Wednesday, November 17, 2021

Wito watolewa kwa wakazi wa Singida kuendelea kupata chanjo ya UVIKO 19.

 

Wakazi wa Mkoa wa Singida wametakiwa kujitokeza kwa wingi na kupata chanjo ya Uviko 19 ambazo zinatolewa na wataalamu wa afya katika vituo mbalimbali  ili kuwa na mtaji wa kiafya utakaosaidia kuongeza uzalishaji na kuimarisha uchumi wao.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge  alipokuwa akifungua kikao cha kamati ya Afya ya msingi  Mkoa (PHC) kilichofanyika leo katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Dkt. Binilith Mahenge amesema kwamba ili kuleta maendeleo makubwa katika Mkoa wa Singida ni muhimu kulinda afya za watu na kuwaepusha maradhi  ili waweze kuwa na nguvu za kuzalisha.

Aidha Mkuu wa mkoa amewataka wataalamu wa afya kuendelea kuwafuata wananchi majumbani na kutoa chanjo kwa hiari kwa kuwa imeonekana kusaidia wananchi ambao kwa sababu moja au nyingine wanashindwa kufika vituo vya kutolea huduma ya chanjo.

Hata hivyo ametoa wito kwa wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu juu uchanjaji iendelee kutolewa kwa wananchi ili kuhamasika na uchanjaji  ambapo kwa sasa hakuna dawa ambayo imeshapatikana ya kutibu uviko 19.

Amewataka wananchi kuendelea kunawa na kutumia vitakasa mikono ili kuepuka maambukizi ambayo yanaweza kuathiri maisha yao.

Aidha Dkt. Mahenge amesema kwamba kikao  kazi hicho kimelenga kutathmini zoezi la utoaji wa chanjo ya korona mkoani hapo Janssen katika awamu ya kwanza na kuangalia namna ya uendeshaji wa zoezi la pili kwa uharaka zaidi.

Amesema kwasasa mkoa unaendelea na utoaji wa chanjo aina ya sinopham japo mwitikio bado  haujawa mzuri hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kupata chanjo hizo ili kujiepusha na athari za ugonjwa wa UVIKO 19.

No comments:

Post a Comment