Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe akipampu maji katika kisima cha maji cha Kijiji cha Sukamahela kilichokarabatiwa na taasisi ya peace corps pamoja na wanakijiji wa Sukamahela, usambazaji wa maji kutoka katika kisima kwenda kijijini unafanywa na shirika la Wolrd Vision.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Goefrey Mwambe naye akipampu maji
katika kisima cha maji cha Kijiji cha Sukamahela kilichokarabatiwa na
taasisi ya peace corps pamoja na wanakijiji wa Sukamahela, usambazaji wa
maji kutoka katika kisima kwenda kijijini unafanywa na shirika la Wolrd Vision.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa Kijiji cha Sukamahela, kisima hicho kimekarabatiwa na
taasisi ya peace corps pamoja na wanakijiji wa Sukamahela, usambazaji wa
maji kutoka katika kisima kwenda kijijini unafanywa na shirika la Wolrd Vision.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe akipanda mti katika chanzo cha maji cha kijiji cha Saranda ili kutunza mazingira ambapo ukarabati na usambazaji wa maji kutoka katika chanzo hicho kwenda kijiji cha Saranda unafanywa na shirika la Wolrd Vision.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe akizungumza na wakazi wa kijiji cha Sukamahela na kuwasisitiza kutunza mazingira na kuachana na biashara ya mkaa kwani huharibu mazingira kwa kukata miti kwa wingi.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambe akipokea maelekezo ya kusimamia wananchi wake kutofanya biashara ya Mkaa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe wakati wa kikao na wakazi wa kijiji cha Sukamahela, kushoto kwakwe ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Manyoni na anayefuata ni Meneja wa Wolrd Vision kanda ya kati Faraja Kulanga.
Meneja wa Wolrd Vision kanda ya kati Faraja Kulanga akisisitiza azma ya shirika hilo kuendelea kushirikiana na serikali katika kuboresha miradi ya maendeleo mkoani Singida.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amepiga marufuku biashara ya mkaa wilayani
Manyoni kutokana na ukataji miti hovyo unaoharibu vyanzo vya maji na
kumwelekeza Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambe kusimamia utekelezaji wa
agizo hilo.
Mhandisi Mtigumwe
ametoa agizo hilo katika vijiji vya Sukamahela na Saranda wilayani Manyoni wakati
akizindua miradi miwili ya maji ambapo shirika la wolrd vision litatoa milioni
355 shirika la peace coarps limetoa shilingi milioni sita na wananchi wakichangia
milioni mbili.
Amesema kumekuwa na
tabia ya ukataji miti hovyo kwa ajili ya biashara ya mkaa hasa kwa halmashauri
hiyo na kuwataka wananchi kuangalia ujasirimali mwingine huku wakiruhusiwa
kukata mkaa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani tu.
Mhandisi Mtigumwe
ameongeza kuwa kamati za miradi hiyo ya maji zinapaswa kusimamia moiradi hiyo
na kutoa elimu ya uitunzaji wa mazingira kwa jamii inayozunguka miradi hiyo ili
iweze kuwa endelevu.
Amesema kamati hizo
zipange bei ya kuuzia maji itakayokuwa rafiki kwa wana jamii wote ili miradi
hiyo iwanufaishe wananchi hao na kupata pesa ya kuendeshea jenerator na utunzaji
wa miundombinu kwa pesa itakayokusanywa.
Mhandisi Mtigumwe
amemshauri Mkuu wa Wilaya hiyo kusimamia mapato na matumizi ya pesa za miradi
hiyo ya maji kutokana na kamati nyingine kufuja pesa za miradi ya maji kasha kuitelekeza
bila ya kuiendeleza.
Meneja wa kanda ya
kati wa shirika la World Vision Faraja Kulanga amesema tayari shirika hilo
limeshatenga shilingi milioni 150 zitakazo tolewa kuanzia mwezi oktoba kwa ajili
ya kutengeneza mifumo na maeneo ya kuchotea maji katika vijiji vya sukamahela
na Saranda.
Kulanga amesema
shirika hilo limeshakarabati mradi wa maji wa Saranda ambao tayari unatumika
huku shirika likiendelea kukarabati miundombinu ya miradi hiyo na kuzisisitiza
kamati za maji kumiliki na kuitunza miradi hiyo kwani wafadhili huondoka.
Naye mwenyekiti wa
kamati ya maji kijiji cha Saranda Julius Kundule amesema kamati hiyo tayari ina
shilingi milioni mbili kwenye akaunti huku wakiahidi kuitunza miradi hiyo.
Kundule ameongeza
kuwa kamati hiyo itajitahidi kutunza miradi hiyo na kutoa elimu kwa wananchi
juu ya uchangiaji wa maji ili kupata pesa kwa ajili ya ukarabati na utunzaji wa
miundombinu kwakuwa wengi hudhani maji ni bure.
Wakazi wa vijiji vya
Sukamahela na Saranda wameyashukuru mashirika ya world vision na peace corps
kwa kukarabati miradi hiyo na kusogeza huduma ya maji karibu na makazi yao.
Wameongeza kuwa
uboreshaji wa huduma hiyo ya maji utasaidia kupunguza muda wa kutafuta maji na hivyo
kupata muda wa kutosha wa kujishughulisha na miradi ya maendeleo badala ya
kutafuta maji.
No comments:
Post a Comment