Katibu Tawala mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga, amewasihi
wazazi mkoani humo kutimiza wajibu wao kila mmoja katika familia ili kuwa na
jamii bora kwa maendeleo bora ya taifa letu.
Kauli hiyo ameitoa leo (tarehe Mei 15, 2024) wakati wa Kongamano la
siku ya Familia Duniani lililofanyika kimkoa katika kata ya Ibaga wilayani
Mkalama na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa,
dini pamoja na wananchi.
“Kila mmoja atimize wajibu wake, tusaidiane, tushirikiane
tuweze kulea familia vizuri, lakini pia tusilee watoto wetu kama mayai,
tufuatilie mienendo ya watoto wetu, suala la kutengeneza familia bora si suala
la Serikali, ni suala la kila familia. Wazazi tutimize wajibu wetu tusiwachekee
watoto wetu” Dkt. Fatuma Mganga
Katibu Tawala huyo wa Mkoa amesema, Baba ni kichwa cha
familia hivyo wanalojukumu kubwa la kusimamia familia kikamilifu kwa kuchukua
nafasi zao katika familia ili kuiwezesha familia kuwa na bora nay a kuigwa
ndani ya jamii.
Awali akiwasilisha hoja kuhusu chanzo cha familia nyingi
kuvunjika, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali, amesema kukosekana kwa
uwazi baina ya wana ndoa kunapelekea ndoa nyingi kuwa na migogoro.
Ushirikishwaji katika familia ni muhimu kwakuwa panapokosekana
ushirikishwaji kunaleta migogoro ambayo inapelekea familia kutengana hivyo
amewasi wanafamilia kuwa na tabia na maadili mema sambamba kwa kufanya kazi kwa
bidii ili kujiongezea kipato na kumudu mahitaji ya familia.
“Kama ni kulima, Baba lima sana kama ni Mama fanya kazi za kuongeza kipato cha famili, kazi ya kutunza familia ni jukumu letu sote. DC Machali
No comments:
Post a Comment