Serikali ya
Mkoa wa Singida imewahakishia Wadau wa Maendeleo ikiwemo Uongozi wa Hospitali
ya Mtakatifu Gaspar ya Halmashauri ya Itigi Wilayani Manyoni kuwa itaendelea
kudumisha ushirikiano uliotukuka katika shughuli mbalimbali wanazofanya ikiwemo
utoaji wa huduma bora za msingi na za kibingwa za afya kwa wananchi wa mkoa
huo.
Mkuu wa mkoa
wa Singida Mheshiiwa Halima Dendego, ametoa kauli hiyo (tarehe 14/May/2024) wakati anazungumza katika maadhimisho ya Miaka
35 ya Hospitali ya Mtakatifu Gaspar Itigi.
Halima
Dendego, amesema amefurahishwa na kazi kubwa inayofanywa na Viongozi na
Watendaji wa Hospitali hiyo katika utoaji wa huduma za kiwango cha juu za afya ikiwemo
mama na mtoto pamoja na uboreshaji majengo na vifaa tiba.
“Baraka na mkono wa Mungu
uwe pamoja nasi na tuendelee kumwomba ili aendelee kutubariki zaidi ya hapa,
Mhe. Halima Dendego.
Mkuu wa mkoa
huyo amesema yeye na Watendaji wake wataendelea kutoa ushirikiano ili
kuhakikisha mashirika yenye nia njema ya kuwaletea maendeleo ya uhakika
wananchi wa mkoani Singida yanafikia malengo yao kwa kutoa huduma zao bila
usumbufu wowote.
Aidha amesisitiza
Viongozi wa Hospitali ya Matakatifu Gaspar Itigi kama wanachangamoto yoyote
ambayo inaweza kusababisha kudumaza au kuchelewesha utoaji wa huduma za afya
kwenye Hospitali hiyo wamweleze ili aweze kuzitafutia majawabu haraka
iwezekanavyo ili wananchi waendelee kupata huduma bora za kisasa za afya.
Naye, Mkurugenzi
wa Hospitali na Chuo cha Mtakatifu Gaspar Itigi Padre Justin Boniface, ameeleza
kuwa mafanikio waliyoyapata katika utoaji wa huduma za msingi na za kibingwa za
afya ni kwa sababu na ushirikiano mkubwa na karibu wanaoupata kutoka Serikalini.
Amesema
mkakati wao ni kuhakikisha kuwa Hospitali ya Mtakatifu Gaspar ambayo kwa sasa
inahudumia wagonjwa wengi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Singida na nje ya
mkoa huo inakuwa bora katika utoaji wa matibabu ya kisasa nchini ambapo kwa
sasa wameanza ujenzi wa kitengo cha kusafisha damu kwa sababu ya uhitaji mkubwa
wa wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Kemilembe Lwota, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment