Monday, September 26, 2016

SINGIDA YAKABIDHI MWENGE WA UHURU MKOA WA TABORA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe akimkabidhi mwenge wa uhuru Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri, ukiwa unawaka na una meremeta pamoja na wakimbiza mwenge kitaifa sita.


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri akiupokea mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe ukiwa unawaka na una meremeta pamoja na wakimbiza mwenge kitaifa sita.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J Mtigumwe akiagana na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2016 George Jackson Mbijima akiwa mzima wa afya kuendelea na mbio za mwenge wa uhuru Mkoa wa Tabora.

Askari polisi wa Mkoa wa Tabora na wale wa Mkoa wa Singida wakishangilia mwenge wa uhuru katika eneo la kijiji cha Mgongolo kata ya Igunga Mkoa wa Tabora.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J Mtigumwe akisoma taarifa ya mbio za mwenge wa uhuru Mkoa 14.2 kushoto kwake ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2016 George Jackson Mbijima.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J Mtigumwe akisoma taarifa ya mbio za mwenge wa uhuru Mkoa 14.2 kushoto kwake ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2016 George Jackson Mbijima na wa kwanza kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dokta Angelina M. Lutambi.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J Mtigumwe akiagana na mkimbiza mwenge kitaihfa Lucia Vitalis kutoka Manyara kabla hajakabidhiwa Mkoa wa Tabora.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J Mtigumwe akifurahi na wakuu wa wilaya za Mkoa wa Singida mara baada ya kuukabidhi mwenge wa uhuru Mkoa wa Tabora.

No comments:

Post a Comment