Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego, akizungumza
kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania ambayo kimkoa
yamefanyika mjini Kiomboi wilayani Iramba amesema pamoja na Serikali Kuu kutoa
fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo lakini bado kuna umuhimu mkubwa
kwa wananchi kushirikiana na Serikali katika kujitolea nguvu kazi ili kuongeza
kasi katika ukamilishaji wa miradi hiyo.
Dendego, amesema maendeleo ya kweli hayawezi kuja kama watu
hawatashirikiana katika kufanya kazi hivyo ni muhimu kwa makundi yote
kushirikiana kwa kiwango cha juu ili kuharakisha maendeleo yao na ya Taifa kwa
ujumla.
Aidha, amewahakikishia wananchi wa mkoa huo kuwa yeye ni muumini
mzuri kwa watu wanaochapa kazi kwa bidii hivyo ni lazima wananchi wote kuchapa
kazi ili kujiletea maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla.
Katika maadhimisho hayo ya miaka 60 ya Muungano, Mkuu huyo wa mkoa ametoa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika uandishi wa isha pamoja na vikundi mbalimbali vya burudani zilizotumbuiza hususan kwa wimbo maalum wa Muungano.
No comments:
Post a Comment