Dendego, ametoa maagizo hayo (tarehe 16 Mei, 2024) katika ufunguzi wa Kongamano la Siku Mbili la Walimu kutoka mikoa ya Kanda ya kati na Kaskazini ambao wamekutana mjini Singida kujadili masuala mbalimbali yanayoikabili sekta hiyo ikiwemo namna bora ya kutetea maslahi yao na kuweka mipango na mikakati madhubuti ya kuongeza maradufu ufundishaji na ufaulu katika maeneo yao ya kazi.
Aidha, Mkuu huyo wa mkoa amesisitiza kuwa matatizo mengi yanayowakabili Walimu yanaweza kutatuliwa na Viongozi waliopo ngazi za Wilaya kwa kukaa pamoja na kujadili kwa kina namna bora ya kutafuta majawabu sahihi ambayo yataongeza ari ya Walimu kufundisha na kupandisha ufaulu kwa wanafunzi.
Amesema Serikali ya awamu ya Sita imefanya mambo makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Elimu hivyo ni muhimu kwa Walimu kote nchini kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na kwa ubunifu mkubwa ili kutengeneza Wanafunzi bora ambao watalisaidia Taifa kusonge mbele Kimaendeleo haraka.
Kuhusu maadili ya Wanafunzi, Mheshimiwa Halima Dendego, amewahimiza Walimu kuhakikisha wanawalea wanafunzi katika njia sahihi kwa kuzingatia mila na desturi za kitanzania ili kuwaepusha na matatizo ya utovu wa nidhamu.
Hata hivyo, Dendego, amewataka Walimu kutoa adhabu stahiki kwa wanafunzi wanaoenda kinyume na taratibu za shule kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizopo nchini ili kuhakikisha wanafunzi wanaomaliza shule au vyuo wanakuwa na maadili mazuri yanayompendeza Mwenyezi Mungu, Jamii na Taifa kwa ujumla.
Katibu Tawala wa mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa huo katika ufunguzi wa Kongamano la Siku Mbili la Walimu kutoka mikoa ya Kanda ya kati na Kaskazini lililofanyika mkoani Singida Mei 16, 2024.
Naye, Katibu Tawala wa mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga, amewataka Walimu kuzingatia kanuni na taratibu katika malezi ya wanafunzi ili kukabiliana na tatizo la mimba kwa wanafunzi jambo ambalo amesema halipendezi hata kidogo.
Dkt. Fatuma Mganga, amewahimiza Walimu kuongeza bidii na ubunifu katika ufundishaji ili kuhakikisha Taifa la Tanzania linapata Watalaamu wazuri na wabobezi ambao watasaidia nchi kusonga mbele kimaendeleo haraka.
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania -CWT- Leah Ulaya, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa huo katika ufunguzi wa Kongamano la Siku Mbili la Walimu kutoka mikoa ya Kanda ya kati na Kaskazini lililofanyika mkoani Singida Mei 16, 2024.
Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Walimu Tanzania -CWT- Leah Ulaya, ameiomba Serikali kuendelea kushughulikia matatizo yanayowakabili Walimu ikiwemo ulipaji wa madeni na upandishaji wa vyeo kwa wakati jambo ambalo amesema litasaidia Walimu kufanya kazi zao kwa ufanisi na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Rais huyo pia amewahakikishia Viongozi wa mkoa wa Singida na Taifa kwa ujumla kuwa wataendelea kufanya kazi kwa bidii kwa sababu wanaimani na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na mwanamama shupavu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, inafahamu kilio chao na itaendelea kutatua changamoto zinazowakabili kwa haraka.
No comments:
Post a Comment