Mkurugenzi
wa Halmashauri ya wilaya ya Itigi, Mhe. Pius Luhende (mwenye tai) akiongoza
timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mkoa wa Singida pamoja na timu ya wilaya
wakati wa kutembelea mradi wa Skimu ya umwagiliaji uliyopo ITAGATA, katika
Halmashauri ya wilaya ya Itigi, wilaya ya Manyoni, mkoani Singida.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya wilaya ya Itigi, Mhe. Pius Luhende (wapili kutoka kulia)
akielezea maendeleo ya mradi mbele ya timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya
mkoa wa Singida pamoja na timu ya wilaya wakati wa kutembelea mradi
wa Skimu ya umwagiliaji uliyopo ITAGATA, katika Halmashauri ya wilaya ya Itigi,
wilaya ya Manyoni, mkoani Singida.
Sehemu ya Bwawa la Skimu ya Umwagiliaji, Itagata
Timu ya
Maji na Usafi wa Mazingira ya mkoa wa Singida pamoja na timu ya Halmashauri ya
wilaya ya Itigi wakishuka kutoka kwenye chanzo cha maji (bwawa) kuelekea kwenye
mashine inayotumika kusambaza maji kupitia kwenye mifereji ya usambazaji maji
yenye ukubwa wa kutosha kupeleka kwenye Mashamba.
Timu ya
Maji na Usafi wa Mazingira ya mkoa wa Singida pamoja na timu ya wilaya wakitoka
kukagua Mradi wa
Skimu ya umwagiliaji uliyopo ITAGATA, katika Halmashauri ya wilaya ya Itigi,
wilaya ya Manyoni, mkoani Singida.
AIDHA kupitia
ziara hiyo, Timu ya Mkoa iliweza kukutana kikao cha pamoja na wafanyakazi wa
Halmashauri ya wilaya ya Itigi wanaounda Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya
Halmashauri ili kuzungumzia maendeleo ya miradi mbalimbali ya Maji na Usafi wa
Mazingira pamoja na changamoto za miradi iliyopo katika Halmashauri hiyo.
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uratibu na Mipango Bw.
Barthelome Temba ambaye ndiye Makamo Mwenyekiti wa Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira
ya mkoa wa Singida akifungua kikao cha pamoja na timu ya Maji na Usafi wa
Mazingira ya Halmashauri ya wilaya ya Itigi mara baada ya kutembelea Mradi wa
Skimu ya umwagiliaji uliyopo ITAGATA, katika Halmashauri ya wilaya ya Itigi,
wilaya ya Manyoni, mkoani Singida.
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Maji Mhandisi. Lydia Joseph
ambaye ndiye Katibu wa Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mkoa wa Singida
akizungumza jambo wakati wa kikao cha pamoja na timu ya Maji na Usafi wa
Mazingira ya Halmashauri ya wilaya ya Itigi mara baada ya kutembelea Mradi wa
Skimu ya umwagiliaji uliyopo kijijini ITAGATA, katika Halmashauri ya wilaya ya
Itigi, wilaya ya Manyoni, mkoani Singida.
Mjumbe akizungumza jambo wakati wa kikao cha pamoja
Kikao kikiendelea
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Itigi, Mhe. Pius
Luhende (wakwanza kushoto) ambaye ndiye Mwenyekiti wa Timu ya Maji na Usafi wa
Mazingira ya Halmashauri ya wilaya ya Itigi akizungumza jambo wakati wa
kikao cha pamoja na Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Mkoa wa Singida mara
baada ya kutembelea Mradi wa Skimu ya umwagiliaji uliyopo kijijini ITAGATA, katika
Halmashauri ya wilaya ya Itigi, wilaya ya Manyoni, mkoani Singida.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa mkoa wa Singida Bw. Patrick
Kasango mjumbe wa Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mkoa wa Singida
akizungumza jambo wakati wa kikao cha pamoja na timu ya Maji na Usafi wa
Mazingira ya Halmashauri ya wilaya ya Itigi mara baada ya kutembelea Mradi wa
Skimu ya umwagiliaji uliyopo kijijini ITAGATA, katika Halmashauri ya wilaya ya
Itigi, wilaya ya Manyoni, mkoani Singida.
Wajumbe wa Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya wilaya ya Itigi wakifurahia jambo wakati wa kikao cha pamoja na timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Mkoa wa Singida.
Mjumbe wa Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya wilaya ya Itigi akizungumza jambo wakati wa kikao cha pamoja na timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Mkoa wa Singida.
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uratibu na Mipango Bw. Barthelome Temba ambaye ndiye Makamo Mwenyekiti wa Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mkoa wa Singida akifunga kikao cha pamoja na timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya wilaya ya Itigi wilaya ya Manyoni, mkoani Singida.
Wajumbe wa Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mkoa wa
Singida wakiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya
Halmashauri ya wilaya ya Itigi wilaya ya Manyoni, mkoani Singida.
Mradi
wa Ujenzi wa Bwala la Skimu ya Umwagiliaji katika Kijiji Cha Itagata
Halmashauri ya wilaya ya Itigi wiliya ya Manyoni mkoani Singida una uwezo wa kuhudumia
Hekta zipatazo 160 katika eneo tambarare kwa ajili ya Kilimo cha Umwagiliaji
hususani zao la Mpunga, mazao ya bustani na vitalu vya kuoteshea miche ya
Tumbaku kwani eneo hilo lina udongo rafiki kwa Kilimo hicho.
Imetolewa na Kitengo cha Technolojia ya Habari na Mawasiliano;
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida.
No comments:
Post a Comment