Kauli hiyo imetolewa leo Novemba 30, 2021 na Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya wilaya hiyo Michael Matomora
alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo wakati wa ziara
ya Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba
vya madarasa katika shule ya Sekondari Kyengege Kata ya Kyengege.
Aidha amebainisha kwamba miradi yote imefikia hatua ya
kupauliwa na tayari wasafirishaji wapo Dar es Salaam kuchukua mabati ambapo
tunatarajia ndani ya siku mbili au tatu yatakuwa yamefika katika maeneo ya
kazi, hivyo ni imani yetu kwamba mpaka tarehe tano tutakuwa tumemaliza kupaua
kwa sababu tumesha nunua kila kitu, Alisema Matomora.
Mkurungezi huyo akabainisha kwamba katika miradi hiyo 47 ni
ya ujenzi wa madarasa katika Shule za Sekondari 19 ambazo zitagharimu kiasi cha
sh.Milioni 940
Aidha Mkurugenzi huyo akaeleza kwamba miradi 14 ni kwa
ajili ya ujenzi wa madarasa 14 katika shule shikizi saba (7) ambazo ni Ulongo, Magugu, Kagera, Itunda,
Masunkune, Kisingu na Ibambasi ambazo zitagharimu kiasi cha Tsh. Milioni 280.
Amesema kwa ujumla Shule
ambazo zinatekeleza miradi ya UVIKO 19 katika wilaya ya Iramba ni Lulumba, New
Kiomboi, Kinambeu, Shelui, Kyengege, Kizaga, Kidaru, Mbelekese na Mtekente.
Nyingine ni Mtoa, Tulya, Ntwike, Urughu, Ushora, Kinampanda, Mukulu, Mgongo, Kaselya
na Kisiriri. alifafanua
Matomora.
Akijibu baadhi ya changamoto zilizojitokeza kwenye
utekelezaji wa miradi hiyo ikiwemo baadhi ya wakuu wa Shule kutotizimiza majukumu
yao vizuri Mkuu wa Mkoa Dkt. Mahenge amesema Serikali haitamvumilia mtumishi
yeyote wa Serikali atakaye sababisha uzembe katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Yeyote atakayefanya uzembe wa makusudi tutamchukulia hatua za
kinidhamu ili iwe fundisho kwakwe na wengine wenye tabia kama hizo, lengo
likiwa sio kumkomoa bali ni kwa ajili ya manufaa ya jamii husika. Alisema Dkt.
Mahenge.
Hata hivo RC Mahenge amewapongeza viongozi
wa wilaya ya Iramba kwa jitihada zao katika kukamilisha ujenzi wa
madarasa hayo ambapo mpaka sasa madarasa yote yamefikia hatua ya kupaliwa.
Aidha RC. Mahenge akawataka viongozi wa Halmashauri ya wilaya
ya Iramba pamoja na viongozi wa CCM kuendelea kusimamia kazi hizo na
kuhakikisha kwamba inakamilika kabla au ndani ya Desemba 5, 2021.
Awali Suleiman Mwenda akimkaribisha Mkuu wa mkoa alisema wilaya inatekeleza miradi 47 ya ujenzi wa madarasa katika shule 19 ambapo jumla ya madarasa 18 yamefikia hatua kupauliwa katika shule saba (7)
No comments:
Post a Comment