Thursday, October 08, 2015

MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI SINGIDA ZAMALIZIKA SALAMA NA KWA SHAMRASHAMRA.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Aziza Mumba akimkabidhi mwege wa uhuru Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge katika kijiji cha Mpendoo mpakani mwa Mikoa ya Dodoma na Singida tarehe 7 October 2015.
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge akiupokea mwenge wa uhuru kutoka Mkoa wa Singida katika kijiji cha Mpendoo mpakani mwa Mikoa ya Dodoma na Singida tarehe 7 October 2015.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Aziza Mumba akiagana na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Juma Khatib Chum kabla ya kuelekea Mkoani Dodoma kukamilisha mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2015.
Mratibu wa mbio za mwenge wa uhuru Mkoa wa Singida Yusufu Makulo akiwashukuru viongozi wote wa Mkoa wa Singida na halmashauri zote kwa ushirikiano na mapokezi mazuri ya mwenge wa uhuru mwaka huu.
Mkoa wa Singida ukiuaga mwenge wa uhuru kwa Shamrashamra katika viwanja vya makabidhiano ya mwenge wa uhuru kwa Mkoa wa Dodoma.

No comments:

Post a Comment