Tuesday, June 24, 2025

KAMATI YA MAADILI MKOANI SINGIDA IPO TAYARI KUWAHUDUMIA WANANCHI.


Posted on: June 24th, 2025

Jaji Mfawidhi Mhe.Dkt Juliana Masabo leo Juni 24,2025 ameapisha kamati ya maadili ya mahakimu ngazi ya Mkoa na Wilaya  tukio lililoshirikisha Wenyeviti,makatibu ,na wajumbe.

Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida huku Kamati zilizoapishwa ikiwa ni Wajumbe wa kamati ya Mkoa wa Singida,Wajumbe wa kamati ya Wilaya ya Singida,Iramba,Mkalama,Manyoni,Halmashauri ya Singida na Ikungi.

 Mhe.Dkt Masebo ametoa maagizo  kwa kamati hizo kuhakikisha wanakutana mara kwa mara ili kujengeana uwezo wa namna ya kushuhulikia kero za wananchi wanaoleta changamoto zao,kadhalika kuhakikisha vikao vinafanyika mara kwa mara kwa kuwaweka pamoja wajumbe wa Kamati ili kupeana miiko ya kamati yao na kuhakikisha wanakutana kila mwaka mara nne endapo kutakua hakuna malalamiko yeyote yanayowasilishwa.

Kadhalika ametoa wasilisho kwa wajumbe juu ya majukumu ya Kamati ya maadili ikiwemo namna kamati hizo zinafanya kazi katika namna ya uwasilishwaji na namna ya kushuhulikia malalamiko kwenye kamati ya Mkoa,upelelezi na utoaji wa  maoni.

Mhe.Moses Machali akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida,ameahidi kuwa Kamati hizo zitakwenda kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kuweza kushughulikia vema malalamiko yote yanayowasilishwa na wananchi.

Kamati hizi zinaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za mwaka 2023 zilizotengenezwa chini ya kifungu cha 66 cha Sheria ya Usimamizi wa Mahakama na zinahusika na uchunguzi wa tuhuma za ukiukwaji wa maadili dhidi ya Maafisa wa Mahakama.


No comments:

Post a Comment