Mkuu wa Willaya ya Singida Mhandisi Pasikas Muragili akiongewa na wananchi wa kijiji cha mughunga kuhusu marufuku ya serikali kuingia kwenye hifadhi ya msitu wa Mugori
Mkuu wa Mkoa wa Singida Binilith Mahenge akimiskiliza ,weyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC Eliya Digha walipotembelea Hifadhi ya msitu wa migori hivi karibuni kujione uharibifu unaoendelea.
wananchi wa Kijiji cha Mghunga wakimsikiza Mkuu wa Mkoa wakati wa ziara yake aliyoifanya hivi karibuni alipokuwa akitolea ufafanuzi juu ya uvamizi wa mistu pamoja hatma ya wale waliondolewa katika eneo la hifadhi ya msitu.
Mkuu wa Mkoa akiendelea na Mkutano
Serikali imedhamiria kuwaondoa wavamizi wa Hifadhi ya msitu wa
Mgori wenye ukubwa wa kilomita za mraba elifu 49 ambao umevamiwa na wnanchi
kutoka maeneo mbalimbali kwa lengo la kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo ujenzi
kilimo uvufugaji na uchomaji wa mkaa hivyo kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.
Akiongea wakati wa ziara yake iliyofanyika hivi karibuni katika hifadhi ya msitu huo Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dk. Binilith Mahenge akiwataka wananchi wote waliovamia kuondoka
wenyewe huku akiwataka wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kwa
kushirikiana na kamanda wa polisi Mkoa wa singida Kuhafanya doria na kuwakamata
wote watakao kaidi agizo hilo.
RC Mahenge amesema, uharibifu wa msitu huo umeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana ambapo alijioea alipotembelea
eneo hilo na kutoa maagizo ya kutolewa kwa elimu ili wavamizi waweze kuondoka
wenyewe lakini bado hali imeendelea kuwa mbaya baada ya wengine kuja na
kuanzisha makazi eneo hilo.
“Si mara ya kwanza kutembelea msitu huu leo ni mara ya pili
lakini naona uharibifu umeendelea kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na mwaka
jana natoa maelekezo mengine kwa wakala wa huduma ya misitu Tanzania na TFS kwa
kushirikiana na kamamnda wa polis mkoa kufanya doria katika eneo hili kila wiki
mara moja na na nitafanya mawasiliano na wiazara ya maliasili na utalii ili
kuona namna ambavyo wanaweza kuingiza msitu huu kwenye hifadhi zaio.” Alisema RC
Mahenge.
Aidha amemuelekeza
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Pasikas Muragili kuhakikisha ulinzi shirikishi
unakuwepo kwa kuwashirikisha wananchi na viongozi wa vijiji vinazunguka
msitu ikiwa na pamoja na kuandaa mkakati
wa muda mrefu wa namna ya kulinda msitu huo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Mhandisi Pasikasi Muragili amemueleza
mkuu wa mkoa huo kwamba walitoa elimu katika vijiji vyote vinavyoizunguka hifadhi hiyo
ikiwemo kuwachukulia hatua baadhi ya viongozi ambao walionekana kushiriki
kuwaingiza waavamizia ndani ya msitu ambapo kesi zao bado zinaendelea.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Singida Vijijini Elia Digha akaiomba serikali kutilia mkazio ulizi wa
msitu huo ambao kwa mkoa wa singida umebaki mmoja TU,huku akieleza kwamba
tayari wapo wananchi ambao wamevamia
katika kijiji cha Muhunga kata ya Mgori wilaya ya singida.
Mwenyekiti huyo amesema kwamba zoezi la kuwandoa wavamizi hao
limefanika Zaidi ya mara moja lakini inaonekana kuja wengine wapya jambo ambalo
linahitaji ushirikiano baina ya serikali ili kulimaliza kabisa.
Hata havyo amesesisitiza kwamba wapo wananchi waliha ondolewa
ambao bado wanasubuiria serikali kuwapatia eneo jingine la makazi na kilimo
jambao ambalo Mwenyekiti huyo alibainisha kwamba serikali inaweza kulifikiria
na kulitolewa majawabui ili wananchi hao waweze kufahamu kinachoendelea.
Kwa
upande wake Diwani wa Kata ya Mughunga ,
Nassoro Hassan amesema uvamizi wa msitu
unasababishwa na ulizni mdogo ambapo doria ya mara kwa mara imeonekana kwuwa
muoarobaini wa changamooto hiyo.
Amesema wananchi wa kijiji chake wapo tayari
endepo watapatiwa polisi hata wawili
kushiri kikamilifu kuwaondoa waavamizi hao kwa kuwa wamekuwa ni hatari hata kwa
maisha yao kutokana na wavamizi hao kutumia
silaha za jadi kama upinde na mishale kupambana na watu wanaowazuia kuingia
katika msitu huo.
Awali
akitoa taarifa yake kwa Mkuu wa Mkoa Muhifadhi
wa Misitu wa Wilaya ya Singida, Uswege Mwasumbi amesema tokea maagizo ya serikali ya kulinda
msitu huo mwaka jana kutolewa wamchoma vibanda 704 vilivyokuwa vimejengwa kwenye
hifadhi na kuwaondoa watu kwenye makazi hayo lakini inaonekana bado wanarudi au
kuja wengine.
Amesema
maelekezo yaliyotolewa na viongozi hao watayatekeleza ikiwemo ya kufanya doria
ya mara kwa mara pamoja na kuchoma moto vibanda vitakavyojengwa na kuwafungulia
mahstaka wote watakokuwa wamekamatwa katika msitu huo.
Baadhi
ya wananchi wa Kijiji cha Mughunga
wameiomba serikali kuwapatia maeneo ya kulima na kujenga nyumba kwa kuwa
wameondolewa katika eneo la hifadhi ambalo walingia kwa kutojua kama ni eneo la
msitu jambo ambalo lilitolewa ufafanuzi na mkuu wa wailaya hiyo Mhandisi
Pasikasi Muragili kwamba tayari wananendelea na utaratibu wa upimaji ili kuweza
kuyatenganisha mazeneo ya makazi na higfadhai
Hata
hivyo RC Mahenge alitawataka waanchi hao waliokubali kuondoka katika eneo la msitu
kuendelea na utulivu walionao wakati serikali ikiangalia namna ya kuwapatia maeneo mengine mbadala.
Mwisho
No comments:
Post a Comment