Monday, October 05, 2015

MIRADI BORA NA YA MFANO WA KUIGWA YAZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU WILAYA ZA MKALAMA NA IRAMBA.

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2015 Juma Khatib Chum akizindua mradi wa kilimo cha mazao ya bustani kwa njia ya umwagiliaji kijiji cha mwanga Wilayani Mkalama. Mradi huo wa bustani una vikundi 15 na hujikita katika kuzalisha mazao ya vitunguu, mbegu za vitunguu, mahindi na mbogamboga; unawanufaisha vijana Zaidi ya 100 wa kijiji hicho.
 
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2015 Juma Khatib Chum akiwa ameshika vitunguu vilivyovunwa katika bustani ya umwagiliaji kijiji cha mwanga Wilayani Mkalama. Mradi huo wa bustani una vikundi 15 na hujikita katika kuzalisha mazao ya vitunguu, mbegu za vitunguu, mahindi na mbogamboga na unawanufaisha vijana Zaidi ya 100 wa kijiji hicho.
 
Sehemu ya mradi wa kilimo cha mazao ya bustani kwa njia ya umwagiliaji kijiji cha mwanga Wilayani Mkalama. Mradi huo wa bustani una vikundi 15 na hujikita katika kuzalisha mazao ya vitunguu, mbegu za vitunguu, mahindi na mbogamboga, unawanufaisha vijana Zaidi ya 100 wa kijiji hicho.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2015 Juma Khatib Chum akitabasamu mara baada ya kumkabidhi mzazi wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi(albino) simu ya mkononi, kadi ya malipo ya uchangiaji wa huduma za afya yaani CHF, filimbi na kofia katika kijiji cha nduguti Wilayani Mkalama. Mradi huo umelenga kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi wilayani hapo ili waweze kuwa na uhakika wa kupata huduma za afya na uwezo wa mawasiliano kwa vyombo husika mara wapatapo matatizo.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2015 Juma Khatib Chum akimkabidhi binti mwenye ulemavu wa ngozi(albino) simu ya mkononi, kadi ya malipo ya uchangiaji wa huduma za afya yaani CHF, filimbi na kofia katika kijiji cha nduguti Wilayani Mkalama. Mradi huo umelenga kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi wilayani hapo ili waweze kuwa na uhakika wa kupata huduma za afya na uwezo wa mawasiliano kwa vyombo husika mara wapatapo matatizo.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2015 Juma Khatib Chum akimkabidhi mtoto mwenye ulemavu wa ngozi(albino) simu ya mkononi, kadi ya malipo ya uchangiaji wa huduma za afya yaani CHF, filimbi na kofia katika kijiji cha nduguti Wilayani Mkalama. Mradi huo umelenga kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi wilayani hapo ili waweze kuwa na uhakika wa kupata huduma za afya na uwezo wa mawasiliano kwa vyombo husika mara wapatapo matatizo.




Zaidi ya misokoto 100 ya bangi ikiwa imewekwa katika shimo tayari kwa kuteketezwa na Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2015 Juma Khatib Chum katika Sekondari ya Lulumba Wilayani Iramba. Pia Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Juma Chum alitembelea klabu ya kupambana na dawa za kulevya iliyoko shuleni hapo, aidha alipata fursa ya kusikiliza ushuhuda wa vijana wawili waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya na sasa wameacha. 
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2015 Juma Khatib Chum akijiandaa kutekeza zaidi ya misokoto 100 ya bangi.
Misokoto ya bangi ikiteketea.
 
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2015 Juma Khatib Chum akishuhudia misokoto ya bangi ikiendelea kuteketea.
Mkimbiza mwenge kitaifa Bakia Abdalah akiwa amesimama mbele ya nyumba bora ya mwananchi wa kijiji cha Mampanta Wilayani Iramba.
Mwananchi wa Kijiji cha Mampanta na mmiliki wa nyumba bora (aliyeshika kipaza sauti)  akiteta jambo na wakimbiza mwenge wa uhuru kitaifa mara baada ya  ufunguzi wa nyumba yake, aliyejifunika kanga ni mke wa mwenye nyumba huyo. Nyumba hiyo imejengwa kutokana na kipato cha mwananchi huyo ambaye ni mkulima na mfugaji.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2015 Juma Khatib Chum akimpa mwanachi huyo mwenge wa uhuru aweze kuushika. 


No comments:

Post a Comment