Wahandisi wa miradi ya maendeleo ikiwemo majengo ya madarasa na vituo vya Afya Mkoani Singida wametakiwa kuwa wabunifu na kutumia utaalamu wao katika kuwashauri viongozi kufanya miradi hiyo kwa awamu ili kukamilika kwa wakati na kuweza kuleta tija kwa muda mfupi.
Hayo
yamesemwa leo na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Sahili Geraruma wakati wa
kuweka jiwe la Msingi katika mradi wa shule ya Sekondari Kitalaka iliyopo Halmashauri
ya Itigi wilayani Manyoni.
Gararuma
amesema Wahandisi wanayo nafasi ya kushauri katika ujenzi kulingana na kiasi cha
fedha zilizopo ili kujenga majengo machache yanayokamilika kwa muda mfupi na
yakatumiwa na wanafunzi kuliko kujenga majengo mengi yasiyoisha kwa wakati uliyopangwa.
Amesema miradi mingi haikamiliki kwa wakati kwa
sababu Wahandisi wanashindwa kushauri kulingana na taaluma zao jambo ambalo
linachangia miradi hiyo kutokamilika kwa wakati na kujikuta inahitaji muda wa
ziada.
"Ukifanya
hesabu vizuri utajua kwamba fedha ulizonazo zinaweza kujenga jengo la namna
gani au majengo mangapi, unaona una fedha za June majengo matano na unaanza mpango
unataka majengo kumi kwa nini usishauri yaanze kujengwa kulingana na fedha
iliyopo", aliuliza Geraruma
Amewataka
wasimamizi wa majengo hayo kuwa na Mpango kazi ambao utaonesha ni kila kazi na
muda wake na itasaidia kujipima wenyewe kama kazi waliojipangia inakamilika kwa
wakati.
Aidha akiwa
katika kituo cha Afya Mitundu Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru ameagiza viongozi
wasimamie misingi na maadili ya kazi zao huku akiwasihi mafundi kukagua vifaa
vya ujenzi kabla ya kuvipeleka stoo.
Kiongozi
huyu amebainisha kwamba vipo vifaa kadhaa vimepokelewa katika kazi mbalimbali
za Ujenzi na kuhifadhiwa stoo wakati ndani yake sivyo vilivyokubaliwa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment