Wednesday, December 05, 2018

TIMU YA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA YA MKOA WA SINGIDA (RWST) YATEMBELEA MIRADI YA MAJI INAYOTEKELEZWA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA MKALAMA MKOANI SINGIDA

Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uratibu na Mipango Bw. Barthelome Temba ambaye ndiye Makamu Mwenyekiti wa Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Mkoa wa Singida akipanda ngazi kwaajili ya kukagua ujenzi wa Tanki 1 la ujazo wa lita wa 200,000 linalojengwa katika kijiji cha Nduguti Halmashauri ya Wilaya Mkalama Mkoani Singida.
Muonekano wa ndani wa Tanki moja la ujazo wa lita laki mbili ambao hadi sasa umekamilika kwa asilimia 70 na kufikia asilimia 16 ya uboreshaji wa mradi wa maji Nduguti katika halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida.



 Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mkoa wa Singida pamoja na Timu ya Wilaya Mkalama ya Maji na Usafi wa Mazingira wakipanda mlima kuelekea kwenye mradi wa ujenzi wa Tanki 1 la ujazo wa lita 200,000 za maji unaojengwa katika kijiji cha Nduguti Halmashauri ya Wilaya Mkalama mkoani Singida.

 Katibu wa Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mkoa wa Singida Mhandisi Emaeli Nkopi akishauri jambo wakati wa ukaguzi wa Mradi wa ujenzi wa Tanki 1 la ujazo wa lita laki mbili unaojengwa katika kijiji cha Nduguti Halmashauri ya Wilaya Mkalama mkoani Singida.



UJENZI WA MRADI WA MAJI KINYANGIRI  ⇩
 Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mkoa wa Singida pamoja na Timu ya Wilaya Mkalama ya Maji na Usafi wa Mazingira wakikagua utekelezaji wa Ujenzi wa Tanki moja lenye ujazo wa lita elfu tisini unaojengwa katika kijiji cha Kinyangiri Kata ya Kinyangiri Halmashauri ya Wilaya Mkalama mkoani Singida.
 Katibu wa Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Mkoa wa Singida Mhandisi Emaeli Nkopi akikagua Ujenzi wa Tanki moja lenye ujazo wa lita elfu tisini linalojengwa katika kijiji cha Kinyangiri Kata ya Kinyangiri Halmashauri ya Wilaya Mkalama Mkoani Singida.


 Makamu Mwenyekiti wa Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Mkoa wa Singida Bw. Barthelome Temba akishauri jambo katika Ujenzi wa Tanki moja lenye ujazo wa lita elfu tisini unaojengwa katika kijiji cha Kinyangiri Kata ya Kinyangiri Halmashauri ya Wilaya Mkalama mkoani Singida.





KIKAO CHA KUJADILI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI HALMASHAURI YA MKALAMA  ⇩



Katibu wa Timu ya Wilaya ya Maji na Usafi wa Mazingira Mhandisi. Antidius Muchunguzi akisoma taarifa ya hali ya Miradi ya Maji inayotekelezwa katika halmashauri ya Mkalama mkoani Singida.







 Katibu wa Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mkoa wa Singida Mhandisi Emaeli Nkopi akizungumza wakati wa kikao cha kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za Maji katika halmashauri ya Mkalama mkoani Singida.


  Kaimu Mkurugenzi Halmashauri na mwenyekiti wa kamati ya Maji na Usafi wa Mazingira halmashauri ya wilaya Mkalama Bw. Elias Mbwambo akizungumza wakati wa kikao cha kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za Maji katika halmashauri ya Mkalama mkoani Singida.


  Makamu Mwenyekiti wa Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mkoa wa Singida Bw. Barthelome Temba akifunga kikao cha kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za Maji katika halmashauri ya Mkalama mkoani Singida.


 PICHA YA PAMOJA

Kwasasa Halmashauri ya Wilaya Mkalama inaendelea kutekeleza Mradi wa Maji Nduguti, Mradi wa Maji Kinyangiri, Uboreshaji wa Mradi wa Maji Ipuli, Mradi wa Utafiti, Mradi wa Maji Nyahaa na uchimbaji na ufungaji wa Pampu za Maji katika visima ishirini.

Aidha, imeelezwa kuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kuharibika kwa miundombinu ya maji katika baadhi ya miradi, muamko duni wa jamii katika kusimamia, kuendesha na kuifanyia matengenezo miundombinu ya maji katika maeneo yao.

Hata hivyo, Timu ya Maji na Usafi wa Mazingira wilaya ya Mkalama imejipanga katika kuendelea kuchukua hatua za matengenezo pale uharibifu unapojitokeza pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya kumiliki, kuitunza na kuifanyia matengenezo miradi ya maji katika maeneo husika ndani ya halmashauri ya Mkalama.

Imetolewa na;
Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa 
SINGIDA

No comments:

Post a Comment