Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Rahabu Mwagisa (kushoto) akisoma bango lenye ujumbe maalumu wa uzinduzi wa mradi wa Kilimo Biashara (MABADILIKO YA SEKTA YA KILIMO ILI KULETA AJIRA ZENYE STAHA KWA WANAWAKE NA VIJANA TANZANIA)
Akiongea wakati wa kuzindua mradi huo kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa Mhe. Rahabu Mwagisa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni
amesema kupitia mradi huo wakulima wadogo watasaidiwa mnyororo wa thamani wa
mazao ya mahindi, mbaazi, mtama, na
alizeti na kuunganishwa na masoko.
Rahabu
amesema mradi huo utasaidia uwepo wa ushirikiano
baina ya sekta binafsi, na kutengeneza
ajira kwa watu wengi lengo likiwa ni kufanya Mkoa kuwa kituo cha ubora (center
of excellence) katika kuboresha maisha ya wakulima wadogo.
Hata
hivyo amesisitiza kwamba mradi utawanufaisha wakulima wapatao 6,000 ikiwa ni
pamoja na kusaidia mnyororo wa thamani katika mazao mbalimbali ili wakulima wadogo
waweze kuchagua zao linalofaa kwa mahitaji na kupanua wigo wa uzalishaji wa
bidhaa.
Mradi
huo utakuwa unatekelezwa katika wilaya
za Ikungi, manyoni na iramba ambapo wakulima wadogo wa mazao ya alizeti mahindi
mtama na mbaazi watafaidika.
Aidha
DC huyo amebainisha mradi huo utakuwa na jukumi la upatikanaji wa chakula cha familia, udhibiti
wa kifedha, na fursa za uwekezaji kupitia Vikundi vya Akiba, Wazalishaji na
Vijiji vya Biashara kwa wakulima wadogo, wanawake na vijana; na kuwaunganishaji
wakulima na taasisi mbali mbali za kifedha na bidhaa za huduma za kifedha zinazopatikana .
“ mradi mpya unalenga kuboresha maisha ya
wakulima wadogo 6,000 katika Mkoa wetu kwa kuimarisha miundo ya kusaidia
biashara na mnyororo wa thamani wa mazao ya mahindi, mbaazi, mtama, na alizeti” Alikaririwa Rahabu
Aidha
ameendelea kufafanua kwamba Mradi huo
umeanza kwa wakati muaafaka ambapo Mkoa wa Singida unatekeleza mpango wa kukuza na uzalishaji wa zao la alizeti
unaolenga kuongeza uzalishaji wa mafuta ya alizeti kutoka tani 90,000 hadi tani 242,500 sawa na 54% ya jumla ya uagizaji
wa mafuta ya kupikia kitaifa.
Amesema
kwamba mpango kamili wa uzalishaji wa alizeti utajumuisha washikadau anuwai
wakiwemo wakulima wadogo, vyama vya ushirika, asasi za kiraia, wakulima
wakubwa, Wizara ya Kilimo, na Sekta Binafsi.
Aidha
DC huyo ameishukuru Wizara ya Kilimo kwa utayari wao wa kuwajengea uwezo Maafisa Ugani wa kilimo kwa kuwapa ujuzi
unaohitajika na vifaa vya kufanya kazi ili kuwasaidia vya kutosha wakulima wa
Alizeti ikiwa ni pamoja na kutoa ruzuku ya mbegu bora za alizeti kwa wakulima
wadogo.
“Matarajio ya uongozi wa Mkoa wa Singida na
Wizara ya Kilimo katika utekelezaji wa
" Mpango
wa uwezeshaji Uboreshaji wa Maisha ya jamii
kupitia mradi wa kilimo cha kibiashara” ni kwamba utainua uchumi wa wakulima
wadogowadogo kupitia kuongezeka kwa tija ya mazao yatakayowezeshwa na mradi huu”.
Alisema DC.Rahabu
Naye
mratibu wa mradi huo Bw. Ivo Manyaku alisema mradi huo ni maalumu kwa vijana na
wanawake na ni muendelezo wa vikundi vilivyokuwa vikitumika katika mradi wa
awali wa kuweka na kukopa.
Vikundi
hivyo vya kuweka na kukopa ndivyo tunavyovigeuza kuwa vikundi vya wakulima ambavyo pia vitakuwa vikipata mikopo kutoka
katika vikundi walivyoanzisha. Alisema Bw. Manyaku.
Aidha
amebainisha kwamba mradi huo utawaunganisha wakulima na wafanyabiashara wakubwa ili kupata mahitaji na aina ya mazao
yanayohitajika sambamba na uzalishaji wenye ubora.
Hata
hivyo wakulima wengi mkoani Singida wamekuwa wakiuza mazao yao yakiwa
shambani jambo ambalo limekuwa
likiwasababishia hasara, hivyo mradi huu
utahakikisha kwamba wanaongeza thamani mazao yao kabla ya kuyauza. Alisisitiza bwana Mnyaku
Mnyaku
aliendelea kusema kwamba vikundi vya wakulima vya kuweka na kukopa vitatumika pia katika kuwakopesha wakulima
wakati wakiendelea kusubiri bei nzuri ya mazao yao.
Pamoja
na mambo mengi mradi huo utaanzisha mashamba darasa na mashamba ya mfano ambayo
yatatumika kama kielelezo cha mbegu na mbolea bora zitakazotumiwa na wakulima
wa vijiji husika.
Amemalizia
kwa kusema mradi utaanzisha maoneho ya vijijiji ya biashara ambapo yatakuwa ni
makutano ya wakulima wa maafisa ugani, wakulima na wanunuzi ili kujadili
mahitaji sahihi ya kilimo husika.
Mwisho
No comments:
Post a Comment