Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Binilith Mahenge amewataka vijana kutumia teknolojia ya mitandao ya simu kutafuta masoko ya bidhaa zao badala ya kutegemea Serikali kufanya kila kitu.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi wa ufugaji wa nyuki wa kisasa katika kanisa la Anglikana Muhala unaomilikiwa na vijana wa Wilaya ya Manyoni chini ya shirika
la Compassion International Tanzania Dkt.
Mahenge amesema yapo mataifa ambayo yanauitaji mkubwa wa asali, mbuzi na ng’ombe lakini hawajaweza kupata kwa utoshelevu kwa
kuwa biashara imekuwa haifanyiki ki kamilifu.
Dkt. Mahenge amewataka vijana kuhakikisha kwamba wanatumia
simu uwepo wa simu na mitandao ya kijamii kwa lengo la kuuza na kununua bidhaa
mbalimbali
Amesema Serikali imetumia fedha nyingi kuwekeza miundombinu
mbalimbali ikiwemo mkongo wa taifa ili kundi
la vijana lipate kufaidika kupata soko na marifa mapya ya ki biashara.
Aidha amewataka vijana kulinda miundombinu pamoja na miradi
wanayotafutiwa na mashirika mbalimbali pamoja na Serikali ili kufikia lengo la
kumkomboa kijana na wanakwake kwa ujumla.
Dkt. Mahenge amebainisha kwamba Serikali inatekeleza sharia inayozitaka
Halmashuri kutenga asilimia kumi (10%) kwa ajili ya vijana na asilimia 40 % kwa
ajili ya wanawake na walemavu hivyo kumtaka Mkurungezi wa Halmashauri ya Manyoni
kuhakikisha kwamba asilimia hiyo inatumika kuendeleza vijana wilayani hapo.
Naye Afisa vijana wa Mkoa wa Singida Bwana Fredrick Ndahani pamoja
na kumshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuzindua mradi wa vijana hao na kuwakabizi
vitendea kazi mbalimbali vikiwemo Pikipiki
na mizinga vyenye thamani ya
shilingi milioni 80.4 amezishukuru Taasisi za dini kwa kuwajali na kuwasaidia
vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa.
Hata hivyo Bwana Ndahani amewaomba viongozi hao kuendelea kutumia rasilimali
walizonazo kuendelea kuwasaidia vijana.
Mwisho amewataka vijana kuendela kuwa waaminifu ili
waweze kuaminiwa na kusaidiwa na jamii
inayowazunguka.
Aidha mbali ya uzinduzi wa mradi wa vijana hao mkuu wa mkoa
ametembelea mradi wa ujenzi wa
zahanati ya maweni, shule ya msiningi
sayuni na shule ya sekondari ya Mlewa.
No comments:
Post a Comment