Tuesday, May 22, 2018

"Elimu ni moyo wa uhakika na hakikisho la uhai wa maendeleo endelevu ya familia, jamii na Taifa kwa ujumla”-Dkt. Nchimbi


 Mkuu wa mkoa wa SINGIDA, Dkt. REHEMA NCHIMBI akishauri jambo kuhusu uwasilishwaji wa ujumbe kwanjia ya katuni na kuwataka mashirika na wadau wengine wa Elimu kuacha kubeza jitihda zinazofanywa na Serikali za kuimarisha kiwango na ubora wa elimu hapa nchini.

Mkuu wa mkoa wa SINGIDA, Dkt. REHEMA NCHIMBI akisisitiza jambo kuhusu uwasilishwaji wa ujumbe kwanjia ya katuni alipotembelea banda la TENMET.


Mkuu wa mkoa wa SINGIDA, Dkt. REHEMA NCHIMBI ameyataka mashirika na wadau wengine wa Elimu kuacha kubeza jitihada zinazofanywa na Serikali za kuimarisha kiwango na ubora wa elimu hapa nchini.

Ametoa kauli hiyo wakati akizindua JUMA LA ELIMU DUNIANI ambalo kitaifa lilifanyika Wilaya ya MKALAMA Mkoani SINGIDA.

Dkt. Nchimbi amesisitiza umuhimu wa kutambua changamoto kwa pamoja na umuhimu wa wadau kufanya kazi kwa pamoja ili kutatua changamoto hizo.

Maadhimisho ya Juma hilo la Elimu yalifanyika hivi karibuni katika Wilaya ya MKALAMA ambayo katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka 2017 ilishika nafasi ya mwisho Kitaifa na yanafayika katika Wilaya hii ili kuleta hamasa kwa wadau wa Elimu wakiwemo wazazi kushirikiana kwa pamoja kunusuru hali hiyo.

Kabla ya kufanya uzinduzi huo Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania ambao ndio waandaaji wa JUMA hilo la ELIMU, CATHLEEN SEKWAO pamoja na mambo mengi ameipongeza Serikali kwa hatua inazochukua za kuboresha sekta ya elimu hapa nchini.

Akizindua maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa SINGIDA, Dkt. REHEMA NCHIMBI amesema pamoja na nia nzuri ya wadau wa elimu lakini wapo wanaobeza jitihada zinazofanywa na Serikali kikubwa akilalamikia baadhi ya mabango yaliyoandaliwa katika maadhimisho hayo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), MHE. SELEMAN JAFO alikuwa ni miongoni mwa viongozi walihudhuria uzinduzi huo wa JUMA la Elimu.

Awali mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, JAMES MKWEGA alidai kuwa utaratibu wa kuhamishia walimu watukutu na wazembe kwenye baadhi ya wilaya ikiwemo ya Mkalama kwa lengo la kuwaadhibu ndio chanzo cha Wilaya hiyo kufanya vibaya katika mititahini ya Kitaifa.

Katika maadhimisho hayo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa SINGIDA pia ilitoa pikipiki kwa ajili ya kusaidia kurahisisha shughuli za kiusafiri shule moja wapo Wilayani Mkalama.

Kauli mbiu ya kampeni hii kwa mwaka huu ni
“UWAJIBIKAJI WA PAMOJA KWA ELIMU BORA KWA WOTE”

 Mkuu wa mkoa wa SINGIDA, Dkt. REHEMA NCHIMBI (mwenye kitabu) akionyesha lugha ya ishara alipotembelea banda la wenye mahitaji maalum wakati wa maadhimisho ya Juma la Elimu yaliyofanyika Wilayani Mkalama, yaliyoratibiwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) ikishirikiana na wadau mbalimbali wa elimu, Serikali na Taasisi binafsi.


 Mkuu wa mkoa wa SINGIDA, Dkt. REHEMA NCHIMBI (mwenye kilemba) akionyeshwa vifaa vinavyotumiwa na wanafunzi kwa lugha ya ishara alipotembelea banda la wenye mahitaji maalum.


 Baadhi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum walioshiriki kwenye maadhimisho ya Juma la Elimu yaliyofanyika Wilayani Mkalama, yaliyoratibiwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) ikishirikiana na wadau mbalimbali wa elimu, Serikali na Taasisi binafsi.
Mkuu wa mkoa wa SINGIDA, Dkt. REHEMA NCHIMBI (mwenye skafu), Mkuu wa Wilaya Mkalama Mhandisi, Masaka (Mwenye tai nyekundu), Katibu Tawala wa Mkoa Singida Dkt. Angelina Lutambi pamoja na washiriki wengine wakisikiliza shughuli zinazofanywa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET).

 Mdau akichangia damu salama wakati wa maadhimisho ya Juma la Elimu yaliyofanyika Wilayani Mkalama, yaliyoratibiwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) ikishirikiana na wadau mbalimbali wa elimu, Serikali na Taasisi binafsi.
 Kikundi cha Tarumbeta kikitumbuiza wakati wa maadhimisho ya Juma la Elimu yaliyofanyika Wilayani Mkalama, yaliyoratibiwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) ikishirikiana na wadau mbalimbali wa elimu, Serikali na taasisi binafsi.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), MHE. SELEMAN JAFO akipokelewa na Mhe. Mkuu wa mkoa wa SINGIDA, Dkt. REHEMA NCHIMBI mara baada ya kuwasili viwanjani wakati wa maadhimisho ya Juma la Elimu yaliyofanyika Wilayani Mkalama, yaliyoratibiwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) ikishirikiana na wadau mbalimbali wa elimu, Serikali na Taasisi binafsi.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), MHE. SELEMAN JAFO akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhandisi Masaka, mara baada ya kuwasili wilayani Mkalama.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), MHE. SELEMAN JAFO akisalimiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina M.  Lutambi mara baada ya kuwasili Wilayani Mkalama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), MHE. SELEMAN JAFO akisalimiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina M.  Lutambi, Mbunge wa Mkalama, Mhe. Allan Mkumbo pamoja na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya mara baada ya kuwasili Wilayani Mkalama.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), MHE. SELEMAN JAFO (mwenye tai) akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi Mkalama mara baada ya kuwasili wilayani Mkalama.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), MHE. SELEMAN JAFO akiteta jambo na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi kabla ya kuzungumza na wananchi waliohudhulia wakati wa maadhimisho ya Juma la Elimu yaliyofanyika Kitaifa wilayani Mkalama mkoa wa Singida 2018.


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), MHE. SELEMAN JAFO akizungumza na wananchi wa Mkalama wakati wa maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa lililofanyika Wilayani Mkalama mkoa wa Singida.



 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza wakati wa maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yaliyofanyika Wilayani Mkalama, Mkoa wa Singida 2018

 Afisa Elimu Mkoa wa Singida Mwl. Nelasi Mulungu akisoma jumla ya mambo mbalimbali yaliyowasilishwa na timu ya wataalam wa wilaya ya Mkalama kwa kushirikiana na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) na wadau mbalimbali wa elimu Tanzania.

 Mwanafunzi mwenye mahitaji maalum akitoa ushuhuda wa uwezo alionao wa kujua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu.


 Mkurugenzi wa Mkalama Eng. Sanga (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Singida Mhe. Rashid Mandoa wakati wa maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa lililofanyika wilayani Mkalama, mkoa wa Singida 2018.

 Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akito zawadi ya mipira kwa walimu wa shule mbalimbali za Wilaya ya Mkalama wakati wa Juma la Elimu Tanzania 2018.

Mwalimu akishukuru zawadi ya mipira aliyokabidhiwa na  Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi wakati wa Juma la Elimu Tanzania 2018.




 Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida wakati wa siku ya kuahirisha Juma la Elimu Tanzania kitaifa lililofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida 2018.


Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akinadisha zawadi mbalimbali kwa Wakurugenzi wa Wilaya za Mkoa wa Singida wakati wa Juma la Elimu Tanzania  wakati wa  Juma la Elimu Tanzania kitaifa lililofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida 2018.

Baadhi ya zawadi ya mbuzi na kondoo waliotolewa na wanakijiji kupongeza waratibu na wadau walioandaa Juma la Elimu lenye lengo la kuhamasisha maendeleo na kuinua elimu  Wilaya ya Mkalama wakati wa Juma la Elimu Tanzania  kitaifa lililofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida 2018.

 Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na wananchi wa Mkalama mkoani Singida wakati wa kuahirisha Juma la Elimu Tanzania lililofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida 2018.


 Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wake ambao pia ni waratibu wa maadhimisho ya Juma la Elimu Tanzania.
.
Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na mdau wa Mtandao wa Elimu Tanzania wakati wa maadhimisho ya Juma la Elimu Tanzania.

"Elimu ni moyo wa uhakika na hakikisho la uhai wa maendeleo endelevu ya familia, jamii na Taifa kwa ujumla”-Dkt. Nchimbi

No comments:

Post a Comment