Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amewataka Watumishi wa Mkoa huo kufanya kazi kwa bidii ili kupatikana tija itakayo saidia kuongeza mapato ambayo yataboresha maslahi ya Watumishi.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa Baraza jipya la Wafanyakazi
lililofanyika Machi 9, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo ambapo
alisistiza uwepo wa mahusiano mazuri baina ya watumishi ili kuongeza tija.
"Pia nipende kusisitizia kuwa bila tija Serikali haiwezi
kupata mapato ambayo yataiwezesha kuboresha maslahi ya watumishi" alisema
Serukamba
Aidha ameagiza Baraza hilo
kutekeleza majukumu yake kuhusu taratibu zinazoweza kuchukuliwa ili
kuleta ufanisi katika mifumo ya kutoa huduma kwa wananchi na kushauri mabadiliko
ya kanuni za kudumu katika utumishi wa umma namna bora ya kuboresha mazingira. Serukama
aliagiza wajumbe wa Baraza hilo kuhakikisha wanapitia rasimu ya bajeti kwa
undani na kushauri kama kuna maeneo hayo yalisahaulika kabla havijafikishwa
bungeni.
Hata hivyo RC Serukamba ameagiza Halmashauri zote Mkoani hapo
ambazo mabaraza yake ya wafanyakazi yalimaliza muda wake kuhakikisha wanachagua
mengine ili yaweze kuendelea kutetea maslahi ya watumishi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni
Katibu Tawala Mkoa Mwl. Dorothy Mwaluko amewaasa watumishi kutumia weledi
katika kutekeleza majukumu ili kuleta tija iliyo kusudiwa huku akikumbusha
kufuata mila na desturi za utumishi ili kufikia malengo.
"Utumishi una mila na desturi zake na mtumishi atapata
tabu endapo atashindwa kuzifuata, tuishi maisha ya utumishi wa umma" Mwaluko
Aidha amehimiza watumishi kuwa wavumilivu na upendo katika
kufanya kazi huku akibainisha kwamba hakuna mwenyekazi zake binafsi katika Mkoa
hivyo watumishi wajifunze kushirikiana katika kutumia rasilimali zilizopo
zikiwemo magari.
No comments:
Post a Comment