Miradi ya maendeleo 15
yenye thamani ya shilingi bilioni 8,391,131,054 imetembelewa na mwenge wa uhuru
katika halmashauri za manispaa na singida wilayani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya
Singida Elias Tarimo amesema miradi hiyo imejikita katika sekta za afya, maji,
elimu, barabara, kilimo, ufugaji, miradi ya akina mama na vijana pamoja na
vilabu vya wapinga rushwa na madawa ya kulevya.
Tarimo amesema katika
halmashauri ya manispaa miradi iliyowekewa mawe ya msingi ni pamoja na stendi
mpya ya mabasi yaendayo mikoani ambapo mradi huo una thamani ya shilingi
bilioni 3,726,072,678 na mradi wa barabara ya kiwango cha lami wenye thamani ya
bilioni 2,694,339,096.
Aidha katika upande
wa kuwajengea uwezo vijana kiuchumi manispaa imeendelea kutenga asilimia kumi
ya bajeti ya mwaka ili kuwawezesha vijana mafunzo ya namna ya kubuni miradi na
kuiendeleza.
Katika mapambano
dhidi ya Ukimwi Tarimo amesema manispaa imeweza kuanzisha vituo kumi vya kupima
Ukimwi na kutoa ushauri nasaha, vituo 26 vya kuzuia maambukizi kutoka kwa mama
kwenda kwa motto na vine vya kutoa dawa za kufubaza VVU.
Amesema kwa kipindi
cha Januari 2015 mpaka septemba 2016 wakazi wa manispaa 19,591 wamepima VVU
ambapo waliopatikana na maambukizi ya VVU ni 1,124.
Kwa upande wa ugonjwa
wa maralia ambapo kauli mbiu yake ni “wekeza katika maisha ya baadaye tokomeza
maralia” manispaa imefanikiwa kupunguza maambukizi na vifo vitokanavyo na
ugonjwa huo kutoka asilimia kumi mwaka 2014 hadi asilimia 3.7 mwaka 2015
kutokana na juhudi za manispaa za kutoa elimu ya kuteketeza mazalia ya mbu na
matumizi ya vyandarua vilivyowekewa da ya viuatilifu.
Tarimo amefafanua
kuwa wananchi wanaelimishwa na kushauriwa kuwahi hospitali pindi wanapoona
dalili za homa na si kujinywea dawa bila maelekezo ya wataalamukwani si kila
homa ni malaria na endapo watagundulika kuwa na ugonjwa wa malaria wanashauriwa
kutumia dawa mseto na kukamilisha dozi.
Kwa upande wa
halmashauri ya singida, mwenge wa uhuru umezindua na kuweka mawe ya msingi katika
miradi minane yenye thamani ya milioni 989,039,279 ambapo nguvu ya wananchi ni
shilingi milioni 84,186,600, halmashauri ya wilaya ni milioni 21,607,450, wahisani ni 76,742,000 na serikali kuu 806,503,229 pamoja na kuhamasisha wananchi juu ya umoja,
mshikamano na uzalendo.
Miradi hiyo ni pamoja
na mradi wa maji wa kijiji cha Itaja wenye thamani ya shilingi milioni 411,405,887
uliokamilika mwezi Mei pamoja na miundombinu ya nyumba ya mashine, ufungaji wa
jenereta na pamu za kusukumia maji, ujenzi wa njia kuu ya kupeleka maji kwenye
matanki na ujenzi wa mtandao wa kusambaza maji kwenye vituo vya kuchotea maji.
Mradi huo utakaonufaisha
wakazi wa Itaja kwa kuwapatia maji safi na salama umekabidhiwa kwa jumuiya ya
watumia maji iliyopewa mafunzo ya uendeshaji na iko chini ya uangalizi kwa
kipindi cha miezi sita.
Naye Kiongozi
wa mbio za mwenge wa uhuru George Jackson Mbijima ameweka jiwe la msingi ujenzi
wa kiwanda cha kusindika mbogamboga kijiji cha msange na kuwashauri wanakikundi
kuendeleza usindikaji wa mazao hayo kwani ni changamoto kwa wakulima kutokana
na kuharibika haraka.
Amesema mradi
ukisimamiwa utakuwa mkombozi wa wakulima kutokana na kuwa wakulima wengi
hulalamika kuharibika mazao kutokana na kukosa masoko haraka hasa kwa mazoa ya
mbogamboga, aidha mradi utatengeneza ajira kwa vijana na akina mama wengi wa
kijiji cha msange na halmashauri ya Singida.
Ameongeza kwa
kusisitiza kuwa mradi utaboresha afya ya wanajamii wanaouzunguka na kuwashukuru
wahisani waliotoa shilingi milioni 47,000,000, huku halmashauri ikichangia
milioni 2,000,000 na wananchi milioni 4,046,000 katika kufanikisha ujenzi wa
kiwanda hicho.
No comments:
Post a Comment