Friday, March 31, 2017

TANGAZO TANGAZO TANGAZO

Kliniki Tembezi ya Madaktari Bingwa

Wananchi wote mnatangaziwa kuwa kutakuwa na zoezi la kliniki tembezi ya madaktari bingwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kuanzia tarehe 3 April 2017 mpaka tarehe 7 April 2017. Madaktari bingwa wa magonjwa ya akina mama, magonjwa ya macho, magonjwa ya ndani, magonjwa ya meno, daktari bingwa wa upasuaji, magonjwa ya mifupa, magonjwa ya mfumo wa mkojo,  magonjwa ya masikio, pua na koo na magonjwa ya watoto watakuwepo kuwahudumia kwa gharama nafuu sana. Wote mnakaribishwa na atayeona tangazo hili tafadhali mjulishe na mwenzako.   Tangazo hili pia linapatikana katika tovuti rasmi ya mkoa wa Singida, bonyeza www.singida.go.tz  sehemu ya matangazo utaliona.

No comments:

Post a Comment