Tuesday, February 27, 2024

RC SERUKAMBA AMKAMATA MFANYABIASHA AKIUZA SUKARI BEI KUBWA, AAGIZA AFUNGULIWE KESI

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, amemkamata mfanyabiashara wa duka la jumla Wilayani Manyoni kwa kosa la kuuza sukari kwa bei ya Sh. 189,000 kwa mfuko wenye ujazo wa kilo 50 ambapo ni kinyume na bei elekezi iliyowekwa na Serikali ambayo ni kati ya Sh.140,000 hadi 145,000 kwenye maduka ya jumla kwa mfuko wenye ujazo wa kilo 50 bei iliyoelekezwa na Bodi ya Sukari Tanzania.

Mfanyabiashara huyo aliyefahamika kwa jina la Mayengela Mboji amekamatwa Februari 27,2024 wakati msafara wa Mkuu wa Mkoa ukipita katikati ya mji wa Manyoni  na lilionekana gari lililosheheni sukari ndipo Serukamba akaamua kusimamisha msafara wa ziara yake na kuanza msako wa wenye gari lililosheheni sukari ambapo walipoulizwa washushaji mizigo walisema wamenunua kwa mfanyabiashara huyo aliyekamatwa.

Mara baada ya kuelezwa kwa ufupi mmilikiwa wa sukari hiyo ikamradhimu Mkuu wa Mkoa huyo aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Kemirembe Lwota pamoja na Mkuu wa Polisi wa Wilaya kwenda katika duka la mfanyabiashara na baada ya kukagua risiti za mauzo alibaini kuwa alikuwa akiwauzia wateja bei ya Sh.189,000 na wengine akiwauzia Sh.184,000 kwa mfuko wenye ujazo wa kilo 50.

Serukamba baada ya mahojiano na mfanyabiashara huyo aliomba asamehewe kwa madai kijana aliyemuacha dukani ndio ameuza sukari kwa bei kubwa bila maelekezo yake utetezi ambao hata hivyo ulipigwa na Mkuu wa Mkoa na kumwagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya kumkamata.

"OCD mkamate huyu mfanyabiashara na nataka huyu awe ndio mfano kwa mkoa huu afunguliwe kesi kwa kuuza sukari bei kubwa kinyume na bei elekezi iliyotolewa na Serikali," amesema.

MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA OPERESHENI YA DUKA KWA DUKA KUMTAFUTA MMILIKI WA SUKARI
Mfanyabiashara wa duka la jumla aliyefahamika kwa jina la Mayengela Mboji, lililopo Wilayani Manyoni akipelekwa rumande mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, (hayupo pichani) kuagiza kukamatwa kwa kuuza sukari bei kubwa ukilinganisha na bei elekezi ya Serikali.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, (kulia) akishuka kwenye gari mara baada ya kuona gari lililobeba shehena ya sukari likishuka kupeleka dukani katika mwa mji wa Manyoni wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa barabara wilayani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, (kushoto), pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Kemirembe Lwota wakiwa kwenye gari lililobeba shehena ya sukari likishusha mzigo  kupeleka dukani kwa mfanyabiashara aliyekamatwa Wilayani Manyoni.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, (wa kati kushoto), akiagiza kupatiwa risiti ya mashine kutoka kwa mfanyabiashara ili kujionea mauzo ya bei elekezi ya sukali wilayani Manyoni.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (katikati) akiwa katika Operesheni ya kubaini wanunuzi wa sukari kwa bei ya jumla wilayani Manyoni.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, (katikati) akikagua risiti kwa mnunuzi wa sukari (wa kushoto) wakati wa operesheni ya kusaka bei ya sukari wilayani Manyoni ambapo aligundua bei aliyouziwa ni Sh. 189,000 kwa mfuko wenye ujazo wa kilo 50 ambapo ni kinyume na bei elekezi ya Serikali. kulia ni mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe Thobias Mwanakatwe akifuatilia kwa ukaribu mahojiano hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akisisitiza jambo wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa barabara inayosimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini wilayani Manyoni. kushsoto ni Mkuu wa wilaya hiyo Kemirembe Lwota

No comments:

Post a Comment