Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge leo amefunga Mafunzo wakufunzi yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Social uliopo mjijini hapo wakijiusisha wataalamu mbalimbali wa upimaji wa ardhi na wachora ramani kutoka maeneo mbalimba hapa Nchini.
Mafunzo hayo yalidumu kwa muda wa Siku kumi (10) na yalilenga kuwafundisha wataalamu namna ya
kubadilisha data ziwe kijiditali ambapo watawafundisha wengine katika mikoa
mbalimbali.
Akiongea katika Mafunzo hayo RC Mahenge amewataka vijana hao
kutumia vyema mafunzo waliyoyapata ili
taarifa hizo ziweze kutumika kikamilifu katika uwekaji wa anwani za Makazi.
Amewataka wakufunzi hao kutumia muda uliobaki kufikia Siku
ya sensa kwa kuhakikisha wanakamilisha zoezi la kutoa Mafunzo kwa wengine ili
kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Naye Kamishina
Msaidizi wa Ardhi Shamimu Hoza amesema kundi hilo la vijana baada ya
Mafunzo hayo litasambazwa katika mikoa Saba ili kutoa elimu na kuendeleza kazi
ya ubadilishaji wa taarifa kwenda katika digitali.
Aidha kundi hilo lenye vijana wapatao 47 kutoka mikoa
mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani linategemewa kuchochea mabadiliko
makubwa katika kuyafikia malengo iliojiwekea alifafanua Kamishna
Amesema taarifa hizo zitasaidia kubaini maeneo ya makazi
hifadhi na maeneo yenye matumizi mengineyo hasa katika kipindi hiki cha kuweka
Anwani za Makazi alifafanua Shamimu
Hata hivyo Shamimu alimalizia kwa kuziomba taasisi nyingine kutoa ushirikiano au msaada wowote utakapohitajika hasa katika matumizi ya Tehama au endapo vitendea kazi vitaleta usumbufu wa aina yeyote.
No comments:
Post a Comment