Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Singida zimekamilika leo na Kukabidhiwa Mkoa wa Dodoma, Wilaya ya Chemba katika kijiji cha Kinyamshindo.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan ameukabidhi mwenge wa uhuru kwa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan akimkabidhi mwenge wa uhuru Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge.
Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2014 Ndugu Rachel Stephen Kassanda ameushukuru Uongozi wa Mkoa wa Singida kwa ushirikiano wa kipekee waliouonyesha.
Kassanda amewataka wananchi wa Mkoa wa Singida kulinda na kuthamini miradi ya maendeleo iliyozinduliwa, kufunguliwa na kutembelewa na Mwenge.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2014 Ndugu Rachel Stephen Kassanda akimshukuru Katibu Tawala Mkoa wa Singida kwa ushirikiano wa kipekee
Pia amewasihi wananchi wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi utakapowadia wakati wa kupiga kura ya maoni ili kupata katiba mpya ya nchi yetu.
Kassanda amesisitiza suala la amani kuwa ni msingi wa maendeleo ya taifa letu hivyo wananchi wanapaswa kuhakikisha wanaitunza amani ya nchi yetu huku wakidumisha ushirikiano na umoja.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge wakipongezana baada ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru.
No comments:
Post a Comment