Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akionyesha ada ya uanachama wake katika
timu ya mpira wa miguu ya Stand Misuna mapema leo asubuhi alipowatembelea
wanachama wa timu hiyo, pembeni yake ni Mwenyekiti wa timu hiyo Yahya Said
Kisiu.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na wanachama wa timu ya Stand
Misuna mapema leo asubuhi alipowatembelea na kuwahamasiha kuendeleza timu hiyo
ili ipande daraja la kwanza katika msimu ujao.
Wanachama
wa timu ya mpira wa miguu ya Stand Misuna wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa
wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi mapema leo alipowatembelea.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameiagiza halmashauri ya Manispaa ya Singida
kusimamia upatikanaji wa mizinga hamsini ya nyuki kwa ajili ya timu ya mpira wa
Miguu ya Misuna Stand kwakuwa imekua ni timu yenye lengo la kuwa kituo cha
mafunzo na marekebisho ya tabia.
Dokta Nchimbi ametoa
agizo hilo mapema leo asubuhi alipokutana na wananchama wa klabu hiyo ambapo
amewaomba radhi kwakuwa Mkoa, wilaya na Halmashauri ya manispaa imekuwa haitoi
ushirikiano wa kutosha kwa timu hiyo.
Amesema timu hiyo
ambayo imeundwa na umoja wa Mawakala wa Mabasi Singida, imekuwa mstari wa mbele
wa kubadilisha tabia mbaya kuwa njema hasa kutokana na mazingira ya stendi
nyingi nchini kutawaliwa na vitendo vya uvunjaji wa sheria.
Dkt. Nchimbi
ameongeza kuwa sasa serikali ya Mkoa, wilaya na halmashauri imewatambua na kwa
kuthibisha hilo yeye kama mkuu wa mkoa amejiunga ramsi kama mwananchama wa timu
hiyo ya mpira wa miguu na kutoa michango ya miezi mitatu ambapo kila siku mwanachama
anatakiwa kuchangia shilingi miatano.
“Nimetoa ada ya
uanachama kuonyesha kuwa tupo pamoja na tutashirikiana kuhakikisha timu yetu ya
Misuna Stand inapanda daraja, kwa sasa nawaomba wanachama wote tushirikiane katika
kuiboresha timu yetu”, amesisitiza.
Dkt. Nchimbi amesema
lengo la Mkoa ni kuwa na timu mbili za mpira wa miguu ambazo zinashiriki ligi
kuu na kwakuwa tayari uwanja wa nyumbani wa Namfua Stadium uko katika hatua za
mwisho za ukamilishaji huku akiwahakikishia mashabiki wa Singida United kuwa
wataishuhudia timu yao ikicheza nyumbani.
Kwa Upande wake Mkuu
wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo ambaye ameteuliwa kuwa Mlezi wa Timu hiyo
amesema stendi zimekuwa ni mahala pa wizi, uvutaji wa madawa ya kulevya na
vitendo viovu lakini jitihada za Misuna Stand FC zitabadilisha tabia hizo na
kuwa njema.
Tarimo amesema
wanachama watakuwa wachapakazi kwakuwa kila siku wanatakiwa kulipa kiasi cha
shilingi miatano lakini pia wamejipanga kuhakikisha wanaelimishana juu ya
madawa ya kulevya jambo ambalo litaufanya Mkoa na Mji wa Singida kuwa wa Amani
sana.
Ameongeza kuwa
atahakikisha anasimamia utekelezaji waq agizo la Mkuu wa Mkoa La kuipatia timu
hiyo Mizinga hamsini pamoja na kuhakikisha halmashauri inatoa eneo la
utundikaji wa miznga hiyo pamoja na kuitunza.
Naye Mwenyekiti wa
tawi la Misuna stand FC Yahya Said Kisiu amesema wanachama wa timu hiyo
wamepata faraja kubwa sana kwa kutembelewa na Mkuu wa Mkoa pamoja na kuwapatia
mizinga hamsini.
Kisiu ameongeza kuwa
timu hiyo iliyoanzishwa mwaka 2014 ilifanikiwa kufika ligi daraja la pili
lakini kwa sasa imeshuka tena daraja huku akisisitiza kuwa ari mpya waliopatiwa
mkuu wa Mkoa itawezesha timu hiyo kupanda tena daraja.
Wanachama
wa timu ya mpira wa miguu ya Stand Misuna wakifurahia jambo wakati Mkuu wa Mkoa
wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi alipowatembelea mapema leo.
No comments:
Post a Comment