Thursday, September 22, 2016

MRADI WA BARABARA YA MUHANGA - MUKAJENGA WENYE THAMANI YA MILIONI 700 WAZINDULIWA ITIGI.

Mkimbiza mwenge kitaifa Alex Christopher Kayuni akizindua mradi wa ujezi wa barabara ya  Muhanga - Mukajenga yenye kilomita 20 kwa kiwango cha changarawe yenye thamani ya milioni 757,000,000. Mradi huo utarahisisha usafirishaji wa mifugo na mazao nje na ndani ya halmashauri ya Itigi (mwenye mavazi meusi ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambe).

Mradi wa ujezi wa barabara ya  Muhanga - Mukajenga kwa kiwango cha changarawe yenye thamani ya milioni 757,000,000 uliozinduliwa na mwenge wa uhuru 2016 ukiwa katika halmashauri ya Itigi.


Mkimbiza mwenge kitaifa  Lucia Vitalis Kamafa akiukimbiza mwenge wa uhuru katika halmashauri ya Itigi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa vyumba vitatu na ofisi ya mwalimu katika shule ya Msingi Mji Mpya. Katika halmashauri hiyo miradi 11 yenye thamani ya shilingi Bilioni 1,328,488,000 ilizinduliwa, kutembelewa na kuwekewa mawe ya msingi.
Mkimbiza mwenge kitaifa Alex Christopher Kayuni akisaidiana na  Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambekuteketeza misokoto ya bangi katika kuonyesha jitihada za halmashauri ya Itigi ya kupambana na madawa ya kulevya.

Wajasiriamali wa asali wakionyesha bidhaa zao za asali wakati mwenge wa uhuru ulipotembelea halmashauri ya Itigi. Katika halmashauri hiyo miradi 11 yenye thamani ya shilingi Bilioni 1,328,488,000 ilizinduliwa, kutembelewa na kuwekewa mawe ya msingi.

Mkimbiza mwenge kitaifa Alex Christopher Kayuni akito ujumbe wa mwenge wa uhuru kwa wakazi wa Itigi (hawapo pichani) kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambe.

No comments:

Post a Comment