Saturday, September 24, 2016

MKALAMA ILIVYOUPOKEA MWENGE WA UHURU 2016

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama (kushoto) Mhe: Injinia Jackson J. Masaka akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Singida mheshimiwa Elias Tarimo.
PICHA 13: viongozi, watumishi, vikundi vya ngoma za asili na wananchi wakipata burudani muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Mwenge wa Uhuru katika eneo la Iguguno uwanjani.





















Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Mkalama, Heke Bulugu (kushoto) akitoa maelekezo juu ya namna mitambo ya kusukuma maji inavyofanya kazi mbele ya kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa ndugu George Jackson Mbijima na viongozi wengine.

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, ndugu George Jackson Mbijima (kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mhe: Injinia Jackson J. Masaka mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji.

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Ndugu George Jackson Mbijima akiweka jiwe la Msingi la ujenzi wa daraja katika kijiji cha Kinampundu huku akishuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mhe: Injinia Jackson J. Masaka.

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa ndugu George Jackson Mbijima (kushoto) akikabidhi cheti cha usajili wa saccos ya vijana ijulikanayo kama Vijana Saccoss katika kijiji cha Ilunda.

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa ndugu George Jackson Mbijima akifungua ofisi ya saccoss ya vijana  ijulikanayo kama Vijana Saccoss katika kijiji cha Ilunda.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Dokta Deogratius Basini akisoma taarifa fupi ya namna ujenzi wa Zahanati ya Kidarafa  ulivyotekelezwa.

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa ndugu George Jackson Mbijima akifungua kiwanda cha kusindika mazao ya Mbogamboga kilichopo katika kijiji cha Gumanga.

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa ndugu George Jackson Mbijima (katikati) akipokea maelekezo juu ya namna kiwanda cha kusindika mazao ya mbogamboga kitakavyokuwa kikifanya kazi kutoka kwa Afisa kilimo wa Wilaya ya Mkalama Cuthbert Mwinuka (kushoto).


Wilaya ya Mkalama jana ilikabidhi rasmi Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Iramba baada ya kuupokea siku ya ijumaa kutoka Wilaya ya Singida.

Mbio za Mwenge Wilayani Mkalama mwaka huu zilijumuisha uzinduzi na ufunguzi wa miradi mitano ukiwemo ule wa Maji katika kijiji cha  Iguguno, Uwekaji jiwe la Msingi la ujenzi wa daraja lililopo kijiji cha Kinampundu, Zahanati iliyopo katika kijiji cha Kidarafa, Saccos ya Vijana katika kijiji cha Ilunda  na mradi wa kiwanda cha kusindika mboga za majani uliopo katika kijiji cha Gumanga.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Saccos ya Vijana kijiji cha Ilunda inayojulikana kwa jina la ‘Vijana Saccoss’  kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa ndugu George Jackson Mbijima aliwasisitiza viongozi wa Halmashauri Wilayani hapa kuwapa kipaumbele vijana na kuwashirikisha katika maamuzi yanayowahusu ili kuwafanya washiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa.

“ Hata hivi vikundi vya vijana mnavyoviunda, hakikisheni nafasi zote za uongozi zinashikwa na vijana na wale ambao wamevuka ngazi ya ujana wabaki kama washauri tu”  alisema Mbijima

Mbijima alizitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatoa asilimia tano kutoka kwenye mapato yao  na kuwapa vijana kama ambavyo muongozo unawataka wafanye.
Akizungumza katika eneo la Mkesha wa Mwenge mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi na ufunguzi wa miradi, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mheshimiwa Injinia Jackson J. Masaka aliwashukuru waanchi wote Wilayani hapa kwa ushirikano waliouonesha kuanzia muda  wa Mapokezi mpaka Mwenge ulipomaliza mbio zake.

“ Nimefarijika sana na mwitikio uliooneshwa na Viongozi na wananchi wa Wilaya ya Mkalama kwa ujumla, nina uhakika kuanzia sasa tutazitumia vizuri baraka zote zilizoletwa na Mwenge wetu wa Uhuru”. Alihitimisha Masaka.

Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2016 katika Wilaya ya Mkalama zilipita kwenye miradi mitano yenye thamani ya fedha za Kitanzania shilingi  1,161048,776,92 ambapo  shilingi 14,500,000.00 zilichangwa na wananchi, shilingi 31,000,000.00  imetolewa na Halmashauri ya Wilaya, shilingi 216,444,873.92 zimetolewa na Serikali kuu huku wahisani wakitoa shilingi 899,103,903.00.


No comments:

Post a Comment