Thursday, September 22, 2016

WAKAZI ZAIDI YA MIA MBILI WA WILAYA YA IKUNGI WAJITOKEZA KUPIMA UKIMWI.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jumanne Mtaturu akisoma taarifa ya miradi inayotembelewa na mwenge wa uhuru katika halmashauri yake.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jumanne Mtaturu akinyakua na watumishi wa halmshauri Ikungi katika mapokezi ya mwenge wa uhuru katika halmashauri yake.Mwenge wa uhuru ukiwa katika halmashauri ya Ikungi.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru 2016 George Jackon Mbijima akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Ikungi (hawapo pichani) na kutoa ujumbe mwenge mara baada ya kutembelea miradi ya maendeleo.

Wakazi 283 wa Wilaya ya Ikungi wamejitokeza kupima virusi vya Ukimwi (VVU) katika mkesha wa Mwenge wa uhuru ambapo kati yao hao wakazi wanne wamebainika kuwa wameambukizwa virusi hivyo.

Akisoma taarifa ya mbio za mwenge wa uhuru wakati wa kuhitimisha mbio Wilayani hapo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu amesema mwitikio huo ni mkubwa na unaonyesha namna ambavyo wakazi hao wamepata elimu juu ya Ukimwi.

Mtaturu amesema ujumbe wa mwenge wa mwaka huu kwenye mapambano dhidi ya UKIMWI zinasema Tanzania bila maambukizi mapya chini ya kauli mbiu ya "Unyanyapaa na vifo vitokanavyo na Ukimwi inawezekana" imekuwa imewahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao ili kurahisishia serikali kujua hali halisi ya maambukizi.

Ameongeza kuwa watanzania wanaweza kuepuka vifo visivyo kuwa vya lazima kwa kupima na kuzifahamu afya zao hivyo kuwa rahisi kwa wao kupatiwa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi jambo ambalo litawafanya kuishi muda mrefu kuliko kuishi na Virusi vya Ukimwi kwa kificho kwani ni hatari kwa maisha yao.

Katika mapambano dhidi ya Maralia Mtaturu amesema ugonjwa huo ni miongoni mwa magonjwa yanayowasumbua watu wengi katika Wilaya hiyo ambapo mwaka 2015/2016 jumla ya wagonjwa 35,408 waliugua Malaria, kati yao watoto wenye umri chini ya miaka mitano ni 15,788 na wenye umri zaidi ya miaka mitano ni 19,620 huku watoto wenye umri chini ya miaka mitano wakiwa sita na watu wazima wawili.

Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndugu George Jackson Mbijima amewashukuru wananchi kwa umoja wao kwa kujitokeza kwa wingi kwenye shughuli za Kukimbiza Mwenge huo kwani wameonyesha imani kubwa tena kwa vitendo na serikali ya awamu ya tano yenye kauli mbiu ya hapa kazi tu.

Mbijima amesema wananchi wamejitokeza kwa wingi na kupima afya zao jambo licha ya dhana potofu kuwa kujitokeza kupima ni kujiaibisha ama kurahisisha vifo kutokana na mawazo mara baada ya kutambua afya yako hasa ukigundulika kuwa umeambukizwa ni kujirahisishia kifo.

Ukiwa Wilayani Ikungi Mwenge wa Uhuru umetoa hamasa na ari kwa vijana na wananchi juu ya uzalendo, ukakamavu na umoja pia umetembea umbali wa Kilomita 141.5 na kutembelea miradi 9 yenye jumla ya Shulingi Milioni 975,991,180.

No comments:

Post a Comment