Wavamizi wa msitu wa Hifadhi ya Mgori uliyopo mpakani mwa wilaya ya Singida Vijijini na Mkoa wa Manyara wametakiwa kusitisha shughuli wanazoziendeleza ndani ya msitu huo na kuondoka Mara moja katika eneo hilo kwa kuwa eneo hilo ni la uhifadhi .
Kauli hiyo imetolewa leo
na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge wakati wa majumuisho ya ziara
yake kwenye msitu wa Hifadhi hiyo ambayo alijionea uharibifu mkubwa iliyokuwa
unaendelea ikiwa ni pamoja na ukataji wa miti uchimbaji wa mkaa na uanzishwaji
wa makazi ndani ya Hifadhi.
Katika ziara hiyo
iliyokuwa na lengo la kutembelea na kujionea hali ya uharibifu katika hifadhi hiyo na kukuta maboma kadhaa yamejengwa na yanaishi watu
na ukataji wa miti pamoja na uchomaji wa mkaa.
Akiwa katika hifadhi hiyo mkuu wa Mkoa ameshangazwa na kitendo cha wavamizi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Manyara kuhamia msitu na kudai kwamba wameuziwa na wakazi wa maeneo hayo huku wengine wakidai wameruhusiwa na Serikali.
Kutokana na mkanganyiko
huo Mkuu wa Mkoa akawataka kuondoka maeneo hayo ndani ya Siku tatu huku
akiitaka kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Singida na viongozi wengine kuandaa mkakati wa kuwaelimisha wananchi wa eneo hilo kuhusu athari ya uharibifu wa
msitu huo.
Aidha Mkuu wa mkoa amebainisha kwamba Serikali ilikuwa na Nia nzuri kuwaambia Wananchi kuyatumia bàadhi ya maeneo lakini hawakutakiwa kutumia maeneo ya Hifadhi ya msitu.
Dkt. Mahenge akawataka Wakala wa Uhifadhi ya misitu Nchini (TFS) kuandaa mikakati ya haraka ya kunusuru msitu huo.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
No comments:
Post a Comment