Thursday, March 02, 2023

Chongolo, aagiza vifungashio vya mbolea kufungwa kulingana na mahitaji Wakulima

Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Daniel Chongolo, amemuagiza Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Iramba Magharibi Dkt. Mwigulu Nchemba kuhakikisha vinakuwepo vifungashio vya mbolea kuanzia kilo mbili ili kuwarahisishia wakulima kununua mbolea hizo kulingana na mahitaji yao.

Maagizo hayo ameyatoa leo wakati akiongea na Wananchi wa Kata ya Ulemo Wilaya ya Iramba Mkoani Singida baada ya kupata malalamiko ya wananchi kuhusu bei ya mbolea na namna ya ufungashaji.

Amesema wapo wakulima wadogo, wakati na wakubwa ambao wana uwezo na mahitaji ya viwango tofauti vya mbolea kulingana na ukubwa wa mashamba waliyonayo.

"Tunashindwaje kuwa na vifungashio vya kuanzia kilo moja hadi mbili ili mkulima mwenye bustani au robo ekari kununua kiasi anachotaka kuliko kuwa na kifungashio cha kilo 50 pekee ambacho sio kila mkulima anaweza kukinunua" alisema Chongolo.

Aidha amewataka wakulima kutokuwa na haraka ya kuuza mazao yao kwa walanguzi ili kusubiri bei nzuri huku akiwasihi kuhifadhi mazao ya sehemu salama.


 

No comments:

Post a Comment