Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru kitaifa Amour Hamad Amour akipanda Mkorosho katika eneo la
shule ya Msingi Kipumbuiko, Wilayani Ikungi katika uzinduzi wa upandaji
mikorosho kimkoa.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru kitaifa Amour Hamad Amour akiweka chupa ya maji iliyofungwa na
kutobolewa tundu dogo litakalokuwa likimwagilia kwa matone Mkorosho alioupanda katika
eneo la shule ya Msingi Kipumbuiko, Wilayani Ikungi ambapo maji ya chupa hiyo
yataisha baada ya siku nne katika uzinduzi wa upandaji mikorosho kimkoa.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru kitaifa Amour Hamad Amour akielekezwa na Afisa Kilimo Kijiji cha
Kipumbuiko Esther Bayda namna ya kuuwekea kivuli mche wa mkorosho alioupanda
ili kutunza unyevu unyevu katika eneo la shule ya Msingi Kipumbuiko, Wilayani
Ikungi katika uzinduzi wa upandaji mikorosho kimkoa.
Halmashauri za Mkoa
wa Singida zimetakiwa kusimamia taasisi za serikali zilizopo kwenye maeneo yao
pamoja na wananchi wao wanapanda zao la Korosho ili kuhifadhi mazingira,
kuongeza kipato na kutimiza azma ya kuwa zao la kudumu na la mda mrefu la kibiashara
mkoani hapa.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru kitaifa Amour Hamad Amour ametoa maelekezo hayo wakati mwenge
wa uhuru ukizindua upandaji wa zao la korosho kimkoa uliofanyika katika kijiji cha
Kipumbuiko, Wilayani Ikungi ambapo wakimbiza mwenge kitaifa wameshiriki
upandaji miche ya mikorosho.
Kabla ya kutoa
maelekezo hayo Amour amekagua shamba la korosho la ukubwa wa ekari moja na
miche 28 linalomilikiwa na shule ya msingi Kipumbuiko na kuelekeza kuwa
upandaji mikorosho usiishie hapo bali kila taasisi yenye eneo inapaswa kupanda
mikorosho ya kutosha.
“Leo tumezindua
upandaji mikorosho kimkoa, sasa juhudi hizi zisiishie hapa, Mkurugenzi wa
halmashauri ya Ikungi hakikisha kila taasisi inalima mikorosho ya kutosha ili
lengo la kutunza mazingiza liweze kutimia kwa ufanisi” amesema na kuongeza kuwa,
“Tunapoelekea kwenye
Tanzania ya Viwanda tunapaswa kuongeza uzalishaji wa malighafi za kuhudumia
viwanda vyetu, hivyo basi hamasisheni wananchi wapande mikorosho kwa wingi,
hata mimi nimehamasika na lazima nitalima mikorosho”.
Naye Mkimbiza Mwenge
Kitaifa Fredrick Ndahani amesema zao la korosho limekuwa mkombozi wa uchumi kwa
wananchi wa mikoa ya lindi na mtwara ambako wanaifananisha na dhahabu ya
kijani, hivyo basi mkoa wa Singida unapaswa kusimamia zao hilo lenye manufaa
makubwa.
Ndahani amesema korosho
ni zao ambalo huweza kutumia maji kwa ufanisi kwakuwa inaweza kupandwa hata
kipindi ambapo sio cha mvua nyingi na pia ni zao ambalo huweza kupandwa katika
shamba ambalo lina mazao mengine.
Ameongeza kuwa
wananchi Mkoani Singida wanapaswa kuchangamkia kilimo cha korosho kwakuwa
mavuno yake ni endelevu huku akiwasisitiza kuwatumia na kuwapa ushirikiao wataalamu wa taasisi zinazofanya tafiti na
kutoa elimu ya kilimo cha Korosho.
Kwa upande wake
mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kipumbuiko Mariam Makera amesema wanafunzi na
wananchi wa kijiji hicho kwa kushirikiana na Wilaya ya Ikungi wameanzisha
kilimo cha korosho shuleni hapo ili wananfunzi wajifunze kilimo hicho kwa
vitendo na kuwahamasisha wazazi wao.
Makera amesema
korosho zinazolimwa shambani hapo zimetumia teknolojia ya umwagiliaji maji kwa
njia rahisi ya matone ambayo hutumia maji kwa ufanisi wa hali ya juu.
Zao la korosho Mkoani
Singida limeanza kulimwa mwaka 1970 huku uendelezaji wake kwa Wilaya ya Ikungi
ukianza mwaka 2013 ambapo hadi sasa mikorosho 17,000 imeshapandwa na lengo la
upandaji mikorosho mingine kwa msimu wa mwaka 2017/2018 likiwa mikorosho laki
tano.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru kitaifa Amour Hamad Amour akizindua upandaji mikorosho kimkoa
katika eneo la shule ya Msingi Kipumbuiko Wilayani Ikungi, akishuhudiwa na Mkuu
wa Wiaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu (kulia kwake) na Mkimbiza mwenge
Kitaifa Fredrick Ndahani (kushoto kwake).
Mkimbiza Mwenge wa
Uhuru kitaifa Fredrick Ndahani akiuwekea kivuli mche wa mkorosho alioupanda ili
kutunza unyevu unyevu katika eneo la shule ya Msingi Kipumbuiko, Wilayani
Ikungi katika uzinduzi wa upandaji mikorosho kimkoa.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru kitaifa Amour Hamad Amour akikagua shamba la Mikorosho katika
eneo la shule ya Msingi Kipumbuiko, Wilayani Ikungi katika uzinduzi wa upandaji
mikorosho kimkoa pembeni yake Afisa Kilimo Kijiji cha Kipumbuiko Esther Bayda na
nyuma yake ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu.
No comments:
Post a Comment