A. Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini na Madhehebu mbalimbali Mkoa wa Singida,(aliyesimama)Hamis Muhamed Kisuke akiongoza kikao ambapo walizungumzia hali ya amani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu na kuja na maazimo saba. (Picha na Rose Nyangasa).
MMkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini na Madhehebu mbalimbali Mkoa wa Singida ambapo ameipongeza Kamati hiyo kwa kuamua kuhamasisha amani na utulivu kwenye kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu (Picha na Rose Nyangasa).
A. Wajumbe wa Kamati ya Amani Mkoa wa Singida wakimsikiliza kwa makini Kamanda wa Polisi wa MKoa wa Singida, Sweetbert Njewike (hayupo pichani) wakati akielezea majukumu ya jeshi hilo kwenye siku ya upigaji kura Oktoba 28, mwaka huu. (Picha na Rose Nyangasa).
John Mapepele na Rose Nyangasa, Singida
Akisoma maazimio hayo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Shehe, Hamis Muhamed Kisuke
amesema miongoni mwa maazimio hayo
ni kuwaomba waumini wao kutenga siku
tatu kuanzia Ijumaa hadi Jumapili ya juma hili kwa ajili ya kufunga na kuomba ili kuombea uchaguzi upite kwa
amani na usalama.
Maazimio mengine yaliyofikiwa
kwenye kikao hicho ni pamoja na viongozi
wa dini katika kipindi hiki kudumisha
Amani, kutotumika kwenye
majukwaani ya siasa kushabikia viongozi
wa vyama vya siasa, kuhubiri Amani,
kuhimiza waumini wao kushiriki kupiga kura na kuhimiza kufuata na kutii
sheria za nchi ambapo pia wamesisitiza kuviacha vyombo halali vilivyopewa dhamana ya kusimamia
uchaguzi huo vifanye kazi yake.
Mwakilishi wa dini ya Kiislam (Baraza la Kiislam
Tanzania) katika Mkoa wa Singida Shehe,
Issa Nassor amesema Amani ikitoweka watakaoumia
zaidi ni watoto, wanawake,
wajawazito, wazee na watu wenye mahitaji
maalum kwa kuwa hawana uwezo wa
kukimbia na kujitetea.
Aidha,
wamewataka wazazi na walezi wa
kila familia kuwaasa vijana
kujiepusha na kushawishiwa na
watu wanaoitakia mabaya nchi ya Tanzania ambapo ameongeza kwamba
baada ya kupiga kura vijana warejee nyumbani
kwa kuwa tayari Serikali
imeshaweka vyombo maalum kwa ajili kuhesabu na kutangaza matokeo hayo.
“Historia inaonyesha kuwa nchi zote duniani
zilizopoteza amani ni nchi ambazo walilewa amani, vilevile tukumbuke kupata
amani ni mchakao wakati kuvunja
amani ni jambo rahisi kabisa. Nawaomba watanzania wenzangu kutumia
vipande vyetu vya kupigia kura kuwachagua
Viongozi bora” aliongeza Shehe,
Nassor
Mwakilishi kwa upande wa wakristo, Askofu wa Kanisa la
TAG mkoani Singida, Gasper Mdimi amesema
amani ya nchi ni jambo nyeti
ambalo linatakiwa kuchukuliwa
kwa uangalifu mkubwa kwa kuwa
lina athari pana kuanzia
kwenye ngazi ya kaya
hadi taifa kwa ujumla na
kwamba Bibilia imefafanua kuwa chanzo cha Amani ni
Mungu mwenyewe, Haki na Watu wanaomcha
Mungu.
Amefafanua kuwa
vitabu vyote vitakatifu vinasisitiza kutafuta kuwa
na amani na watu wote ambapo na kwamba watanzania wanatakiwa kupendana katika kipindi hiki bila kuangalia
vyama vyao vya Siasa
na kuiombea nchi yao ipate
viongozi ambao watailinda amani.
Pia amesema
wakati wananchi wanakwenda katika siku za mwisho wa kuhitimisha zoezi la
kuwachagua viongozi ni muhimu
kuzingatia kuacha kuongea maneno
ambayo yatasababisha machafuko na
uvunjifu wa amani.
Mwakilishi wa Mhashamu Baba Askofu wa Jimbo
Katoliki la Singida, Padre Padri Elia Mnyakanka amesema Uongozi Bora ni
tunu na zao la amani na kwamba
ili kuwa na maendeleo na ustawi
kuanzia ngazi ya familia na taifa ni muhimu kwa wananchi kutafakari kwa kina na kuwachagua viongozi wanaoweza kuilinda
amani.
Akitoa mfano amesema katika taifa la Israel uongozi
bora ulikuwa ni nyenzo ya kuwafikisha
kwenye nchi ya ahadi kupitia manabii mbalimbali ambapo kwa kufanya hivyo
amani ilipatikana.
Amesema
viongozi wa dini wanapaswa kuwapa
elimu ya uraia waumini wao ili
kuwapa uwezo wa
kuwachagua wagombea makini
kupitia ilani zao ambapo amesisitiza
kwamba uchaguzi wa haki na amani ndiyo njia pekee ya kujitawala na
kuleta amani katika nchi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike amesema kwenye kipindi hiki cha uchaguzi majukumu yao ni pamoja na
kutunza na kudumisha Amani, kusimamia utekelezaji wa sheria, kuzuia na
kubaini makosa ya jinai, kuwakamata wahalifu wanaohatarisha amani na
kuwafikisha katika vyombo vya sheria, kulinda
mali za raia, kutoa ulinzi kwa maafisa na vituo, pia kuhakikisha hakuna
mtu anaye watishia wapiga kura na kuhakikisha usalama wa vifaa vya kupigia
kura.
Mkuu wa Mkoa Singida Dkt.Rehema Nchimbi amewashukuru
viongozi hao kwa kuandaa mkutano huu ambao
umelenga kudumisha amani na kuwahimiza wananchi washiriki kikamilifu kupiga kura ili kuwa chagua viongozi bora.
Aidha Dkt.Nchimbi amewataka Viongozi wa Dini kutotumika kuharibu amani na mshikamano ambao upo kwa kipindi kirefu sasa hapa nchini kutokana na kazi nzuri ya kusimamia amani hiyo iliyofanywa na Serikali.
No comments:
Post a Comment