Saturday, April 05, 2014

KIKAO CHA 36 CHA BODI YA BARABARA YA MKOA WA SINGIDA APRIL 5, 2014.

Mwenyekiti wa Bodi ya barabara ya Mkoa wa Singida, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko V. Kone (katikati) akiendesha kikao cha 36 cha Bodi ya barabara ya Mkoa wa Singida leo asubuhi, Kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya barabara ya Mkoa wa Singida, Mbunge wa Singida Magharibi Mohamedi Misanga, na kulia kwake ni Katibu wa Bodi hiyo Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Liana Hassan. 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko. V. Kone amewataka watendaji wote wa Mkoa wa Singida kuwahudumia wananchi kwa wakati bila ya kusubiri vikao kwani kwa kufanya hivyo ni kuchelewesha huduma kwa Wananchi.

Dkt. Kone ameyasema hayo leo asubuhi katika kikao cha 36 cha bodi ya barabara ya Mkoa wa Singida huku akisisitiza kuwa kufanya hivyo ni kutaka kuonekana kwenye vyombo vya habari huku huduma kwa wananchi zikicheleweshwa.

Aidha amesema sekta ya barabara ni miongoni mwa sekta ambazo zimeainishwa na Serikali katika Mpango wa Matokeo Makubwa sasa hivyo usimamizi na utunzaji wa barabara utaharakisha ukuaji wa uchumi wa wananchi.

Dkt Kone amesema sekta ya barabara inaigharimu Serikali fedha nyingi, hivyo ni lazima kuhakikisha kuwa thamani ya fedha zinazotolewa na Serikali au wafadhili zinalingana na uhalisia wa matumizi yaliokusudiwa.

Pia amewataka watendaji kuwashirikisha wananchi katika mipango, utekelezaji, usimamizi na tathmini za miradi ya barabara kwani wananchi hao wanaweze kuwa walinzi wa barabara hizo ili zidumu na zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.Wajumbe wa Bodi ya Barabara, wa kwanza ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Queen Mlozi, akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Yahaya Nawanda na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Manju Msambya wakifuatilia kikao hicho.
Wajumbe wa Bodi ya Barabara, wa kwanza ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Fatma Toufiq akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Edward Ole Lenga wakifuatilia kikao hicho. 
Pia amewataka watendaji kuwashirikisha wananchi katika mipango, utekelezaji, usimamizi na tathmini za miradi ya barabara kwani wananchi hao wanaweze kuwa walinzi wa barabara hizo ili zidumu na zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
Dkt. Kone amewashauri watendaji kuhakikisha fedha za ukarabati, ujenzi na ufuatiliaji wa miradi ya barabara zinawekewa vipaumbele kwa wakala wa barabara Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ili maeneo muhimu yaweze kuhudimiwa.

Ameongeza kuwa ni vizuri sasa kuandaa na kupanga maeneo zitakapopita  barabara za michepuko ili kuepuka tatizo la msongamano wa magari kwakuwa Mji wa Singida unakua kwa haraka na vyombo vya usafiri vinaongezeka.
Wajumbe wa Bodi ya Barabara wakifuatilia kikao hicho.
Kwa upande wao wajumbe wa bodi hiyo kutoka Wilaya mpya ya Mkalama wameilalamikia wilaya ya Iramba  kushindwa kusimamia miradi ya barabara ipasavyo iliyo sainiwa mapema kabla ya kuundwa kwa halmashauri hiyo.

Mkuu wa Wilaya hiyo Edward Ole Lenga amesema taarifa iliyoandaliwa na Wilaya ya Iramba haikuendana na hali halisi ya miradi ya barabara zilizopo wilayani humo, ambazo mikatabaka yake ilisainiwa na Wilaya ya Iramba.

Ole Lenga amesema maazimio ya kikao kilichopita cha bodi ya barabara kiliazimia kuunda tume ya kutathimini miardi ya barabara iliyosainiwa na Wilaya ya Iramba lakini badala yake azimio hilo halijatekelezwa.

Kutokana na hoja hiyo Dkt. Kone ameamuru uangaliwe uwezekano wa utaratibu wa kuvunja mikataba ya barabara za Wilaya ya Mkalama iliyosainiwa na Wilaya ya Iramba awali.


Wajumbe wa Bodi ya Barabara wakifuatilia kikao hicho.

No comments:

Post a Comment