Thursday, October 08, 2015

MWENGE WA UHURU WILAYANI MANYONI.

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Juma Khatib Chum na mkimbiza mwenge kitaifa Delina Friday Semfukwe wakimsikiliza mwanafunzi wa sekondari ya Manyoni akitoa maelezo ya namna ya kuchanganya kemikali mara baada ya  Kiongozi huyo kuzindua jengo hilo la maabara.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Juma Khatib Chum akizindua Mradi wa ushonaji wa viatu kutoka kwa wadau wa Ngozi wilayani Manyoni.
 
Mkimbiza mwenge kitaifa Anold George Litimba akinunua viatu kutoka katika mradi wa wadau wa Ngozi wilayani Manyoni mara baada ya amradi huo kuzinduliwa.
 
Mkimbiza mwenge kitaifa Karim Haruna Mzee akiangalia kiatu ambacho ni bidhaa iliyotengenezwa katika mradi wa ushonaji wa viatu kutoka kwa wadau wa ngozi Wilayani Manyoni.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Juma Khatib Chum akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa daraja la Mwiboo-Makutupora lililopo Wilayani Manyoni.

Mkimbiza mwenge wa uhuru Hassan Hakim Mohamed akikagua ujenzi wa daraja la Mwiboo- Makutopora wakati Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Juma Khatib Chum akiweka jiwe la msingi katika daraja hilo.
Wakimbiza mwenge kitaifa Bakia Abdalah Khamis na Delina Friday Semfukwe wakiangalia ng'ombe wakioshwa katika josho lililowekewa jiwe la msingi na Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Juma Khatib Chum katika kijiji cha Maweni Wilayani Manyoni.
 
Mkimbiza mwenge kitaifa Delina Friday Semfukwe akiangalia ng'ombe wakioshwa katika josho lililowekewa jiwe la msingi na Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Juma Khatib Chum katika kijiji cha Maweni Wilayani Manyoni.

No comments:

Post a Comment