Tuesday, June 05, 2018

RC SINGIDA DKT. REHEMA NCHIMBI AONGOZA KIKAO CHA MKAKATI MAHUSUSI WA UNUNUZI WA PAMBA 2018/2019


Mkuu wa mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wakatikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Pamba mara baada ya kumaliza kikao ambacho kimejipanga kuwa na mkakati mahususi wa ununuzi wa Pamba 2018/2019 mkoani Singida.

Mkuu wa mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi aongoza kikao ambacho kimejipanga kuwa na mkakati mahususi wa ununuzi wa Pamba msimu huu wa mwaka 2018/2019 mkoani Singida. 

Akizungumza na Katibu Tawala wa mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi na wadau wengine wa  Pamba wakiwemo; Wakala wa Vipimo, Mjumbe wa vyama vya Ushirika mkoa wa Singida (SIFACU) pamoja na Mrajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoa wa Singida Bw. Tomas Nyamba waliofika ofisini kwake Dkt. Nchimbi alisema, mkoa wa Singida msimu huu wa mwaka 2018/2019 kwa kuzingatia maelekezo ya Serikali na hasa maelekezo na usimamizi wa Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassimu Majaliwa, umetekeleza na unauhakika wa kuwa na mavuno makubwa sana ya Pamba.


Dkt. Nchimbi alisema, Serikali ya mkoa wa Singida imejipanga kwa kuwa na timu ya pamoja ambayo imekuwa nayo mwaka huu 2018 kwa kila mmoja kuwa Afisa Ugani.


"Mkuu wa mkoa Afisa Ugani, Mkuu wa wilaya Afisa Ugani, Katibu Tawala mkoa (RAS) Afisa Ugani, viongozi wa Dini nao ni maafisa Ugani, Wakulima wenyewe maafisa Ugani, wanachama wa vyama vya Ushirika maafisa Ugani ili kuondoa swala la kulaumiana kwamba mkoa haukufanya vizuri kutokana na mmoja wetu amekosea sehemu" alisema Dkt. Nchimbi.

Awali Dkt. Nchimbi alianza kikao kwa kuwashukuru Wakulima wa mkoa wa Singida ambao waliyapokea maelekezo kwa kulima pamba kiutalaamu kwa kufuata mstari na kuendelea kutunza mashamba yao vizuri. 

Kwa upande wao Wakala wa Vipimo wamesema, umejipanga vizuri kuhakikisha kwamba mizani zote zitakazotumika kwenye ununuzi wa mazao hasa pamba vimehakikiwa ipasavyo ili kuhakikisha vipimo haviwi sababu ya kuharibu ubora wa pamba, ambapo awali wakulima wa pamba walikuwa wanaweka maji kwenye pamba au mawe ili kufidia mapunjo wanayoyapata kwenye mizani.


Mkuu wa mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiongoza kikao ambacho kimejipanga kuwa na mkakati mahususi wa ununuzi wa Pamba msimu huu wa mwaka 2018/2019 mkoani Singida. 

Mjumbe wa Wakala wa Vipimo akizungumza wakati wa kikao ambacho kimejipanga kuwa na mkakati mahususi wa ununuzi wa Pamba msimu huu wa mwaka 2018/2019 mkoani Singida. 

Mkuu wa mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba) akiongoza kikao ambacho kimejipanga kuwa na mkakati mahususi wa ununuzi wa Pamba msimu huu wa mwaka 2018/2019 mkoani Singida. 

Katibu Tawala mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi kulia akizungumza wakati wa kikao ambacho kimejipanga kuwa na mkakati mahususi wa ununuzi wa Pamba msimu huu wa mwaka 2018/2019 mkoani Singida. 





Wadau wa ununuzi wa pamba wakifuatilia jambo wakati wa kikao ambacho kimejipanga kuwa na mkakati mahususi wa ununuzi wa Pamba msimu huu wa mwaka 2018/2019 mkoani Singida. 

 Kikao cha wadau wa ununuzi wa pamba mkoa wa Singida kikiendelea



 Mjumbe akizungumza wakati wa kikao ambacho kimejipanga kuwa na mkakati mahususi wa ununuzi wa Pamba msimu huu wa mwaka 2018/2019 mkoani Singida. 



Imetolewa na:
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano:
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida

No comments:

Post a Comment