Mwenge wa
Uhuru umefikisha siku ya Tatu Mkoani Singida na leo umekabidhiwa Wilaya ya
Singida Vijijini katika viwanja vya Kihonda ambapo walibainisha kwamba Mwenge wa
Uhuru utakimbizwa km 130 Wilayani hapo.
Akipokea Mwenge
wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili amesema Mwenge wa
Uhuru utakagua Miradi mitano na prodramu Tano katika maeneo mbalimbali ya eneo
hilo.
DC Muragili
amesema programu hizo zinahusiana na kupinga Rushwa, Mapambano dhidi ya Malaria,
mapambano dhidi ya UKIMWI/VVU na Lishe Bora kwa wananchi.
Aidha
Muragili amesema programu hizo zinalenga kuondoa viwango vya maambukizi ya
UKIMWI na Malaria ambayo kwa Mkoa wa Singida ni asilimia 2.3 ikilinganishwa na
asilimia 7.3 ya maambukizi ya Malaria ki Mkoa.
Kwa upande
wake Mratibu wa Malaria Wilaya ya Singida Bwana Mafanikio Mamba amesema Wilaya
imechukua hatua kadhaa kupambana na Ugonjwa wa Malaria kwa nia ya kupunguza
maambukizi hasa kwa mama wajawazito.
Amesema kwa
mwaka 2021/22 watu 25,589 walipima Malaria ambapo wanaume walikuwa 9369
wanawake ni 16,220 na kubainika kwamba watu 451 walikuwa na vimelea vya Malaria.
Aidha
Halmashauri ya Singida imegawa vyandarua
25,000 sawa na robota 625 kwenye huduma za kutolea huduma kwa mama wajawazito
na watoto chini ya miaka mitano alisisitiza Bwana Mafanikio.
Wilaya ya
Singida Vijijini imeendelea kutoa elimu ya kujikinga na maagonjwa ya kuambukiza
jkiwemo ukimwi ambapo programu ya VVU/UKIMWI Singida ina vituo 37 vinavyotoa
huduma ya ushauri nasaha na upimaji.
Kwa mujibu
wa Mratibu wa UKIMWI wa Wilaya hiyo amesema jumla ya watu waliopima VVU katika
kipindi cha mwaka 2020 hadi 2021 ni 45162
kati yao wanaume ni 18251 sawa na asilimia 40 na wanawake walikuwa ni
26911 sawa na asilimia 60.
Hata hivyo Mwenge wa Uhuru utaendelea na ukaguzi wa miradi ya maendeleo kesho Agosti 12, 2022 Singida Mjini.
No comments:
Post a Comment