Maadhimisho ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania yanafanyika hapa katika Wilaya ya Iramba na Kitaifa yanafanyika Dar es
Salaam yakiwa na Kauli Mbiu Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
“Tumeshikamana na Tumeimarika, kwa Maendeleo ya Taifa letu”.
Mkoa wa
Singida unaungana na Watanzania wote katika maadhimisho haya kuanzia tarehe 14 April, 2024 hadi leo tarehe 26
April 2024 ambapo katika kipindi hicho shughuli mbalimbali zilifanyika
katika Mkoa huo ikiwemo maombi na dua ya kuliombea Taifa, usafi katika maeneo
ya Umma, michezo, Sanaa, utamaduni na kupanda miti kwenye maeneo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment