Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba ameiomba Wizara ya Fedha kuweka kodi katika mafuta ya kula ya kutoka nje ya nchi ili soko la mafuta ya ndani liweze kuimarika
Maombi hayo ameyatoa leo mbele ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
CCM Daniel Chongolo wakati akiongea kwenye Mkutano wa Shina namba Tano
uliofanyika katika Kata ya Iguguno Wilayani Mkalama Mkoa wa Singida.
Serukamba amesema Mkoa umeongeza eneo la uzalishaji wa alizeti lakini soko la
alizeti aliendani na uzalishaji kwa kuwa mafuta yanayoingizwa kutoka nje
hayatozwi kodi jambo ambalo linawakatisha tamaa wakulima.
Aidha ameeleza kwamba mafuta yanayotoka nje hayatozwi kodi jambo
ambalo limesababisha bei ya alizeti kushuka na wakulima kukata tamaa ya
kuzalisha jambo ambalo linachangia viwanda vya mafuta kuzalisha chini ya
kiwango. Alisema
Hata hivyo ametolea mfano wa kiwanda cha usindikaji wa mafuta
ya alizeti cha Mount Meru kilichopo Mkoani hapo ambacho kinafanya kazi kwa
asilimia 25 tu kutokana na upatikanaji mdogo wa mbegu za alizeti.
"Tumepewa jukumu la kuongeza eneo la uzalishaji wa
alizeti jambo ambalo tumeshalitekeleza, changamoto yetu ni soko ambapo mafuta
kutoka nje hayana kodi hivyo kuathiri soko la mafuta ya alizeti" Serukamba
Amesema ekari zaidi ya laki sita zitazalishwa katika msimu
huu wa kilimo ambapo zaidi ya asilimia 44 za mafuta yatatoka Mkoani Singida
hivyo kuomba kulinda soko la ndani ili wakulima waweze kunufaika.
Akijibu maombi hayo Katibu Mkuu Chongolo amesema atalipeleka
kwa wahusika na anahakika litakuwa na majibu chanya kwa kuwa kazi ya chama
hicho ni kuhakikisha kilimo kinawanufaisha wananchi.
Amesema Serikali imetoa mbegu na mbolea ya ruzuku kwa
wakulima lengo likiwa ni kuwasaidia ki uchumi wananchi hivyo hatakuwa tayari
kuona fedha zinatumika bila kufikiwa kwa malengo.
Mwanzo mwa mwaka jana Serikali iliamua kuondoa kodi kwenye
mafuta ya kupikia kutoka nje ili kupunguza bei ya mafuta ambayo ilikuwa ipo juu
sana.
No comments:
Post a Comment