Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge Leo Novemba 30,
2021 amezindua Rasmi na kukabidhi basi aina
ya Coasta kwa ajili ya kusafirishia wafanyakazi wa Hospitali ya Mandewa iliyopo
mkoani hapo kama kitendea kazi kitakachowasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji
kazi.
Akongea na wafanyakazi akiwa Hospitalini hapo baada ya kuwakabidhi
basi Mkuu wa Mkoa amewapongeza watumishi kwa namna ambavyo wamekuwa wakifanya
kazi katika mazingira magumu na wengi
wao wakitumia bodaboda kufika kazini lakini pia hawakukata tamaa.
RC Mahenge amemtaka Afisa usafirishaji wa Hospitali ya mkoa
wa Singida kuhakikisha kwamba basi hilo linatunzwa na kuzingatia muda wa kufanyia huduma (service) kila inapofika muda
wake ili kulifanya lidumu kwa muda mrefu na kuendelea kuwasaidia watumishi.
Amewataka madaktari katika hospitahi hiyo ambayo ni Tawi la
Hospitali ya Mkoa wa Singida kuboresha
huduma zao na kuzifanya ziwe za kibingwa
ili kuifanya Singida kuwa kimbilio la
mikoa ya jirani (center of excellence )
Aidha ameitaka bodi ya Hospitali hiyo kuanza kufikiria namna
ya kujenga nyumba za watumishi kupitia vyanzo vyao vya ndani au kupitia mashirika mbalimbali kwa kuwa kukaa karibu na hospitali kunaongeza
ufanisi katika kazi.
Akimalizia hotuba yake mkuu wa mkoa amewataka madaktari hao
pamoja na bodi kuyafanya majengo ya zamani kuwa hospitali ya Wilaya halafu
majengo ya Hospitali ya Mandewa yatumike kama hospitali ya mkoa.
Awali Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa Dkt. Deogratius Banuba akisoma hotuba yake
amesema gari hilo lina thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 236 ambazo zilitokana na
makusanyo ya ndani.
Hata hivyo amemhakikishi RC kwamba gari hilo litatumika kubeba watumishi kuwaleta kazini na kuwarudisha na pia kutumika katika shughuli za kijamii kwa watumishi hasa zile ambazo zipo ki sharia kama Msiba.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA WAKATI WA HAFLA FUPI YA UZINDUZI WA BASI
No comments:
Post a Comment