ziara yake ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza katika kikao cha kuwasilisha hali ya Kilimo cha Pamba kwa ujumla mkoani Singida kwa Mhe. Waziri wa Kilimo katika ziara ya Waziri wa Kilimo ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt. Charlse Tizeba akizungumza katika kikao cha kuwasilisha hali ya Kilimo cha Pamba kwa ujumla mkoani Singida katika ziara ya Waziri wa Kilimo ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
ZIARA WILAYANI IRAMBA JUNI 9, 2018.
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akionyesha wakulima wa pamba wilayani Iramba jinsi ya kuondoa uchafu uliyo kwenye pamba ili kuhakikisha pamba inayopatikana ni safi (grade one) katika ziara yake ya kukagua na kuzindua ununuzi wa Pamba pamoja na kujionea jinsi namna ya kilimo hususani zao la Pamba linavyosimamiwa wilayani na mkoa wa Singida kwa ujumla.
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akisisitiza umakini wa upimaji katika mizani ili mkulima wa pamba asipoteze hata shilingi moja katika vipimo jana alipotembelea wilaya ya Iramba, mkoani Singida. Kulia Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Luhahula akishuhudia uzinduzi wa ununuzi wa pamba katika wilaya ya Iramba.
Imetolewa na:
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
SINGIDA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
SINGIDA
No comments:
Post a Comment