Monday, June 04, 2018

KATIKA KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA, USHIRIKA NDIYO NJIA PEKEE YA KUPATA MALIGHAFI ZA KULISHA VIWANDA VYETU-DKT. NCHIMBI


Mhe. Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akitoa mafunzo ya matumizi sahihi ya viuatilifu kwa wakulima wa Pamba wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa mshamba ya pamba mkoani Singida.

Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Singida (Singida Farmers Co-Operative Union-SIFACU LTD) kimefanya Mkutano wake Mkuu wa Pili  wa Mwaka  31/05/2018 pamoja na kupitisha makisio ya mapato na matumizi sambamba na kufanya uchaguzi wa viongozi wa Ushirika wa Mkoa wa Singida katika ukumbi wa mikutano wa Askofu Rwoma katika Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Akisoma hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Singida Mhe. Elias Tarimo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Singida alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli imewaamini  kusimamia Chombo chao cha kiuchumi wao wenyewe (Ushirika).
“Kwa kuwa Serikali imewaamini basi na ninyi mjiamini kwamba mnaweza kuwasimamia wakulima wenzenu bila kuwasaliti" alisema Dkt. Nchimbi
Katika hotuba yake Dkt. Nchimbi amesema kuwa, katika kufikia uchumi wa Viwanda, Ushirika ndiyo njia pekee ya kupata malighafi za kulisha viwanda vyetu hapa nchini na nje ya nchi. 
Aidha, amewasihi wana Singida kuwekeza katika kilimo cha mazao ya biashara na chakula hususani Pamba, Korosho, Tumbaku, Alizeti, Ufuta, Mahindi na mazao mengine yalimwayo mkoani Singida kulingana na hali ya hewa.
 "Singida imejaliwa kwa neema ya mazao mbalimbali ambayo yanaweza kututoa wana Singida kiuchumi" Dkt. Nchimbi 
Hata hivyo, Dkt. Nchimbi aliwahakikishia washiriki kuwa, Serikali itashirikiana nao katika kuondoa dhuluma dhidi yao (wana Ushirika) inayofanywa na wajanja wachache kwa kununua mazao ya wakulima kwa bei za chini na kutumia vipimo visivyo rasmi

Dkt. Nchimbi amewaagiza watendaji wote kusoma nyaraka mbalimbali ikiwa ni pamoja na zile zinazohusu Bodi ya pamba na Sheria ya Ushirika Na. 6 ya Mwaka 2013 na kanuni zake, bila kusahau Ilani ya Chama Tawala ambayo inasisitiza uwezeshaji wa wananchi kiuchumi kupitia Ushirika kama ndiyo njia pekee ya kuwalinda wanyonge.
KWA UPANDE WAKE, Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Singida Bw. Tomas Nyamba amesema kuwa mkoa wa Singida unavyama 107 vya kilimo na masoko maalufu kwa jina la Amcos, ambapo kati ya vyama hivyo, 65 ndivyo vilivyofanya uchaguzi wake wa viongozi na vyama 17 vinategemewa kukamilisha uchaguzi wake mara baada ya kuwafikia na hii ni kutokana na Rasilimali watu (maafisa) kuwa wachache, na vyama 17 bado havijafanya uchaguzi akisema kuwa vimesinzia ambapo ndio wanaviamsha ili kuvifanya kuwa  vyama hai hatimaye kuwa na vyama kamili 107 kama inavyosomeka kwenye daftari la msajili wa vyama vya Ushirika Taifa.
Aidha, amesema kuwa vyama vyote vya Ushirika vinavyolima zao la pamba mkoani Singida wamevifikia pamoja na vikundi vyote na vile vikundi ambavyo vilikuwa havijasajiliwa vimepewa usajili wa muda kama vyama vya Ushirika vya awali ili vitakavyoweza kufikia sifa vya kuwa vyama vya Ushirika ndivyo vitapatiwa Hati kamili ya kutambuliwa kama vyama vya Ushirika vya kilimo na Masoko mwishoni mwa msimu huu 2018 ili kuendelea navyo mwakani 2019.
"Endapo vyama vitakavyoweza kutimiza au kukidhi mahitaji yaliyotolewa ikiwa ni pamoja na kufanya ukusanyaji wa pamba kwa wanachama wake na ushuru watakaoupata waweze kujiendesha bila hasara vitapatiwa Hati kamili vya kutambulikuwa kuwa vyama vya Ushirika mwishoni mwa mwaka huu 2018" Bw. Tomas Nyamba alisema.

Naye Mkaguzi wa Bodi ya pamba mkoa wa Singida Bw. Abdulrahman Sempule amesema kuwa, kuanzia msimu ujao wakulima wote wa zao la Pamba watapatiwa pembejeo zote bure  ili kuongeza uzalishaji. 

Aidha, amewashauri wakulima wa pamba kutochanganya mazao ya pamba na mahindi na kusisitizia kwamba mipaka ya mashamba ya pamba yanashauriwa kuwa mbali urefu wa mita 5 kutoka shamba moja na lingine ili kusaidia kama kuna mdudu kwenye mahindi hatoweza kushambulia mimea ya zao la pamba.

 Katibu Meneja wa chama kikuu cha Ushirika Mkoa wa Singida (SIFACU) Bw. Paul Mbogo akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Pili wa Chama cha Ushirika uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Askofu Rwoma katika Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.


Sehemu ya Meza Kuu wakati wa mkutano mkuu wa Pili wa Chama cha Ushirika (SIFACU) uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Askofu Rwoma katika Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Mjumbe akiuliza swali wakati wa mkutano mkuu wa Pili wa Chama cha Ushirika (SIFACU) uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Askofu Rwoma katika Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Mjumbe akieleza jambo wakati wa mkutano mkuu wa Pili wa Chama cha Ushirika (SIFACU) uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Askofu Rwoma katika Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Afisa Mahusiano kutoka Benki ya CRDB Mkoa wa Singida na Dodoma Bw. Evance Makundi akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa Pili wa Chama cha Ushirika (SIFACU) uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Askofu Rwoma katika Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Mkaguzi wa Bodi ya Pamba mkoani Singida Bw. Abrahaman Athuman akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa Pili wa Chama cha Ushirika (SIFACU) uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Askofu Rwoma katika Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Kikao kikiendelea 

 Mrajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoa wa Singida Bw. Tomas Nyamba akitoa maelezo mafupi kabla ya mgeni rasmi kuwasili ukumbini wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Pili wa Chama cha Ushirika.

Mheshimiwa Mwenyekiti wa SIFACU aliyemaliza muda wake Bw. Idd Mnyapanda akitoa maelezo mafupi kabla ya kuwasili ukumbini mgeni rasmi wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Pili wa Chama cha Ushirika.

Afisa Vipimo mkoa wa Singida akionyesha umuhimu wa mizani wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Pili wa Chama cha Ushirika.



Afisa Vipimo mkoa wa Singida Bw. Magezi Jivunda akitoa elimu kwa  wakulima wa pamba kuhusu umuhimu wa mizani na mzani gani ni mzuri kwa kupimia pamba. Aidha aliwasihi wakulima kuwa makini wakati wa kupima pamba ili kila mkulima apate faida na kuepuka kuibiwa wakati wa kupima pamba.
  
 Mjumbe akiuliza swali wakati wa mkutano mkuu wa Pili wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Singida (SIFACU).

Mjumbe akiuliza swali wakati wa mkutano mkuu wa Pili wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Singida (SIFACU).

Mjumbe akiuliza swali wakati wa mkutano mkuu wa Pili wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Singida (SIFACU).

Mkutano mkuu wa Pili wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Singida (SIFACU) ukiendelea.


Sehemu ya wadau na wataalamu mbalimbali wa pamba wakiwemo mjumbe kutoka bodi ya pamba, wajumbe akiuliza swali wakati wa mkutano mkuu wa Pili wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Singida (SIFACU).

Mwakilishi wa Kampuni ya Biosustain  akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa Pili wa Chama cha Ushirika (SIFACU) uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Askofu Rwoma katika Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Meneja Uendeshaji (O.M) wa Kampuni ya Biosustain  Bw. Zakaria Marko akitoa elimu kuhusu pamba wakati wa mkutano mkuu wa Pili wa Chama cha Ushirika (SIFACU) uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Askofu Rwoma katika Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.



Mkuu wa wilaya ya Singida (mgeni rasmi) Mhe. Elias Tarimo (wa kwanza kushoto) akiwasili kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Singida.

Mkuu wa wilaya ya Singida Mhe. Elias Tarimo (wa pili kushoto) akipokelewa mara baada ya kuwasili ukumbini, kushoto kwake mstari wa mbele ni mwenyekiti mstaafu Mhe. Idd Mnyampanda na kulia kwake ni Mrajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoa wa Singida Bw. Tomas Nyamba.

Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Mhe. Idd Mnyampanda akisoma yatokanayo na mkutano uliyopita wa tarehe 26/10/2016 mara baada ya kufungua mkutano. 


Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Bw. Slauslaus Choaji (wa kwanza kushoto) akiteta jambo na Mrajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoa wa Singida Bw. Tomas Nyamba wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 2 wa Chama cha Ushirika, mkoani Singida.
Mjumbe kutoka Amcos Kata ya Chikala wilayani Manyoni Bw. Gofrey Saguda Magawa ambaye pia katika sherehe za Nanenane za mwaka 2008 alikuwa mshindi wa pili ngazi Taifa  kwa kulima pamba akitokea mkoani Singida,  akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 2 wa Chama cha Ushirika uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kanisa kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Mrajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoa wa Singida akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Pili wa Chama cha Ushirika (SIFACU) uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kanisa kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Wajumbe wakipiga makofi wakati mgeni rasmi alipowasili ndani ya ukumbi wakati wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Singida (SIFACU).

Mkuu wa wilaya ya Singida Mhe. Elias Tarimo akizungumza mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 2 wa Chama cha Ushirika uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kanisa kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Wajumbe wakifuatilia jambo makini kutano Mkuu wa Mwaka wa 2 wa Chama cha Ushirika uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Askofu Rwoma katika Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.


Mwenyekiti wa muda Bw. Gofrey Saguda Magawa ambaye pia katika sherehe za Nanenane za mwaka 2008 alikuwa mshindi wa pili ngazi Taifa  kwa kulima pamba akitokea mkoani Singida,  akiongoza uchaguzi wa bodi ya uongozi wa SIFACU wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 2 wa Chama cha Ushirika uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kanisa kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Bw. Slauslaus Choaji akisisitiza  jambo kwa wakulima wa pamba mkoa wa Singida wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 2 wa Chama cha Ushirika, mkoani Singida.


Afisa Kilimo mkoa wa Singida Bw. Mashaka Mlangi akizungumza jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 2 wa Chama cha Ushirika, mkoani Singida.

Katibu Meneja wa chama kikuu cha Ushirika Mkoa wa Singida (SIFACU) Bw. Paul Mbogo akisisitiza jambo mara baada ya kusoma makisio ya mapato na matumizi wakati wa Mkutano mkuu wa Mwaka wa Pili wa Chama cha Ushirika uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Askofu Rwoma katika Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Kura zikiesabiwa wakati wa uchaguzi wa bodi ya viongozi wa chama kikuu cha Ushirika Mkoa wa Singida (SIFACU) katika Mkutano mkuu wa Mwaka wa 2 wa Chama cha Ushirika uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Askofu Rwoma katika Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Uchaguzi wa bodi ya viongozi wa chama kikuu cha Ushirika Mkoa wa Singida (SIFACU) ukiendelea katika Ukumbi wa mikutano wa Askofu Rwoma katika Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Mhe. Mwenyekiti mpya aliyechaguliwa wa bodi ya chama kikuu cha Ushirika Mkoa wa Singida (SIFACU) Bw.  Hamis Rajab akitoa neno la shukrani na kuomba ushirikiano wakati wa Mkutano mkuu wa Mwaka wa 2 wa Chama cha Ushirika uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Askofu Rwoma katika Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.


Mrajisi Msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoa wa Singida Bw. Tomas Nyamba akifunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 2 wa Chama cha Ushirika (SIFACU).

Katika msimu ujao wa kilimo 2018/19, wakulima wote watapanda mbegu aina ya UKM08 AMBAYO Imeidhinishwa, mbegu hii kwa mujibu wa utafiti itamwongezea mkulima tija kwa zaidi ya asilimia 25 kwa sababu inaukinzani na magonjwa ya pamba ambayo ni Mnyauko Fuzari na Bakabakteria, pia ina uwiano mkubwa wa nyuzi ikilinganishw na aina nyingine za mbegu hususan UK91.

Msimu wa ununuzi wa pamba umefunguliwa rasmi tarehe 1 Mei, 2018. 
Pamba inazalishwa zaidi katika mikoa 17 nchini Tanzania ambayo ni Singida, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Geita, Mara, Kagera, Tabora, Kigoma, Katavi, Dodoma, Morogoro, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Manyara na Iringa.

Imetolewa na:
 Kitengo cha Technolojia ya Habari na Mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida

No comments:

Post a Comment