Monday, April 23, 2018

MKUU WA MKOA SINGIDA DKT. REHEMA NCHIMBI ASHIRIKI KATIKA IBADA YA UZINDUZI WA MIAKA 22 YA RADIO MARIA TANZANIA ILIYOFANYIKA KATIKA KANISA KUU LA KIASKOFU LA MOYO MTAKATIFU WA YESU, JIMBO KATOLIKI LA SINGIDA


Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewashukuru viongozi wa Radio Maria Tanzania kwa heshima kubwa iliyoipa mkoa wa Singida kwa kuyaleta maadhimisho ya sherehe ya miaka 22 ya Utume wa Uinjilishaji wa Radio Maria Tanzania na kusema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawapongeza sana kwa Miaka 22 ya kuzalia Radio Maria Tanzania. 


Dkt. Nchimbi aliyasema hayo jana katika sherehe ya Uzinduzi wa Miaka 22 ya kuzaliwa Radio Maria Tanzania katika kufikisha ujumbe kwa wananchi, "Utume unaofanywa na Radio Maria ni msaada mkubwa sana kwa Serikali maana Neno la Mungu linaingia mpaka nyumbani mwetu" alisema. 

"Watu ambao walifikiwa na Neno la Mungu kupitia Radio Maria Tanzania na wakawa waadirifu, waaminifu, wakatii miito, wakawa wakweli, wakapenda kufanya kazi, watu wenye hofu ya Mungu, wakatii sheria bila shuruti, kwa vyovyote ndio furaha ya Serikali" alisisitiza Dkt Nchimbi.

Aidha, katika uzinduzi huo wa miaka 22 ya kuzaliwa Radio Maria Tanzania Jimbo Kuu Katoliki la Singida liliweza kuchangia fedha taslimu na ahadi kwa Utume wa Radio Maria Tanzania kiasi cha shilingi Milioni 20 ambapo zoezi hilo liliendeshwa na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.

Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida ambaye pia ndiye mgeni rasmi wa sherehe za Uzinduzi wa Miaka 22 ya Radio Maria Tanzania akipongezwa na Mhashamu Baba Askofu Edward Mapunda wa Jimbo Katoliki la Singida mara baada ya kumtunuku Cheti cha shukrani kwa kufanya Utume wa Radio Maria katika uhamasishaji na uimarishaji wa Utume wa Radio Maria Tanzania.
 Mhashamu Baba Askofu Edward Mapunda akiongoza Ibada ya Misa Takatifu wakati wa Uzinduzi wa sherehe za miaka 22 ya kuzaliwa Radio Maria Tanzania iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Moyo Mtakatifu wa Yesu, Jimbo Katoliki la Singida mkoani Singida.

Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida ambaye pia ndiye mgeni rasmi wa sherehe za Uzinduzi wa Miaka 22 ya Radio Maria Tanzania akizungumza na Waumini waliofika kushuhudia Uzinduzi wa sherehe za miaka 22 ya kuzaliwa Radio Maria Tanzania.Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida ambaye pia ndiye mgeni rasmi wa sherehe za Uzinduzi wa Miaka 22 ya Radio Maria Tanzania akiongea na Waumini waliofika kushuhudia Uzinduzi wa sherehe za miaka 22 ya kuzaliwa Radio Maria Tanzania.


Waumini wakifurahia jambo wakati Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza wakati Ibada ya Misa na sherehe za Uzinduzi wa Miaka 22 ya kuzaliwa Radio Maria Tanzania.


Mhashamu Baba Askofu Benard Mapunda akimkabidhi Baba Padri zawadi ya Rozari zilizotolewa na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (ambaye ndiye mgeni rasmi) katika maadhimisho ya Uzinduzi wa sherehe ya Miaka 22 ya kuzaliwa Radio Maria Tanzania.

 Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Elias Tarimo akichangia Utume  wa Radio Maria Tanzania wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Miaka 22 ya kuzaliwa Radio Maria Tanzania.


Umoja wa Wanakwaya wa Kanisa Kuu la Kiaskofu la Moyo Mtakatifu wa Yesu Jimbo Katoliki la Singida wakiimba kwa furaha wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Miaka 22 ya kuzaliwa Radio Maria Tanzania.


Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wakwanza kulia), Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Elias Tarimo (katikati) na Mbunge wa Singida Kaskazini Mhe. Justine Monko (wakwanza kushoto)  wakicheza kwa madaha wimbo wenye asili na milindomo ya Kinyaturu wakati wa maadhimisho ya Uzinduzi wa Miaka 22 ya Radio Maria Tanzania katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Moyo Mtakatifu wa Yesu Jimbo Katoliki la Singida.

Waheshimiwa Mapadri wa Jimbo Katoliki Singida wakiongozwa na mtunzi wa nyimbo Padri Nkoko wa Parokia ya Kristo Mfalme Kibaoni Singida wakicheza kwa madaha wimbo wenye asili na milindomo ya Kinyaturu wakati wa maadhimisho ya Uzinduzi wa Miaka 22 ya Radio Maria Tanzania katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Moyo Mtakatifu wa Yesu Jimbo Katoliki la Singida.

Waheshimiwa Mapadri wa Jimbo Katoliki Singida wakiongozwa na mtunzi wa nyimbo Padri Nkoko wa Parokia ya Kristo Mfalme Kibaoni Singida wakicheza kwa madaha wimbo wenye asili na milindomo ya Kinyaturu wakati wa maadhimisho ya Uzinduzi wa Miaka 22 ya Radio Maria Tanzania katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Moyo Mtakatifu wa Yesu Jimbo katoliki la Singida.


Mhe. Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Singida Mhashamu Bernard Mapunda pamoja na Mapadri wakicheza kwa madaha wimbo wenye asili na milindomo ya Kinyaturu wakati wa maadhimisho ya Uzinduzi wa Miaka 22 ya Radio Maria Tanzania katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Moyo Mtakatifu wa Yesu Jimbo Katoliki la Singida.

 Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (Mgeni rasmi wa sherehe) akiongoza zoezi la uchangizi wa Utume wa Radio Maria Tanzania wakati wa sherehe za Uzinduzi.

Mhe. Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Singida Mhashamu Bernard Mapunda akichangia Utume wa Radio Maria Tanzania zoezi lililosimamiwa na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi wakati wa maadhimisho ya Uzinduzi wa Miaka 22 ya Radio Maria Tanzania katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Moyo Mtakatifu wa Yesu Jimbo Katoliki la Singida.
Viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Singida wakiongozwa na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi wakiitikia wito wa kuchangia Utume wa Radio Maria Tanzania.

Viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Singida wakiongozwa na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi wakiitikia wito wa kuchangia Utume wa Radio Maria Tanzania.
Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ambaye pia ndiye mgeni rasmi wa sherehe za Uzinduzi wa Miaka 22 ya Radio Maria Tanzania akitoa neno la shukrani na kukabidhi michango iliyokusanywa kutoka kwa Serikali ya Mkoa wa Singida kwa  ajili ya kuimarisha Utume wa Radio Maria Tanzania.

No comments:

Post a Comment